Author: Geofrey Stephen

Na Emmanuel wa A24Tv. Waziri wa habari,mawasiliano na teknolojia ya habari Nape Nnauye amesema kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia hakuna budi serikali ikaendelea kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano kwa kujenga minara ya simu inayoweza kusaidia kupunguza adha kwa wananchi. Nape ametoa kauli hiyo Wakati akizindua mnara wa simu wa Vodacom katika Kijiji cha Kinenulo kata ya Imalinyi Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe uliojengwa kwa ushirikiano na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF na hivyo Ni lazima kuwekaza kwenye mawasiliano ili kuendana na teknolojia hiyo. Justina Mashiba ni mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF…

Read More

Na  Geofrey Stephen .Arusha Balozi Mstaafu,Daniel Ole Njoolay amesema  wakati umefika wa Chama Cha Mapinduzi[CCM] kujisafisha na kujirekebisha kasoro zote ili chama hicho kiwe kitu kimoja kwa maslahi ya Nchi. Njoolay alisema hayo leo Jijini Arusha wakati akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha,Stephen Zellothe na viongozi mbalimbali wa Chama wakitoa kauli ya Mkoa juu ya kuruhusiwa kwa vyama vya siasa kufanya Mikutano ya hadhara,marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa na marekebisho ya katiba iliyotolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan. Alisema iwapo CCM itakuwa kitu kimoja vyama vya siasa hawatakuwa naa hoja katika Mikutano yao ya…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv  Njombe Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dk Ashatu Kijaji amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe kuhakikisha inakusanya mapato ya Mbao kwa asilimia 3 kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Serikali na siyo shilingi 100 kwa kila ubao kama ilivyo sasa kwa baadhi ya Halmashauri. Hii ni baada ya wafanyabiashara mbalimbali kuomba Mapato ya ushuru wa Mbao walipe kwa asilimia 3 wakati wa Mkutano wa Saba wa Baraza la wafanyabiashara Mkoa wa Njombe wakiwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara unaofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe.

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha . Jamii imeaswa kuacha Tabia ya kuwapeleka watoto ambao wamefiwa na wazazi wao kwenye vituo vya mayatima na badala yake wawatunze ikiwa ni pamoja na kuwapa maitaji muhimu ya Kila siku. Endapo kama jamii itaweza kuwasaidia watoto hao kwa njia hiyo basi kutakuwa hakuna ongezeko la watoto yatima lakini pia ongezeko la watoto wa mitaani Hayo yameelezwa na Wakili Mary Mwita ambaye ni mkurugenzi wa kituo cha kisheria kijulikanacho kama smart community on legal protection wakati akikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wa kituo cha watoto yatima Ungalmt kituo Kinachomilikiwa na kanisa la International Evangelism church…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Fadhili Maganya amempongeza Rais Dk,Samia Hassan Suluhu kwa kutoa ruhusa ya kuanza kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini Aidha amesititiza kuwa ziara za nje wanazofanya Rais Dk, Samia zinaleta tija zaidi kwani akirudi nchini harudi bure na zinafungua milango nje na ndani ya nchi. Maganya aliyasema hayo leo Jijini Arusha wakati Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa tamko la umoja huo. Alisema fursa ya mikutano ya hadhara iliyotolewa na Rais Samia ni kuonyesha namna bora ya kuendesha siasa hapa nchini. Alisema Rais amesema mikutano ya vyama…

Read More