Author: Geofrey Stephen

Nà Emmanuel mkulu Njombe Mahakama ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imemhukumu kifungo cha miaka minne jela Baraka Luoga (20) mkazi wa Kimelembe wilayani humo kwa kosa la kumjeruhi kwa kumkata kiganja cha mkono bosi wake kwa madai ya sh. 65,000. Tukio hilo ambalo lilitokea Desemba 25, 2022 ambapo mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo wakiwa mashambani baada ya kupishana kauli na bosi wake huyo wakati wakieleweshana juu ya malipo ya pesa hizo. Baada ya kusomewa shitaka lake kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo na mwendesha mashtaka Angelo Marco mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi wa mahaka ya wilaya Ludewa Isaac…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha Kanisa la Kilutheri Afrika ya Mashariki(KKAM) limetoa msimamo wake katika mjadala unaendelea duniani wa ndoa za jinsia moja na utoaji wa mimba kwa kupinga vikali ndoa hizo huku likiweka bayana mipango ya jimbo la Arusha katika kuielemisha jamii kusimama katika maadili. Msimamo huo umebainishwa na makamu askofu mkuu wa kanisa hilo hapa Tanzania ambaye pia ni askofu wa jimbo la Arusha Dkt.Philemon Mollel wakati wa mkutano mkuu wa kwanza wa halmashauri kuu ya kanisa hilo nchini. Askofu Mollel amwsema kwamba awawezi kufumbia macho matukio kama ayo kwani jamii kwa sasa imekua na changamoto kubwa…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma MHADHIRI Msaidizi wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Roggers Ndyonabo amesema kuwa chuo hicho Kimekuwa kikifanya tafiti kuhusu masuala ya uendeshaji wa mashauri ya watoto na wamebaini kuwa yapo mahitaji wanayotakiwa kupewa waendeshaji wa mashauri ya Watoto. Akiongea na waandishi wa habari katika ufunguzi wa wiki ya Mahakama jijini Dodoma Mhadhiri huyo amesema baada ya Kutoa utafiti uliofadhiliwa na shirika la watoto duniani (UNICEF) tulipata picha juu ya mahitaji yanayotakiwa wapewa waendeshaji wa mashauri ya watoto kuwa wanaotakiwa kupewa elimu endelevu. Aidha Mhadhiri Ndyonabo amesema baada ya kubaini hali hiyo waliweza kupata fursa ya kutoa…

Read More

Na Juliana Laizer Monduli Wanafunzi takriban 170 wasio kuwa na uwezo waliotakiwa kujiunga na Elimu ya Sekondari Wilayani Monduli wamepatiwa msaada wa Baadhi ya vifaaa vya Shule vikiwemo Magodoro, Masanduku(tranga) kutoka Ofisi ya Mbunge. Akizungumza katika Makabidhiano ya vitu hivyo Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Frederick Lowassa amesema zoezi Hilo ni utamaduni wa Ofisi yake na hiyo imeenza baada TU ya kutangazwa kuwa mbunge wa Jimbo Hilo Kwa kuwasaidia watoto waliomaliza shule za misingi mahitaji Kwa baadhi yake kuelekea Sekondari. ”kwa kutambua umuhimu wa Elimu Kwa Jimbo la Monduli kuwa ni kitovu Cha nchi , nimeona iwe desturi ya…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Njombe Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia watu 13 akiwemo mhusika mkuu wa uchakachuaji mbolea za ruzuku na kuwauzia wakulima baada ya msako mkali wa takribani wiki mbili. Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa Amesema awali walikamatwa baadhi ya wafanyakazi wa wakala huyo ambaye jina lake limehifadhiwa lakini sasa na yeye amekamatwa tayari. Aidha Kamanda Issa Amesema kati ya watu hao 13 waliokamatwa wawili ni wanawake pamoja na waliokuwa wakisafirisha vifaa vya kufanikisha uchakachuaji huo wa mbolea na wauzaji wa maduka. Wakati hayo yakijiri katika Jeshi la polisi mkoani…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema kuwa uzalishaji wa sukari nchini umeongezeka hadi kufikia zaidi ya tani 70,000 na kufanya kuwa na zaidi ya tani 160,000 kwenye maghala katika kipindi cha 2022 /2023 na kupunguza kwa kiasi kikibwa uhaba wa sukari nchini. Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji katika kikao na wadau wa uzalishaji wa sukari chini kilicholenga kufahamu hali ya uzalishaji wa sukari nchini, Dkt. Abdalah amesema Serikali inaendelea  kuhakikisha  uwepo wa uwekezaji mkubwa…

Read More