Author: Geofrey Stephen

Na mwandishi wa A24Tv _Dodoma_ Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa uchimbaji wa makaa ya mawe hususan katika mkoa wa Ruvuma umeendelea kuipaisha Sekta ya Madini kutokana na wawekezaji wengi kuendelea kujitokeza yakiwa ni matokeo ya mazingira mazuri ya uwekezaji pamoja na Serikali kuendelea kutangaza fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini. MAKAA YA MAWE YAENDELEA KUIPAISHA SEKTA YA MADINI Mhandisi Samamba ameyasema hayo leo tarehe 16 Januari, 2023 jijini Dodoma kwenye mahojiano maalum na waandishi wa habari kutoka kituo cha Imaan TV ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kipindi maalum chenye lengo la kuangalia…

Read More

Na WyEST Masasi, MTWARA Wito umetolewa kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kutowaficha watoto ndani badala yake wawapeleke shule kwa kuwa zipo shule maalum kwa ajili ya watoto hao. Hayo yamesemwa na Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokuwa akizindua majengo mapya ya Shule Jumuishi ya Mfano ya Msingi Lukuledi iliyojengwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa Elimu na Kuendeleza Ujuzi na Stadi za Kazi (ESPJ) na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kumnyima mtoto haki yake ya msingi ya kupata elimu. “Nipende kuwaasa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum popote nchini kutowaficha watoto ndani kwani…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro pamoja na viongozi wa kata ya Irisya wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya ikungi Mhe. Ali juma mwanga ambae ni diwani wa irisya wamefanikiwa kuumaliza mgogoro wa ardhi baina ya Mama Hadija Mohamed na Ndugu Masoud Jumanne Tipa wa kitongoji cha mghondwe kijiji cha munyu kata ya irisya Mgogoro huo uliodumu kwa miaka 18 mara baada ya kumalizika kwenye baraza la ardhi kata na wilaya lakini bado wananchi hao waliendelea kuvutana hatua iliyosababisha eneo kutolimwa katika msimu huu wa kilimo hatua ambayo Mkuu wa wilaya Mhe.…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara ya Elimu Bara na ile ya Zanzibar zinafanya kazi kwa kushirikiana katika suala la mageuzi ya Sera ya Elimu na maboresho ya mitaala ili kuwawezesha vijana wa pande zote mbili kupata ujuzi na stadi zitakazowasaidia kujiari ama kuajiriwa na kuchangia katika uchumi wa Taifa. Akizungumza mjini Zanzibar Januari 11, 2023 katika hafla ya ugawaji wa vishkwambi kwa walimu wa Zanzibar vilivyotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema anaamini mapendekezo yatakayotolewa na Serikali baada ya kupokea maoni ya wadau yatashabihiana isipokuwa tu pale ambapo…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Monduli. Arusha Viongozi wanane wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Engaruka wilayani Monduli, mkoani Arusha, wamelazwa hospitali baada ya kudaiwa kushambuliwa hadi kujeruhiwa na kundi la wananchi wakati wakifuatilia migogoro ya ardhi. Habari za kuaminika zinasema kuwa wananchi hao wa Kijiji cha Engaruka Juu, waliwashambulia viongozi hao kutokana na hasira za kuuzwa kwa ardhi ya kijiji hicho kinyemela. Tukio hilo limetokea juzi jioni wakati viongozi hao ambao ni wajumbe wa kamati ya siasa ya chama hicho walipokwenda kijijini hapo kufuatilia tuhuma za Mwenyekiti wa kijiji hicho, Abrahamu Logolie kudaiwa kuuza ardhi kinyemela. Hata hivyo, mara…

Read More