Author: Geofrey Stephen

Ikiwa leo ni ijumaa kuu kwa wakristo kote nchini kanisa la Kkkt Usharika wa Salei Jijini Arusha umeadhimisha ibada iyo kwa vijana kufanya igizo la mateso ya Yesu live kuanzia Mwanzo mpaka mwisho A24Tv ilikua ibadani hapo kufuatilia matukio yote na hapa ni picha za matukio ya igizo la bwana  Yesu Bwana Yesu wakati wa igizo akiwa amepanda mwana Punda tayari kwa safari ya kuelekea Yerusalem  Picha za igizo la bwana Yesu akiwa ameingia mji wa Yerusalem akiwa na wanafunzi wake na kuanza kuwafundisha masomo gafla wazee wa baraza waka mvamia katika mafundisho yake. Wazee wa Baraza wakimuuliza yesu…

Read More

Na Geofrey Stephen .Arusha Vijana wabunifu wameagizwa kutengeneza bidhaa zenye mahitaji sokoni ili kuwa na ubora zaidi utakaowawezesha kupata masoko na kuweza kujiajiri katika soko la ndani . Agizo hilo limetolewa katika Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) na Meneja wa Shirika la Viwanda Vidogo(Sido) ,Jafari Donge wakati wa kufunga mafunzo ya wiki ya ujasiriamali na ubunifu yaliyofanyika chuoni hapo. Alisema vijana wengi wanatengeneza bidhaa mbalimbali na serikali inatoa fedha kwaajili ya kuendeleza bunifu zao hivyo ni vema sasa wabunifu vijana wakatengeneza bunifu zenye mahitaji sokoni ili kujikwamua kiuchumi. Alisema Sido na chuo hicho wanashirikiana katika kuhakikisha wabunifu wanatumia ziatamizi vilivyopo…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Sabaya achiwa huru mama yake mzazi amwaga machozi nje ya mahakama ALIYEWAHI kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, leo April 5, 2023 ameachiliwa huru na mahakama baada ya kufutiwa mashtaka saba yaliyokuwa yakimkabili, ikiwemo uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya madaraka na kuongoza genge la uhalifu. Mahakama imetoa uamuzi wa Lengai Ole Sabaya kulipa kiasi cha shilingi milioni 5 kama fidia kwa mwathirika na hapaswi kufanya kosa lolote la jinai kwa muda wa mwaka mmoja. Sabaya ambaye mapema asubuhi ya leo alifika kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Moshi, kabla uamuzi wa kuachiwa…

Read More

Na Geofrey Stephen ,Arusha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Arusha wamemchagua Namelok Sokoine kuwa Mwakilishi wa Mkoa huo katika nafasi ya NEC Mkoa Kuwasilisha Chama hicho Taifa. Akitangaza Matokeo hayo,Waziri Mkuu Mtaafu,Mizengo Pinda alimtakaza Sokoine kwa kuongoza na kupata kura 39 na kumwangusha mpinzani wake wa karibu Mfanyabiashara Hussein Gonga aliyeambulia kura 16. Pinda alisema kuwa wajumbe waliopiga kura walikuwa 67 na nafasi ya tatu Daniel Palangyo aliyetetea nafasi ya NEC kwa kupata kura 5,nafasi ya Judith Mollel alipata kura 3,Elibahati Lowassa na David Lemilla walioambulia kura 2 na wagombea wengine Novatus Makunga,Prf Samweli Ilila…

Read More

Mwandishi wetu Shirika la wanahabari la kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) limegawa vitabu vya maarifa ya asili katika utunzwaji wa Mazingira, vyanzo vya maji na misitu kwa wakurugenzi wa mashitaka yasiyo ya kiserikali nchini. Wakurugenzi wa mashirika hayo na ambao ni wanachama wa Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu (THRDC) walitembelea MAIPAC kujifunza Utendaji wake. wakurugenzi na wawakilishi wa Mashirika hayo,waliongozwa na Mkuu wa Dawati la Wanachama la THRDC,Lisa Kagaruki . Wawakilishi wa mashirika hayo,licha ya kutembelea MAIPAC pia waliweza kupatiwa vitabu vya maarifa ya asili katika utunzwaji wa Mazingira, vyanzo vya maji na misitu ambavyo vimeandaliwa na MAIPAC…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Kaya zaidi ya 15 katika eneo la Tanganyika pekazi kata ya Moshono jijini Arusha, zimekumbwa na maji ya mvua yaliyojaa ndani ya nyumba zao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini hapa. Wakiongea na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo,baadhi ya wananchi hao akiwemo balozi wa eneo hilo,Nicolas Kivuyo na Elisifa Zabron wamedai kwamba athari hiyo imekuja mara baada ya jeshi la wananchi kambi ya Tanganyika pekazi kuweka tuta na kuziba mkondo wa maji hali iliyosababisha maji hayo kuelekea kwenye makazi yao huku wakimtuhumu diwani wao Miriamu Kisawike kushindwa kuwasaidi huku akiwajibu majibu yasiyofaa. Aidha…

Read More