Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha . Asasi zisizo za kiraia nchini zimetakiwa kuangalia namna ambavyo wataweza kujitegemea katika kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuendelea kujenga uelewa wa kutosha katika kuchochea uboreshaji katika shughuli za kijamii. Hayo yamesemwa  mkoani Arusha na Mwenyekiti wa bodi ya AZAKI ,Mercy Silla wakati akifunga wiki ya AZAKI iliyokuwa ikiendelea  kwa muda wa wiki moja mkoani Arusha. Silla amesema kuwa, kukutanisha asasi hizo wiki nzima wameweza kujadili maswali mbalimbali ya kuboresha katika utendaji kazi sambamba na kujifunza zaidi kutoka kwa wenzao wa nje ya nchi. Amefafanua kuwa,ni wajibu wao kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele ili…

Read More

Na Mosses Mashala. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendeleza juhudi za kuimarisha Michezo kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana. Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 14 Sept 2024 katika Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kushuhudia Fainali ya Michuano ya Yamle Yamle kati ya timu ya Ponchinki City na Wete City. Aidha Rais Dk.Mwinyi amelitaka Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kuendelea kuimarisha Michuano hiyo ambayo sasa imekuwa na sura ya kitaifa na kuunga Mkono kila Mwaka. Katika Mchezo huo wa Fainali timu ya Ponchink City imeibuka na…

Read More

Na Prisca Libaga Arusha Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa niaba ya Kamishna Jenerali tarehe 13.09.2024 imeteketeza kwa mujibu wa sheria vielelezo vya dawa za kulevya aina ya mirungi kilogramu 23.74 zilizokamatwa katika operesheni zilizotekelezwa hivi karibuni. Uteketezaji wa vielelezo hivyo ulifanyika katika dampo la Murieti jijini Arusha. Zoezi hilo limeshuhudiwa na wawakilishi kutoka Mahakama ya Wilaya Arusha, Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Arusha, Ofisi ya Mkemia Mkuu Arusha kulingana na Matakwa ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Mwisho.

Read More

Na. Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo, leo Septemba 13, 2024 wamechangia damu kwa wagonjwa wenye uhitaji na kufanya mazoezi ya kutembea katika Jiji la Arusha. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Debora Lukololo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetumia maadhimisho hayo kuwakumbuka wagonjwa kwa kuchangia damu kwa wale wenye uhitaji lakini pia kufanya matembezi ya hiari kwa kushirikiana na Wananchi kwa lengo la kufikisha ujumbe kuhusiana na masuala ya uhalifu. ACP Lukololo ameendelea kufafanua kuwa…

Read More

Bahati Siha, Mahakamani ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro September 12 mwaka huu,imemuhukumu kwenda jela Mkazi wa Majengo SanyaJuu Wilayani humo,Issa Chando( Meleki) (53),mkulima kutumikia kifungo cha Maisha kwa kosa la kubaka watoto wa miaka (6) wakazi wa Majengo Mwendesha mashitaka wa Serikali Kurwa Mungo mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama hiyo Jasmine Abdul amesema tukio hilo lilitokea January mwaka huu kwa nyakati tofauti likifanyika nyumba kwa mshitakiwa “Ni kweli alikuwa akiwaingiza kwa wakati mmoja kwenye nyumba yake nakuwafanyia ukatili huo uku alifahamu kufanya hivyo ni kosa”amesema Kurwa Akielezea kwa undani kuhusu tukio hilo amesema siku moja wakati mzazi…

Read More

GEofrey Stephen  ARUSHA MTANDAO wa Watetea wa haki za binadamu Tanzania(THRDC)umeomba kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuzungumzia hatima ya masuala ya utekaji na ukatili yanayoendelea nchini pamoja na kumkumbusha mikataba ya kimataifa ya kupinga ukiukwaji wa haki za binadàmu. Akiongea na vyombo vya habari katika mkutano mkuu wa 13 wa wanachama wa mtandao THRDC unaoendelea katika wiki ya AZAKI jijini Arusha, mratibu wa Taifa wa Mtandao wa kutetea haki za Binadamu, Onesmo Ole Ngurumwa alisema mkutano huo umelenga kuangazia masuala mbalimbali ikiwemo kupitia na kuidhinisha taarifa ya nusu muhula ya hali ya haki za binadamu ,utekelezaji…

Read More

Na Bahati .Siha Mashindano ya West Champion Ligi yanatarajiwa kufikia tamati September 15 mwaka huu katika uwanja wa kilima hewa Matadi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Timu zitakazo cheza Fainali hiyo ni Timu ya Roseline kutoka West Kilimanjaro Wilayani humo na timu ya Kware fc kutoka Wilayani Hai mkoani hapa Ambapo mgeni rasmi atakuwa Antony Mallya mdau mkubwa wa maendeleao Wilayani humo, mashindi wa tatu mechi yao itachezwa September 14 Mwaka huu, kati timu ya Nafco na Zinduka Fc kutoka Wilaya Siha. Eli Pius mwanzilishi wa lig hiyo Akizungumza na waandishi wa habari,amewataka Wananchi Wilayani humo, kujitokeza kwa wingi kwenye…

Read More