Author: Geofrey Stephen

Na Doreen Aloyce,Dodoma Spika wa Bunge dkt Tulia Akson ameishukuru Bank ya Nmb kwakutambua umuhimu wa ibada ya kufunga kwakushiriki Iftari na wabunge pamoja na watumishi wa Bunge jambo ambalo linadumisha Upendo,Amani na mshikamano pande zote mbili. Pia ameipongeza benk hiyo kwa kazi wanazofanya kama vile kurudisha faida kwa wateja kwakuchangia shughuli mbalimbali kama vile sekta ya elimu, afya na upandaji miti milioni moja nchi nzima. Akizungumza katika viwanja vya Bunge wakati wa iftari iliyoandaliwa na bank ya nmb Dkt Tulia amesema kupitia iftari hiyo wamesikia mipango mbalimbali iliyofanywa na inayoendelea kufanywa na bank hiyo kwaajili ya kuleta maendeleo katika…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma SERIKALI kupitia Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini Mkataba wa upanuzi wa mkongo wa Taifa na mawasiliano katika wilaya 23 unaogharimu takribani Bilioni 37.4. Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa Mradi huo unalenga kumaliza changamoto za mtandao katika wilaya hizo. Amesema kuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imepanga kutekeleza mradi wa kuimarisha mawasiliano katika ngazi ya Wilaya kwa kuunganisha Wilaya zote kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa mawasiliano ambayo yatachochea maendeleo katika Wilaya hizo, sambamba…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza katika utekelezaji wa miradi nane ya Redgrow yenye thamani ya sh, bilioni 157.2. Mradi huo unalengo la kutangaza vivutio vya utalii katika mikoa ya kusini utakapokamilika na umegawanyika katika makundi mawili yenye⁰01qz maeneo manne,manne ikiwemo uboreshaji wa viwanja vya ndege. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mikataba nane ya ujenzi wa majengo ya utalii,ujenzi wa viwanja vya ndege aliisisitiza hatasita kuwachukuliwa hatua wakandarasi watakaopewa kazi ya kujenga vivutio hivyo na majengo kwani mkataba huo umecheleweshwa kwa zaidi ya miaka minne. Alisema…

Read More

Na Wandishi wa A24tv .SIMANJIRO Mashahidi 24 wa Jamhuri wanatarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya shambulio na kukaidi amri ya Wizara ya Madini inayomkabili Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Jiji la Arusha Joel Saitoti pamoja na Wafanyakazi wake sita wa mgodi wa Gem and Rock Venture uliopo Mererani. Mwishoni mwa wiki katika mahakama ya wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, washtakiwa hao walisomewa maelezo ya awali baada ya kubadilishiwa mashtaka katika tukio lililotokea marchi 13 mwaka huu katika mgodi uliopo kitalu B unaomilikiwa na kampuni ya Gem & Rock Venture. Akisoma maelezo ya awali katika kesi ya shambulio inayowakabili washtakiwa…

Read More

Na Geofrey Stephen .Arusha CHAMA Cha wafanyabiashara, wenye viwanda na Kilimo TCCIA mkoa wa Arusha wamelalamikia Kodi ya huduma(service levy) inayotozwa na Halmashauri ambayo imepanda kutoka 0.03 hadi kufikia 0.3 jambo ambalo wamesema ni ongezeko kubwa. Wakizungumza katika kikao Chao na mkurugenzi wa Jiji la Arusha mkoani hapa walisema ongezeko la Kodi katika biashara ni maumivu kwao na wakati mwingine inapelekea wafanyabiashara kufilisika na kushindwa kuendesha biashara zao. Mwenyekiti wa Chama hicho Walter Maeda alisema hawakatai Kodi hiyo ila wanaomba Halmashauri kuwapunguzia angalau ifike kwenye 0.1 lakini siyo 0.3 inakuwa mzigo mkubwa kwao na Kwa kuwa serikali ilitoa agizo Kwa…

Read More