Author: Geofrey Stephen

Na John Mhala,Mirerani Meneja wa Mgodi wa Gem & Rock Venture,Joel Mollel Maarufu kwa jina la Saitoti ametiwa mbaroni na wenzake 21 na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kwa tuhuma za kuongoza genge la Wachimbaji wadogo wadogo maarufu kwa jina la Wana Apollo na kuvamia kinyemela ndani ya mgodi wa madini ya Tanzanite uliopo Kitalu C katika Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro. Mgodi wa Kitalu C unaochimbwa kwa ubia kati ya Serikali na mwekezaji mzawa Onesmo Mbise ulivamiwa marchi 12 mwaka huu majira ya kati ya saa 6.30 na saa 8 mchana na kundi hilo wakiwa na silaha za jadi…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutoa elimu nchini. Waziri Mkenda ametoa wito huo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa huduma ya mkopo wa Elimu inayotolewa na Benki ya NMB. Amesema kinachofanyika na Benki ya NMB ni kuonyesha njia kwa kuwa pamoja na kuanzisha mkopo wa elimu wamekuwa wakitoa ufadhili wa masomo ambapo kwa mwaka huu wamenufaisha wanafunzi 100. “Mwaka jana Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB alikuja ofisini kwangu akasema tunataka kuunga mkono juhudi za Serikali na tunachagua eneo ambalo Mhe Rais ameelekeza…

Read More

Na John Mhala,Mirerani Kikundi cha Wachimbaji Wadodo Wadogo zaidi ya 30 kutoka katika kampuni ya Gem$ Rock Venture Unaomiliki Mgodi Tanzanite Kitalu B  jana mchana wakiwa na silaha za jadi na majabali yenye ncha kali  wamevamia Mgodi wa Kitalu C na kujeruhi zaidi ya wafanyakazi kumi na wafanyakazi hao wako katika hali mbaya na wamekimbizwa hospital wakiwa mahututi. Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara,Kamishina Msaidizi wa Polisi,George Katabazi na alisema kuwa baadhi ya watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi hilo. Katabazi alisema ni kweli tukio hilo limetokea juzi mchana majira ya kati ya saa 6.30 hadi saa 8…

Read More

Na Geofrey Stephen Manyara . Kundi la wafaransa 20 wamejitolea madawati 30 na viti na meza 20 kwa ajili ya shule ya msingi Saniniu Laizer iliyopo kijiji cha Naepo Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, iliyokuwa na upungufu wa samaini hizo. Mmoja kati ya wafaransa hao Jean Claude Petit akizungumza baada ya kukabidhi samani hizo amesema wao hujihusisha na masuala ya madini ikiwemo usonara hivyo wakaamua kutoa msaada huo. “Tulifika kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite tukasikia sifa za bilionea Saniniu Laizer kujenga shule na kuikabidhi serikali hivyo tukaamua kuisaidia madawati, viti na meza hizo,” amesema Petit. Amesema wana uzoefu wa sekta…

Read More

Doreen Aloyce, Dodoma KUFUATIA kuwepo kwa taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii hususan Twitter na Instagram kuhusu malalamiko dhidi ya shirika la uwakala wa Meli Tanzania (TASAC )kuvunjwa Mikataba ya mafunzo kazi kwa vijana zaidi ya 400 bila kufuata utaratibu na ikiwa imebaki muda wa mwaka mmoja kuisha kwa mikataba hiyo Shirika limekanusha taarifa hizo na kutolea ufafanuzi. Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma ukumbi wa Idara maelezo ,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,Kaimu Mkeyenge ameeleza malalamiko hayo hakiwemo vijana hao kudai kufanya kazi bila bima ya afya, mikataba na kwamba TASAC ilitoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi…

Read More

Na Geofrey Stephen Manyara Kundi kubwa la watalii wapatao 17 kutoka nchini Ufaransa wametembelea mgodi wa kuzalisha madini aina ya Tanzanite katika mgodi wa kitalu C unaomilikiwa na  kampuni ya Franone Mining iliyopo  wilayani Simanjiro Mkoani Manyara . Kundi hilo ambalo  ndani yake wapo wataalamu wa kukata na kuongeza thamani ya madini pamoja na wanafunzi wa kuongeza thamani ya madini  wamesema wamefurahia kuona sehemu pekee inayochimbwa madini ya Tanzanite mkoani Manyara. Kundi la watalii kutoka nchini Ufaransa wakisikiliza kwa makini namna uzalishani wa madini ya Tanzanite yanavyo zalishwa katika mgodi wa kisasa wa kitalu C unaomilikiwa na kampuni ya mzawa…

Read More