Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv . Waziri wa kilimo Nchini Husein Bashe ameagiza kukamatwa kwa Mshindo Mbete msola Meneja mauzo kampuni ya mbolea ya Minjingu na Meneja wa kanda wa nyanda za juu kusini wa mamlaka ya kudhibiti mbolea Tanzania TFRA baada ya kukamatwa kwa mifiko 776 ya mbolea iyojazwa mchanga tayari kwa kuwauzia wakulima Njombe. Kamati ya Ulinzi na usalama Mkoa wa Njombe wamefanikiwa kukamata shehena hiyo ya mifuko 776 uliyo jazwa mchanga mithili ya mbolea ya minjingu tayari kwa kuwauzia wakulima mkoa wa Njombe. Mshindo Msolwa ambaye Meneja mauzo wa mbolea za Minjingu ni miongoni mwa viongozi walio agizwa…

Read More

Na John Walter-Manyara Kufuatia kuanza ugawaji mahindi ya msaada wilayani Babati mkoani Manyara  ili kupunguza makali ya njaa kutokana na upungufu wa chakula kwa wananchi uliosababishwa ukame, mfanyabiashara mmoja  mkoani hapa, anadaiwa kushikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa na mifuko 42 yenye ujazo wa  kilo hamsini kwa kila mfuko. Hayo yamesemwa na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kata ya Maisaka  ambapo wamesema taarifa hizo walizipata kutoka kwa raia wema ambapo baada ya kufuatilia wakiwa na polisi walikuta mahindi hayo kwenye nyumba ya mwananchi mmoja  eneo la Changarawe majira ya saamoja Usiku Machi 4,2023. Katibu wa CCM kata ya Maisaka…

Read More

Makao Makuu ya Tanzania Labour Party yalioko Magomeni usalama.  Wanachama wa chama cha Tanzania Labour Party wanatarajia kumpata mwenyekiti mpya atakaye kiongoza chama hicho mpaka mwaka 2025 kabla ya mkutano mkuu kufanyika Rasmi kumpata mwenyekiti Mpya Uchaguzi huo utafanyika kesho tahe 06 mwezi wa 3 mwaka huu wa 2023 mara baada ya aliyekua mwenyekiti wa Tlp Mh Mrema kufariki Dunia mwaka jana mwezi wa nane 2022 uchaguzi huo unatarajia kutafanyika katika ukumbi wa mikutano ya Hotel ya Lego Hotel iliopo Sinza Jijini Dar es Salaam kuanzia majira saa tatu Asubui. Wanachama kutoka Mikoa yote Tanzania bara na Visiwani zaidi…

Read More

Na Geofrey Stephen  Longido ,Arusha Watumishi 12 wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido Mkoani Arusha wametakiwa kukaa pembani kupisha uchunguzi wa tuhumiwa ya  ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 150 wakiwemo wakuu wa idara nne ambao tayari wametelemshwa vyeo. Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi{CCM} iliyosomwa na Katibu Mwenezi wa Chama, Solomoni Lekui na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Saimon Oitesoi ilisema kuwa hatua hiyo ni kufuatia taarifa ya ukaguzi ya mwaka 2021. Lekui aliwaeleza waandishi Habari kuwa mbali ya ubadhilifu watumishi hao walikuwa wakifanya mambo kinyume na utaratibu na kutumia vibaya madaraka yao…

Read More

Na Mwandishi wetu Vurugu zimezuka katika Kijiji cha Engikaret Wilayani Longido Mkoani Arusha baada ya wananchi 10 kukamatwa kwa madai kuwa walikuwa wakizuia wataalamu wa mradi wa umeme wa KV400 unaotoka Mkoani Singida hadi Mji wa Namanga kufanya kazi kwa madai kuwa mradi huo umepita katika maeneo yao ambayo hadi sasa hawajalipwa fidia ya shilingi bilioni 1.8 zilizotolewa na serikali. Akizungumza kwa simu ya kiganjani na mwandishi wa gazeti hili,Thomas Mollel alisema kuwa wananchi hao kweli walifanya hivyo kwa kuwa eneo linalopita mradi ni mali yao na sio mali ya kijiji kama inavyotangazwa na baadhi ya viongozi wa serikali…

Read More