Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen .Arusha Arusha.Mwenyekiti wa wazazi Taifa (MCC) Fadhili Maganya ameitaka jumuiya ya wazazi kuendelea kumuunga mkono Rais Samia katika maswala mbalimbali ya maendeleo anayoendelea kuyafanya . Ameyasema hayo jijini Arusha wakati akikaribishwa rasmi na jumuiya ya wazazi mkoani Arusha Maganya amesema kuwa, Rais Samia amekuwa akifanya mambo mengi sana ambayo kila mmoja wetu anapaswa kuyaunga mkono na kuhakikisha kazi inasonga mbele. Amefafanua kuwa,wataendelea kumuunga mkono Rais Samia kwa namna yoyote ile na yupo tayari kumtetea Rais na kamwe hatakubali kuona jina la mama linachezewa na mtu yoyote. Aidha amesema kuwa, wanachotakiwa kutambua wao ni kuwa,kama kura zimetosha au…

Read More

Na mwandishi wa A24Tv . (Mr. Amani Golugwa ameshinda tuzo ya THE TOP 100 EXECUTIVE LIST 2022 TANZANIA AWARDS. Mr. Amani amekuwa mmoja wa washindi kwenye kundi la Wakurugenzi (CEO) wa Asasi za Kiraia (Mashirika yasiyo ya Kiserikali) na kutwaa tuzo ya MKURUGENZI BORA WA TAASISI KWA MWAKA (CEO OF THE YEAR 2022) katika mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs. Mr. Amani Golugwa ni Mkurugenzi (CEO) wa shirika la Help to Self Help lililopo Jijini Arusha, ambalo linahusika na masuala ya Elimu (Ujuzi na Ufundi Stadi), Kuiwezesha Jamii (Economic Empowerment) na Afya (Community Health). Tuzo hizo zilifanyika Jijini Dar es Salaam…

Read More

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha Wanawake na Vijana wa Bara la Afrika kutumia fursa na kushiriki kikamilifu kwenye biashara katika Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA). Ameyasema hayo Novemba 25, 2022 wakati akimwakilisha Rais katika Mkutano wa Dharula wa 17 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Maendeleo ya Viwanda Barani Afrika uliofanyika Novemba 20-25, 2022 Jijini Niamey Niger. Aidha, Wakuu hao wa Nchi…

Read More

Na Geofret Stephen Arusha MKURUGENZI WA BANK YA DUNIA KWA NCHI YA TANZANIA,MALAWI,ZAMBIA NA ZIMBABWE NATHAN BALETE AMEONESHWA KURIDHISHWA NA UWEKEZAJI KUBWA UNAOFANYWA NA SERIKALI YA TANZANIA KWA KUSIMAMIA MIRADI MBALI MBALI IKIWEMO MRADI WA NISHATI MBADALA WA KIKULETWA ILIYOPO WILAYANI HAI  MKOANI KILIMANJARO. MRADIO HUO WA DOLLAR MILIONI 6 WENYE LENGO LA KUONDOA CHANGAMOTO YA UMEME HUKU AKIELEZA NIA YA BENKI HIYO KATIKA KUWEKEZA KWA VIJANA WA KIAFRIKA KATIKA KUSIMAMIA MIRADI INAYOFADHILIWA NA BENKI HIYO. AMESEMA WAO KAMA SEHEMU YA MRADI HUO WANAFURAI KUONA HITIADA KUBWA ZA CHUO HICHO CHA ATC LUSIMAMIA VYEMA MIRADI YA MAENDELEO KAMA HUO WA…

Read More

Na Juliana Laizer Mbunge wa Jimbo la Monduli mh Fredrick Lowassa ameelekeza mara Moja kufanyika kwa ukarabati wa madarasa matatu katika shule ya msingi Kilimatinde kata ya Moita , yenye uhitaji mkubwa wa sakafu na Kuta Fredrick ametoa agizo Hilo katika mahafali ya tatu ya darasa la Saba katika shule hiyo ambapo amesema madarasa hayo atayakarabati mwenyewe na kumtaka Diwani na viongozi wengine wa serikali pamoja na kamati ya shule kumtafuta fundi Ili kuangalia na kupima Gharama ya ukarabati wa madarasa hayo Ili ukarabati huo uanze mara Moja ambapo wazazi nao walimshika mbunge mkono Kwa harambee iliyoendeshwa na Diwani wa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Dkt Fredrick Gilenga afisa madini mkoa wa Njombe amesema Kutokea kwa vita vya Ukraine na Urusi kumepelekea uhitaji mkubwa wa madini ya makaa ya mawe na kupelekea bei yake kupaaa zaidi. Dkt.Gilenga ametoa kauli hiyo katika kikao Cha ushauri mkoa wa Njombe RCC ambapo amesema uwepo wa makaa ya mawe mkoani Njombe Ni fursa kubwa inayoweza kuuingizia mkoa fedha nyingi za kigeni. Makaa ya mawe kwa mkoa wa Njombe yanapatikana Wilaya ya Ludewa ambayo yanaweza kuchimbwa kwa miaka 100 huku wawekezaji wakitaja changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara kuwa ni kikwazo.

Read More

Mwanza Wahitimu wa Vyuo Vikuu wameaswa kutumia vema elimu wanayopata kuleta tija kwa Taifa. Hayo yamesemwa Jijini Mwanza na Mhe. Dkt. Phillip Mpango wakati wa mahafali ya 41 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT). Aidha, Mhe. Mpango ameagiza Wizara ya Elimu kuhakikisha vituo vyote vya Chuo hicho vinaunganishwa na mkongo wa Taifa ili kuwezesha matumizi ya TEHAMA na kupunguza gharama za uendeshaji . “Vituo vyote vya Chuo Kikuu Huria vitaunganishwa na mkongo wa Taifa na hili naagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhakikisha linafanyika mara moja ili kupunguza gharama za uendeshaji,” ameongeza Mhe. Mpango. Awali akiongea katika mahafali…

Read More