Author: Geofrey Stephen

Na Doreen Aloyce,Dodoma Mtendaji Mkuu wa TBA Daud Kondoro Amesema Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeishukuru serikali ya Rais Dkt. Samia kwa kukuendelea kuwawezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ikiwemo kupewa fedha bilioni 54.2 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi. Daud Kondoro ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu wa wakala huo katika kipindi cha miaka miwili. “Naishukuru sana serikali ya Rais Dk. Samia kwa kuendelea kuiwezesha TBA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni Pamoja na kutoa fedha za ruzuku kwa ajili ya kutekeleza miradi ya serikali. katika kipindi…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma JAMII meshauriwa kuacha kukopa mikopo umiza kiholela Almaharufu Kama (KAUSHADAMU) na baadala yake wameshauriwa kuchukua fedha hizo kwa Matumizi lengwa kwani wanawake wengi wamekuwa wakichukua mikopo na kufanya mambo ambayo hayaingizi kipato kama vile kulipa ada,ujenzi wa nyumba na fahari za mavazi. Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Being’i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekekezaji wa majukumu ya baraza hilo . Pia amesema kuwa watanzania wengi bado hawana elimu ya kutosha juu ya matumizi ya fedha itokanayo na mikopo na badala…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Serikali imechukua hatua mbalimbali kutatua changamoto za kiuchumi katika vituo vya utangazaji nchini kwa kupunguza ada za leseni za mwaka kwa takribani asilimia 40. Pia Serikali imepunguza ada za masafa ya utangazaji katika maeneo ambayo hayana tija kibishara. Haya yameelezwa jijini hapa jana, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Kundo Methew, wakati akifungua Mkutano Siku Mbili wa Nwaka wa Watao Huduma wa Sekta ya Utangazaji pamoja na Maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani. “Hatua za kwanza Serikali iliyochukua ni kupunguza ada za mwaka za leseni utangazaji kwa takribani asilimia 40,” amesema Methew Methew alisema, Serikali…

Read More

Mwandishi wetu , Longido Shirika la wanahabari la kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) limeanza kusambaza vitabu vya maarifa ya asili katika utunzaji wa Mazingira, misitu na Vyanzo vya maji, katika makundi mbalimbali ikiwepo mashuleni,kwa vijana na makundi mengine. Vitabu hivyo,vilizinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dr Seleman Jafo jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita. Vitabu hivyo, ambavyo vinatokana na simulizi la viongozi wa Mila ya kimasai, wanawake na vijana vimechapishwa Ikiwa ni sehemu ya mradi wa Uhifadhi na utunzwaji Mazingira kwa maarifa ya Asili ambao unaofadhiliwa na mfuko wa Mazingira duniani (GEF) kupitia…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma . Dodoma Baraza la Taifa la ujenzi limeendesha mafunzo ya kusimamia mikataba ya ujenzi na utatuzi wa migogoro kat toika miradi ya ujenzi kwa wadau 155 kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani. Mtendaji Mkuu wa baraza la taifa la ujenzi Dk.Matiko Mturi Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa baraza hilo katika serikali ya awamu ya sita. Dkt Mturi amesema wameandaa Rasimu ya Mapendekezo ya gharama za msingi za ujenzi wa barabara (base unit rates) kwa kila mkoa wa Tanzania bara na kuwakilisha katika kikao cha wadau wa ndani ya…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Morogoro Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ametoa wito kwa wakulima walioko katika maeneo yenye hali ya hewa kama ya Mang’ula Kilombero kulima zao la Mpira ili kukidhi mahitaji ya soko la 99.7% ambalo kwa sasa mauzo ya zao hilo ni 0.03% Waziri Kijaji ameyasema hayo Februari 11, 2023 alipotembelea Shamba la Mpira la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro kuangalia jitihada zinazofanywa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) katika kuendeleza uzalishaji wa zao hilo la Mpira ambalo ni zao la kimkakati linalotumika kutengeneza bidhaa kama matairi,…

Read More