Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Njombe Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia watu 13 akiwemo mhusika mkuu wa uchakachuaji mbolea za ruzuku na kuwauzia wakulima baada ya msako mkali wa takribani wiki mbili. Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa Amesema awali walikamatwa baadhi ya wafanyakazi wa wakala huyo ambaye jina lake limehifadhiwa lakini sasa na yeye amekamatwa tayari. Aidha Kamanda Issa Amesema kati ya watu hao 13 waliokamatwa wawili ni wanawake pamoja na waliokuwa wakisafirisha vifaa vya kufanikisha uchakachuaji huo wa mbolea na wauzaji wa maduka. Wakati hayo yakijiri katika Jeshi la polisi mkoani…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema kuwa uzalishaji wa sukari nchini umeongezeka hadi kufikia zaidi ya tani 70,000 na kufanya kuwa na zaidi ya tani 160,000 kwenye maghala katika kipindi cha 2022 /2023 na kupunguza kwa kiasi kikibwa uhaba wa sukari nchini. Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji katika kikao na wadau wa uzalishaji wa sukari chini kilicholenga kufahamu hali ya uzalishaji wa sukari nchini, Dkt. Abdalah amesema Serikali inaendelea  kuhakikisha  uwepo wa uwekezaji mkubwa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Tawi Jipya ndani ya Jiji la Arusha Benki ya United of Afrika (UBA) imezindua Tawi Lake jipya la likiwa ni miongoni mwa matawi 8  ndanibya jijini Arusha, Ambapo wafanyabiashara katika Jiji la Arusha na viunga vyake wametakiwa kuchangamikia fursa ya kupata mikopo yenye riba nafuu kwa lengo la kukuza biashara Akiongea Katika uzinduzi wa tawi la benki hiyo iliyopo katika kata ya Levolosi mkabala na Ofisi ya Shirika la nyumba la taifa (NHC),Naibu Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango bw.Lawrence Mafuru,kwa niaba ya Waziri wa fedha na Mipango dkt.Mwigulu Nchemba aliitaka benki hiyo kuongeza uwekezaji…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Nabii Mkuu wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Geor Davie ametoa hundi ya sh,milioni 100 kwaajili ya kusaidia wafajasiamali wa soko la Samunge lililopo Kata ya Kati Jijini Arusha ili waweze kujionea kiuchumi. Aidha amesena kuwa yeye sio mwanasiasa bali anamshukuru Mungu kwani baraka imekuja na kutoa rai kwa viongozi wa dini rudisheni sadaka walizotoa waumini wetu Pia alishukuru wananchi waliobeba picha na mapokezi mazuri na kusema kuwa awali aliandaa hundi ya sh,milioni 50 lakini baada ya kuona umati huo na chagamoto za soko hilo ameongeza tena sh,milioni 50 nyingine. Alisema sh,milioni 80 inaenda kwa watu…

Read More

Na Emmanuel Njombe . Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania TFRA imetangaza kufuta leseni ya wakala wa mbolea aliyekamatwa akitakatisha mbolea mkoani Njombe na kuwauzia wakulima kinyume Cha sheria. Akitangaza hatua hiyo mkurugenzi wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania TFRA Dokta Stephan Ngailo baada ya kuzulu mkoani Njombe na kushuhudia nyumba nyingine ya mfanyabiashara huyo iliyopo mtaa wa Kwivaha mjini Njombe ambayo imekuwa ikifanya kazi ya kuhamishia mbolea zinazochakachuliwa amesema licha ya kufuta leseni hiyo lakini anapaswa kushtakiwa kwa tuhuma anazokabiliwa nazo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema hadi sasa zaidi ya watu 10 wanashikiliwa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Njombe Serikali mkoani Njombe imekamata nyumba chakavu inayotajwa kutumiwa na mfanyabiashara (jina linahifadhiwa) kwa ajili ya kuchakachua mbolea zikiwemo za ruzuku katika mtaa wa Ramadhani uliopo halmashauri ya mji wa Njombe na kwenda kuwauzia wakulima. Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Njombe iliyoongozwa na mkuu wa mkoa huo Anthony Mtaka imefika katika eneo la nyumba hiyo na kukuta shehena ya marobota ya mifuko yenye mbolea na isiyokuwa na mbolea ya ruzuku pamoja na vifaa vingine vinavyotumiwa kwa ajili ya kuchakachua mbolea. “Tumebaini uwepo wa nyumba ambayo kuna mfanyabiashara anaitumia kuchakachua mbolea,kwa hiyo tumejionea wenyewe marobota…

Read More