Author: Geofrey Stephen

Na GeofreyStephen ,Arusha Katibu Tawala Mkoa wa Arusha ,Missaile Musa amewataka wakurugenzi wa Halmshauri za Mkoa wa Arusha kubaini makundi au vikundi yanayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa zao ili kupata mafunzo kutoka Tume ya Ushindani (FCC) kwa lengo la kuongeza tija ikiwemo mnyororo wa thamani ,kwalengo la bidhaa kuwa na viwango kwenye ushindani wa soko. Katibu Tawala  wa Mkoawa  Arusha Messaile Musa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa uwamasishaji . Agizo hilo limetolewa  Jijini Arusha na Katibu Tawala,Musa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uhamasishaji wa masuala ya ushindani na Udhibiti wa Bidhaa Bandia kwa wazalishaji Kanda ya Kaskazini. Alisema…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma KATIKA kuimarisha miundo mbinu sekta ya umeme hapa nchini, na kuondoa changamoto kwa jamii, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema linatekeleza miradi ya uzalishaji iliyopo maeneo mbalimbali ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka, zitakazo patikana Megawati 5000 hadi 6000 ifikapo mwaka 2025 zitakazo uzwa ndani na nje ya nchi Aidha Shirika hilo limesema haliuzi nguzo za umeme bali linauza huduma ya umeme kutokana na maneno ya wananchi ambayo yamekuwa yakisemwa bila uelewa wa kutosha . Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma. IMEELEZWA kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 6.4 kupitia Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi kwaajili ya kuimarisha uthibiti ubora na uhuishaji wa mitaala ya vyuo vikuu ambapo zaidi ya mitaala 300 ya vyuo vikuu iko katika hatua mbalimbali zakufanyiwa mapitio. Akizungumza Jijini Dodoma Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU Prof.Charles Kihampa alipokuwa akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Time ya Vyuo Vikuu Tanzania kwa kipindi Cha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya awamu ya 6 amesema lengo nikuhakikisha elimu itolewayo na vyuo vikuu Tanzania vinakidhi…

Read More

Na Geofrey  Stephen,Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kuzoa taka na Usafi wa Mazingira ya Together We Can Do Women Group ya Jijini Arusha,Neema Mosha{39} mkazi wa kata ya Moshono Mtaa wa Moshono Kati amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma kushindwa kuwasilisha shilingi milioni 49.9 za Jiji hilo. Akisomewa mashitaka hayo leo na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa{TAKUKURU} Mkoani Arusha,Rubein Maduhu ilidaiwa kuwa Mosha alitenda kosa hilo katika kipindi cha mwaka 2021/22 wakati Kampuni hiyo ilipopewa Uwakala wa kazi hiyo ya kuzoa taka na usafi wa Mazingira. Maduhu alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya…

Read More

Na Geofrey Stephen ARUSHA SHIRIKA la Hifadhi za Taifa TANAPA,linatarajia kufanya maadhimisho ya kwanza ya miaka 50 tangia kuanzishwa kwa hifadhi ya Mlima Kilimanjaro yatakayofanyika, Machi 16 Mwaka huu katika makao makuu ya mlima huo yaliyopo, Marangu Mkoani Kilimanjaro . Akiongea na vyombo vya wa habari Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha,naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho alisema maadhimisho hayo ya kwanza ya aina yake , yanalenga pia kuutambulisha umma kuwa mlima kilimanjaro unapatikana katika nchi pekee ya Tanzania. Alisema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Marangu, mkoani Kilimanjaro, huku Makamu wa Rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa…

Read More

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Ephraim Mafuru ameahidi kufanya kazi kwa bidii ili kurudisha heshima iliyopotea ya kituo hicho. Mafuru aliyasema hayo wakati alipofika rasmi kuanza majukuu yake mapya katika ofisi za Aicc mara baada ya kuteuliwa na Mh Rais Samia Suluhu Assan ambapo amesisitiza kurudisha tena  imani ya wateja wa zamani wa AICC. Mafuru amesema kwamba kituo hicho kilikua kikifanya vizuri sana kipindi cha nyuma hivyo atatumia uongozi wake vyema kurudisha kituo icho katika soko la mikutano ambapo wateja wategemee ushirikia o mkubwa kuyoka katika uwongozi wa Aicc kwa ujumla.  “Tumedhamiria kuwabakisha wateja…

Read More

Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick lowassa Hii Leo amewasili Ofisi ya Mkuu Mpya wa Wilaya ya Monduli Kwa lengo la kumkaribisha DC mpya Mh Selemani Mwenda katika Jimbo Hilo. Katika utambulisho na ukaribisho huo mh Frederick Lowassa amempongeza DC Mwenda Kwa kuteuliwa Kuja Monduli pamoja na ziara alizozifanya ikiwemo ya kukutana na Viongozi WA Mila (malaigwanani) pamoja na Kuzindua kampeni yake ya upandaji wa miti. “Nikupongeze sana Mh DC wewe sio mgeni Monduli ni mtu ambaye tayari ulikuwa kwenye kazi hizi karibu Monduli naaahidi kukuunga mkono katika utekelezaji na usimamizi wa miradi lakini Nina maombi kwako ikiwemo swala…

Read More