Author: Geofrey Stephen

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu Fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza Masuala ya Biashara Bw. Lord Walney alieambatana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar katika Ofisi ndogo zilizopo Dar es salaam Novemba 30, 2022. Waziri Kijaji amemhakikishia Mjumbe huyo kuwa Tanzania iko tayali kuendela kushirikiana na Uingereza katika kuendeleza sekta ya biashara na uwekezaji na iko tayali kupokea wawekezaji kutoka nchini humo.

Read More

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu Fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Cryogas Equipment Private Limited Bw. Nayan Pandya kutoka India katika Ofisi ndogo zilizopo Dar es salaam Novemba 30, 2022. Waziri Kijaji amemhakikishia Mwekezaji huyo mwenye nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati hususan gesi asilia kuwa Serikali iko tayali kupokea uwekezaji huo.

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Mkuu wa wilaya ya  Arusha Arusha ,Said Mtanda ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji  Ewura Mkoa wa Arusha kwa kuandaa mafunzo kwa madiwani wa Jiji la Arusha pamoja na watendaji wa kata wote kwa pamoja kuelimishwa kazi za Ewura . Mtanda ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau mbalimbali wa   sekta ya maji uliofanyika jijini Arusha uliolenga kujadili kero mbalimbali zitokanazo na sekta  ya maji ,umeme ambayo ndio matumizi makubwa kwa wananchi ya kila siku ambapo wananchi wengi watahitaji kutambua huduma wanazo pata kama ni sahihi . Amesema kuwa  madiwani na…

Read More

_Ni kupitia ushirikishwaji wa watanzania katika Sekta ya Madini, uboreshaji wa huduma za jamii unaofanywa na migodi ya madini_ *KAHAMA* Watoa huduma kwenye migodi ya madini katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wameipongeza Serikali kwa usimamizi mzuri wa Sekta ya Madini kupitia Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Tume ya Madini hali iliyopelekea watanzania wengi kushiriki katika sekta hiyo kupitia utoaji wa huduma katika shughuli za uchimbaji wa madini na kuongezeka kwa kasi ya uboreshaji wa huduma za jamii unaofanywa na kampuni za madini. Watoa huduma hao waliyazungumza hayo jana tarehe 29 Novemba, 2022 katika eneo la Kahama kwenye mahojiano…

Read More

Mwandishi wetu, Babati Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Burunge(JUHIBU) kwa takriban miezi mitatu sasa kumekuwa na mgogoro ambao unatokana na uwekezaji katika kitalu cha uwindaji ambacho kinapakana na hifadhi ya Taifa ya Tarangire Mgogoro huo umeibuka baina ya Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Hamis Juma na Bodi ya wadhamini wa jumuiya hiyo ambayo inaungwa mkono na baraza la ushauri la maliasili la wilaya hiyo na wananchi waliowengi. Katika mgogoro huo, Juma na baadhi ya wafuasi wake kutoka baraza la uongozi wanataka kuvunjwa mkataba ambao bodi ya jumuiya hiyo lisaini julai 14, mwaka huu na kampuni ya uwindaji wa kitalii ya EBN…

Read More

Na Geofrey Stephen ,Arusha Kamishna wa bima nchini ,Dkt Baghayo Saqware amezitaka mamlaka za bima nchini kuendelea kuelimisha wananchi juu ya matumizi ya sahihi ya bima kwa lengo la kuwapunguzia gharama pale wanapofikwa na majanga mbalimbali ikiwemo matibabu ya afya. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa bima kanda ya Kaskazini,Dkt Saqware alisema pamoja na serikali kuweka mpango mkakati wa ukuzaji na uendelezaji wa sekta ya fedha nchini wa miaka 10 hadi kufikia juni 2030 bado mwitikio wa wananchi ni mdogo. Alisema mamlaka ya bima nchini inapaswa  kuhakikisha inafikia malengo ikiwemo kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania watu…

Read More