Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv . Kaya zaidi ya 15 katika eneo la Tanganyika pekazi kata ya Moshono jijini Arusha, zimekumbwa na maji ya mvua yaliyojaa ndani ya nyumba zao kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini hapa. Wakiongea na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo,baadhi ya wananchi hao akiwemo balozi wa eneo hilo,Nicolas Kivuyo na Elisifa Zabron wamedai kwamba athari hiyo imekuja mara baada ya jeshi la wananchi kambi ya Tanganyika pekazi kuweka tuta na kuziba mkondo wa maji hali iliyosababisha maji hayo kuelekea kwenye makazi yao huku wakimtuhumu diwani wao Miriamu Kisawike kushindwa kuwasaidi huku akiwajibu majibu yasiyofaa. Aidha…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha kesi ya kulazimishwa kupotea Mzee Oriais Oleng’iyo mkazi wa  Ololosokwani tarafa ya Loliondo itajulikana Mei 10,2023. Mahakama Kuu ya Tanzania,Masijala ya  Arusha, Leo imesikiliza maombi madogo yaliyoletwa na Ndoloi Oriais ambaye kupitia Mawakili wake imewataka  wajibu maombi kwa ujumla wao kumleta, kumuachilia au kusema popote alipo Mzee Oriais Pasilange Oleng’iyo(85). Wajibu maombi ni pamoja na Kamanda wa jeshi la polisi (RPC), Mkuu mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya na OCD Ngorongoro, Mkuu wa jeshi la polisi(IGP) na Mwanasheria Mkuu wa serikali. Mbele ya Jaji Mohamed  Gwae,Wakili wa mleta maombi, Saimon Mbwabwo aliieleza kuwa Juni 9,2022 huko…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Mazingira ya Biashara cha Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw. Baraka Aligaesha amewashauri Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kutangaza na kielimisha umma kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini (MKUMBI) . Bw. Baraka ameyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu utekelezaji wa MKUMBI na mafanikio yake katika Kikao Kazi cha 18 cha Maafisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) Machi 29, 2023 JNICC jijini Dar es Salaam. Akiongea na Maafisa hao, amesema ni jukumu la kila Afisa Mawasiliano na Uhusiano Serikalini kutangaza na kuelimisha umma kuhusu maboresho yanayotokea…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma SHIRIKA La Umeme Tanzania (TANESCO), limezindua Programu ya Mpango wa miaka minne wa jinsia wenye lengo la kutatua changamoto za wanawake katika maeneo yao ikiwemo vitendo vya unyanyasaji. Akizindua program hiyo Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato amesema mradi huo unalenga kutengeneza sera za shirika na kujenga uwezo kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia. Amesema mradi huo, utasaidia kuwepo kwa taarifa sahihi za unyanyasaji wa kijinsia katika shirika, kuruhusu fursa ya ukuzaji taaluma kwa wafanyakazi wanawake na kuongeza mafunzo kwa vitendo kwa wafanyakazi wanawake waliopo kazini. “Mradi huu unatekelezwa na TANESCO lengo ni kuhakikisha watumishi wanaofanya…

Read More