Author: Geofrey Stephen

Na John Walter-Manyara Serikali na wadau wa Kampeni ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania ( SMAUJATA) wilaya ya Babati mkoani Manyara wamesema familia zikiamua kuacha kusuluhisha Kinyumbani vitendo vya ukatili wa kijinsia, tatizo hilo litapungua na hatimaye kumalizika kabisa. Utafiti unaonesha kwamba asilimia 60 ya ukatili kwa watoto  unafanyika nyumbani ambapo ndugu na jamaa wa karibu wanatajwa kuhusika na asilimia 40 nje ya familia ikiwamo mashuleni. Viongozi hao wamezungumza hayo katika Kata ya Dareda wilayani Babati mkoani hapa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Familia Duniani inayofanyika kila mwaka Mei 15. Afisa Ustawi wa Jamii mkoa…

Read More

Na John Walter-Manyara KAMPENI Naibu waziri wa Katiba na Sheria Paulina Gekul amewataka wanasheria na wasaidizi wa sheria kutumia uwezo wao na maarifa waliyonayo kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukatili na wahitaji wengine kupata haki zao. Ametoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo maalum kwa Mawakili na wasaidizi wa kisheria mjini Babati ikiwa ni mwendelezo wa  Kampeni ya Mama Samia Legal Aid  yenye lengo la kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu masuala ya kisheria na haki za binadamu lakini pia ukatili wa kijinsia. Amesema vitendo vingi vya ukatili vinafanyika na kesi zake kumalizwa kinyumbani jambo ambalo sio sawa kwa kuwa walitendewa ukatili…

Read More

TAHARUKI MGOMO WA MADAKTARI HOSPITALI YA SELIAN, UONGOZI WADAI HAKUNA MGOMO NI UVUMI TU ‘WANACHAPA KAZI’ May 15, 2023 Na Joseph Ngilisho Arusha TAHARUKI imewakumba wagonjwa katika hospitali ya SELIAN Lutheran (ALMC) ya jijini Arusha,kufuatia taarifa za kuwepo kwa mgomo wa madaktari wakiwemo mabingwa wa magonjwa mbalimbali. Wafanyakazi hao wanadaiwa kugoma kama njia mojawapo ya kushinikiza kulipwa madai yao ya malimbikizo ya mishahara . Hata hivyo uongozi wa hospitali hiyo kupitia mch. Godwin Lekashu na Mkurugenzi wa tiba ,dkt.Frank Madinda umekanusha madai hayo na kusema ni uvumi wa mtaani na Madaktari wote wapo kazini. MCH.LEKASHU “Hapa hakuna mgomo, madaktari…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Leo Tarehe 15.05.2023 saa 4Asubuhi Shauri No. 21 ya Mwaka 2022 kuhusu Maombi ya Mapitio ya Sheria (Judicial Review Application) dhidi ya Tangazo la Waziri wa Mali asili na Utalii (GN no 421 ya tarehe 17 Juni 2022 kuhusu ardhi ya Vijiji vya Loliondo kuwa Pori Tengefu la Pololeti ,linakuja kwa ajili ya Maamuzi madogo mbele ya Jaji Tiganga. Katika shauri hilo Waleta maombi Watano kutoka vijiji vilivyoathirika wanaomba Mahakama: 1) Iagize Serikali kuondoa zuio dhidi ya Wananchi kuingia kwenye eneo la Km2 1502 ambalo wamekuwa wakitumia kwa ajii ya malisho ya mifugo yao na…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Mamlaka ya udhibiti wa Usafiri wa Ardhini na Majini LATRA Imesisitiza kutokuwepo kanuni mahsusi zinazoonyesha utaratibu wa huduma za kintandao kama tiketi mtandao na mfumo wa ufuatiliaji wa mwendo vyonbo vya Usafirishaji kunaleta mkangwnyiko wa kushindwa Kutoa adhabu. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Imesisitiza kuwa maoni ya wadau wa Usafirishaji ni muhimu Kwa lengo la utekelezaji wa majukumu ua shughuli za LATRA. Akiongea  Mkurugenzi Msaidizi huduma za Usafirishaji wa Barabara Andrew Magombana wakati akifunga kikao cha wadau wa Usafirishaji kujadili mapendekezo ya kanuni mpya zilizoandaliwa chini ya Sheria ya LATRA…

Read More