Author: Geofrey Stephen

Na mwandishi wa A24Tv Kibaha . Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk. Ashatu Kijaji (Mb.) amekitaka Kiwanda cha kutengeneza viuadudu (TBPL) kuhakikisha kinajitangaza ndani na nje ya nchi ili kuongeza wigo wa masoko kwa kuuza bidhaa hiyo ya kipekee ambayo inazalishwa hapa nchini. Dk. Kijaji ameyasema hayo Machi, 29, 2023 alipotembelea kiwanda hicho kilichoko Kibaha Mkoani Pwani kushuhudia namna uzalishaji wa dawa za viuadudu unavyofanyika kiwandani hapo. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na wajumbe wengine wakipewa maelezo na Jovin Magayane (mwenye koti jeupe), Mtaalam wa Maabara wa Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) namna…

Read More

Na Geofrey Stephen ,Arusha Hatimaye mgomo wa siku mbili wa Wafanyakazi wa kampuni ya kufua Vyuma na kutengeneza matanki ya maji ya Lodhia Group ya Jijini Arusha waliogoma kushinikiza  kudai masilahi kilio chao kimesikilizwa na uongozi wa kampuni hiyo kuongeza mshahara na nyongeza za malipo ya masaa ya ziada kwa wafanyakazi wake . Awali wafanyakazi zaidi ya 700 wa Kampuni hiyo waligoma kufanya kazi kwa siku mbili kwa madai ya mshahara kuwa mdogo sana wa shilingi 150,000 hautoshi ,vitendea kazi hakuna,kudhalilishwa kwa matusi ya nguoni na uongozi wa juu hatua iliyofanya Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Felician Mtehengerwa kuingilia kati na …

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina yake na Marekani na inawakaribisha wawekezaji kutoka nchini humo kuja kuwekeza na kushirikiana na watanzania katika ufanyaji biashara katika sekta mbalimbali nchini. Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya nchi hizo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Michael Battle Machi 27, 2023 katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam. Aidha, Waziri Kijaji ameiomba…

Read More

Na Mwandishi wetu, Kigoma. Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amemuhakikishia mwekezaji wa kiwanda cha TROLLE MEES LE TANZANIA IVS LTD soko la uhakika la mafuta ya mawese baada ya kuanza utekelezaji wa kutatua changamoto zilizojitokeza kwenye ziara ya Mhe Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Mhe Kigahe ameyasema hayo Mkoani Kigoma wakati wa kupokea taarifa ya kamati ya kufanya tathimini ya changamaoto zilizojitokeza katika kuongeza thamani ya zao la mchikichi mkoani Kigoma. Akiwa mkoani Kigoma mnamo tarehe 27 February ,2023 Mhe. Waziri Mkuu alipokea changamoto anuai kutoka kwa mwekezaji anajenga kiwanda cha kuchakata na kuongeza thamani…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv .Mirerani Kamati Maalumu ya Wataalamu wa Ramani Mgodini kutoka Chuo Cha Madini Dodoma imemamliza Mgogoro kati ya Kampuni ya Franone na Gem & Rock Venture na kusema kuwa madini kilo 4 yalichimbwa mita 650 ndani ya Mgodi wa Kitalu C unaomilikiwa na serikali na mwekezaji Mzawa Onesmo Mbise kinyume na sheria ya madini. Mbali ya hilo Kamati imebaini katika uchunguzi wake kuwa mageti yaliyowekwa na Kampuni ya Gem & Rock Venture inayochimba mgodi kitalu B inayomilikiwa na Mkurugenzi Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti yaliwekwa ndani ya Mgodi wa kitalu C eneo ambalo kampuni ya…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amewakaribisha wawekezaji wenye nia kutoka India kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali hususani viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba, uchumi wa bluu na viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo kama Parachichi na Mbaazi zinazohitajika kwa wingi katika soko la India. Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Tanzania na India na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan Machi 27, 2023 katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam. Katika…

Read More

Na. Salim Bitchuka Imeelezwa kuwa muamko mdogo wa vijana katika fani ya ubaharia ndio chanzo kinachopelekea taifa la Tanzania kutokuwa na Mabaharia Vijana wa kutosha. Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na mkurugenzi wa huduma za Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Rajabu Mabamba wakati wa hitimisho la mafunzo kwa walimu wa Mabaharia nchini Akimuwakilisha mkurugenzi wa TASAC, Mabamba alisema muamko umekuwa ni mdogo kwa vijana kutokana na kukosa kutengenezewa ufahamu wa kutosha kuhusu fursa zipatikanazo katika eneo hilo. “Kwa kutambua kuwa nchi kama nchi wakati tukielekea uchumi wa Buluu kwa kushikiana na DMO tuligundua kwamba kulikuwa…

Read More