Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Morogoro Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) ametoa wito kwa wakulima walioko katika maeneo yenye hali ya hewa kama ya Mang’ula Kilombero kulima zao la Mpira ili kukidhi mahitaji ya soko la 99.7% ambalo kwa sasa mauzo ya zao hilo ni 0.03% Waziri Kijaji ameyasema hayo Februari 11, 2023 alipotembelea Shamba la Mpira la Kalunga lililopo Kata ya Mang’ula Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro kuangalia jitihada zinazofanywa na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) katika kuendeleza uzalishaji wa zao hilo la Mpira ambalo ni zao la kimkakati linalotumika kutengeneza bidhaa kama matairi,…

Read More

Na Geofrey Stephen ,Arusha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dr. Suleyman Jaffo amezindua kitabu Cha kwanza Cha aina yake Cha maarifa ya asili katika uhifadhi wa Mazingira ,misitu na Vyanzo maji.. Kitabu hicho kimeandaliwa na taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) Kwa kushirikiana na taasisi ya CILAO kimetokana na simulizi za wazee la Mila ya kimasai, wanawake na vijana wa jamii hizo katika wilaya za Ngorongoro, Longido na Monduli. Akizindua kitabu hicho leo february 11, 2023 Waziri Dr. Jafo amepongeza MAIPAC Kwa kuja na mradi huo wa aina yake na kueleza…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Wakala wa Majengo Tanzania TBA imeanza kuwaondoa ndani ya nyumba wapangaji wake ambao ni wadaiwa sugu mkoa wa Arusha kutokana na Malimbikizo makubwa ya madeni yao kutoka kwa wapangaji walio kodi nyumba za shirika ilo . Vyombo vya wadaiwa sugu zikitolewa nje na madalali walio pewa kazi iyo mara baada ya wadaiwa kukimbia na kuacha nyumba zao tupu . Akiongea wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo,kwa wapangaji watatu akiwemo mdaiwa sugu mwenye mwenye malimbikizo ayo kaimu meneja wa TBA mkoa sa Arusha ,Mhandisi Juma Dandi alisema kuwa operesheni hiyo ni ya nchi nzima na imelenga kukusanya…

Read More

Na Mwandishi A24Tv Arusha . Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilayani Monduli Ndugu Moitiko kisioki ameendeleea na ziara yake ya kata Kwa kata Kwa lengo la kushukuru, kukagua uhai wa wanachama ,kusikiliza kero za jumuiya hiyo pamoja na kutoa Elimu kwa viongozi . Akizungumza katika ziara yake katika Kijiji cha Mti mmoja kata ya Sepeko hapo jana Amewapongeza Wananchi pamoja na wanachama wa kata hiyo kwa kuwa na mpango Bora wa ufugaji na kuwahidi kurudi kata hiyo kwa ajili ya Semina ya namna ya kuvuna majani(malisho) kupitia maeneo tengefu maarufu ilaliliak ili waweze kuvuna mifugo Yao kwa tija. “Sepeko ni…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha. Halmashuri ya Jiji la Arusha limetoa kiasi cha Shilingi Milioni 33 kwaajili ya kununua unga lishe maalum kwaajili ya watoto wenye mahitaji maalum waliyopo mashuleni katika halmashauri hiyo lengo likiwa ni kuwaongezea afya ya mwili na akili kwa watoto hao. Akikabidhi unga huo pamoja na vifaa vingine kwenye shule za msingi 9 ambazo zina idadi ya watoto 519 wenye mahitaji maalum Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Hargeney Reginald Chitukuro, amesema serikali kupitia halmashauri yake imefikia hatua hiyo ya kutoa vyakula vyenye lishe kwa watoto hao wenye mqhitaji maalum ili wazidi kukuwa kiafya na waweze kukuza taaluma…

Read More

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa ufafanuzi kuhusu watahiniwa waliofutiwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2022. Akitoa ufafanuzi huo Jijini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb), Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema kati ya watahiniwa 560,335 waliofanya mtihani, 337 ndio waliofutiwa matokeo na wengine 20 matokeo yao yamezuiliwa yakisubiri uchunguzi kukamilika. Waziri Mkenda amesema kuwa kati ya waliofutiwa matokeo wanne waliandika lugha isiyo na staha, 51 walikutwa na maandishi yasiyoruhusiwa ndani ya chumba cha mtihani, 10 walikamatwa na simu na smart watch, 9 walifanyiwa mtihani na watu…

Read More