Author: Geofrey Stephen

Mwandishi wetu,Monduli Monduli.Mkuu wa wilaya ya Monduli,Joshua Nassari amewataka wakazi wa Monduli kupunguza idadi ya mifugo yao, Ili kutoathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yanaendelea kupunguza malisho ya mifugo yao. Amesema wafugaji hao wanapaswa kuuza sehemu ya mifugo Ili kusomesha watoto badala ya kuwaacha wachungani. Wafugaji wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,mwaka 2021/22 walipata hasara ya sh 18.3 bilioni baada ya mifugo yao 127,786 kufa kutokana na ukame ambao umesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi. Licha wa wafugaji kupata hasara hiyo,pia serikali wilaya ya Monduli, ilipoteza Kodi na tozo kiasi cha sh 487.3 milioni ambazo zimekusanywa katika minada…

Read More

Na Mwandishi wetu. Mradi wa afya ya macho katika mikoa ya Morogoro na Singida umeonyesha kuwa kuna uwezekano wa kuepuka upofu unao zuilika nchini Tanzania. Mnamo 2022, ilikadiriwa kuwa watu milioni 8.2 nchini walipoteza uoni na bila juhudi za makusudi, idadi hii inaweza kuongezeka (ripoti ya IAPB, 2020). Boresha Macho, ni mradi wa afya ya macho uliosimamiwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Sightsavers, uliolenga kurejesha na kulinda uoni kwa kutoa huduma ya afya macho kwa makundi yote yakiwemo, wazee, watu wenye ulemavu na wasio na ulemavu. Ukifadhiliwa na serikali ya Uingereza kupitia UK Aid Match na kutekelezwa na…

Read More

Na Geofrey Stephen Monduli ARUSHA KUMBUKIZI ya miaka 39 ya Hayati Moringe Sokoine aliyefariki kwa ajali ya Gari mwaka 1984 imefanyika leo katika kanisa  Katoliki Parokia ya Emairete Kigango cha Engwikie Monduli Juu Wilayani Monduli huku viongozi wa dini wakikemea rushwa ,ufisadi na kuhimiza kuyaenzi mema ya Marehemu Paroko wa kanisa hilo,padri,Arnold Baijukie alisema kuwa hayati Edward Sokoine alikuwa ninkiongozi aliyeacha alama aliyepinga  masuala ya rushwa ,wizi wa mali za umma ikiwemo uhujumu uchumi. Akiongoza ibada ya kumbukizi ya kifo cha Sokoine,Paroko Baijukie, alisema lengo la  kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha  marehemu Sokoine kilichotokea Aprili 12,1984 ni alama aliyoiacha katika…

Read More

Mwandishi wetu,Mwanza. Chama Cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) kimetangaza kushirikiana na Kituo Cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) kuwasaidia wafanyakazi 195 wa kampuni ya Sahara Media kudai kulipwa malimbikizo ya madai ya mishahara yao kiasi cha sh 3.5 bilioni. Uamuzi huo,umetangazwa Jana na Mwenyekiti wa JOWUTA Taifa,Mussa Juma na Mjumbe wa bodi ya udhamini wa JOWUTA,Mutta Robert katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa chama cha ushirika Nyanza.baada ya kukutana na pande zote katika mgogoro huo. Juma amesema baada ya majadiliano baina ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na ofisi ya Idara ya kazi mkoa…

Read More