Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv . Arusha  Dc Mtanda amjibu Mbunge wa Arusha mjini Mrisho Gambo kutoa madai ya kutishiwa kuuawa na watu aliodai ni viongozi  wa serikali, Mkuu wa wilaya ya Arusha,Saidi  Mtanda kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kufika ofisini kwake kueleza kwa kina madai ayo  “Kama Mbunge  alitishiwa maisha kwanini hakutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ,kama unatuhuma yoyote unatakiwa wewe mwenye ukathibitishe kwenye vyombo vya usalama” Akiongea na vyombo vya habari ofisini kwake Mtanda alidai kutokuwa na taarifa za mbunge huyo kutaka kuuawa akisisitiza kuwa taarifa hizo hana na wilaya ya Arusha ipo salama . Hata hivyo…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Waziri wa Malii Asili na Utalii Nchini,Dkt Pindi Chana amezitaka Mamlaka za Hifadhi na Utalii Nchini kuhakikisha wanabuni vyanzo vipya wa Urithi wa Dunia lengo ni kuvutia Watalii zaidi kuja Nchini kutalii na kuacha kutegemea pekee vyanzo vya zamani. Chana alisema hayo jana Jijini Arusha wakati  akifungua Mkutano wa siku mbili wa Wataalamu wa Tafiti za Hifadhi ya Asili na Tamaduni kutoka katika Nchi 52 Duniani katika kuadhimisha miaka 50 ya Mkataba wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalishughulikia Masuala ya Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO} ambapo Tanzania ni Mwenyeji. Alisema hadi sasa Tanzania ina vyanzo saba tu…

Read More

mwandishi wetu,Dar es salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Saalam,imezuia kuendelea mchakato wa Mnada wa Kitalu cha uwindaji katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii Burunge (JUHIBU) Mahakama imetoa zuia la dharura la mchakato wa kukigawa kitalu hicho kutokana na kesi iliyofunguliwa na kampuni ya EBN ambayo imekuwa na mkataba katika kitalu hicho tangu mwaka 2013. Hakimu Mkazi mwandamizi Ferdnadri Kiwonde ametoa uamuzi huo kutokana na maombi ya dharura yaliyowasiloshwa na EBN na kukubaliana na hoja ya msingi kuwa tayari ina mkataba kuendesha kitalu na kutaka kesi ya msingi kusikilizwa Zuia mnada huo liliwekwa na EBN…

Read More

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT ) kimetakiwa kusimamia ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapo ili kuhakikisha hadhi ya Chuo na elimu ya Tanzania kwa ujumla inalindwa. Hayo yamesemwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Mpango wakati alipotembelea Chuo hicho kwa lengo la kukutana na viongozi, wanataaluma na watumishi ili kujionea hali halisi ya chuo hicho ambapo amesema kumekuwa na malalamiko kidogo kuwa kuna urahisi wa kuhitimu katika chuo hicho hivyo kuonekana baadhi ya wahitimu kutokuwa na ubora. “Kuna malalamiko kuwa baadhi ya wahitimu wa Shahada za Uzamili na Uzamivu huandikiwa ripoti zao…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Tengeru  MKUU wa wilaya ya Arumeru,mkoani Arusha, mhandisi Richard Ruyango, amewataka vijana wilayani humo sanjari na wale  wanaosoma  kwenye vyuo , kuhakikisha wanajitambua na  kujilinda na maambukizi ya ukimwi kwa kutumia kinga wanapokuwa kwenye mahusiano. Mhandisi Ruyango ameyasema hayo katika chuo cha maendeleo ya Jamii Tengeru wilayani humo,wakati alipohudhulia maadhimisho ya siku ya udhibiti wa ukimwi duniani  ,ambapo kitaifa yamefanyika mkoani Lindi. Alisema maadhimisho hayo ambayo kiwilaya yalifanyika katika chuo hicho ,walilenga kutoa elimu zaidi kwa kuwakumbusha vijana kuwa Ukimwi bado upo na unaua hivyo nijukumu lao kama rasilimali ya taifa kujilinda na kuacha ngono uzembe.…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Singida Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro leo tarehe 09/12/2022 amewaongoza mamia ya wananchi katika Maazimisho ya sherehe za miaka 61 ya uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya kongamano la kihistoria lililowaleta wananchi, viongozi wa dini, wazee maarufu, watumishi wa umma na wafanyabiashara pamoja na wadau wa maendeleo wilaya ya Ikungi Akitoa hotuba kwebye kongamano hilo Mhe. Muro amesema katika miaka 61 ya uhuru taifa limeweza kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umasikini kwa mafanikio makubwa kutokana na serikali za awamu zote kuwekeza vya kutosha katika mapambano ya kutokomeza maadui…

Read More