Author: Geofrey Stephen

-Rais Samia asema ni haki yao kikatba, akumbusha siasa za kistaarabu, kujenga nchi Na Mwandishi wa A24Tv Dar es salaam RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ametangaza rasmi kuruhusu kuanza kufanyika kwa mikutano ya vyama vya siasa nchini kuanzi leo. Ametoa ruhusa hiyo leo Januari 3,2023 wakati wa kikao kati yake na vyama vya siasa nchini ambao kimefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba mikutano ya hadhara ni haki ya vyama vya siasa. “Moja ya jambo ambalo limezungumzwa sana hata kwenye kikosi kazi ambacho nilikiunda kwa ajili ya kufuatilia hali ya…

Read More

Doreen Aloyce, Arusha. Wazazi kote nchini wametakiwa kuanza mwaka mpya wa 2023 kwa kuwa makini na watoto wao hasa wanapotoka shule kuwadhibiti katika matumizi ya simu za kiganjani ili kujenga kizazi kilicho bora. Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la KilutherI Afrika Mashariki(KKAM) Tanzania Oscar Olotu kwenye Ibada ya kuukaribisha mwaka mpya 2023 iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheri la Afrika Mashariki lililopo Kwangulelo jijini Arusha. Askofu Olotu amesema kuwa watoto wengi wa siku hizi wamekuwa wajanja na mitandao ya kijamii kwa kutumia simu jambo linalopelekea kuangalia video ambazo hazina maadili kwenye jamii. “Niwatake wazazi tunapoanza mwaka huu wazazi muendelee…

Read More

Na Mwandishi wetu, Mirerani WATOTO 13 wakiwemo wasichana nane na wavulana watano wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, katika kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 watachuana vikali kuwania ubingwa wa Mr & Miss Mazubu Grand Hotel. Meneja wa Mazubu Grand Hotel, Charles Rioba amesema michuano hiyo kabambe inatarajiwa kufanyika leo Jumapili ya Januari mosi mwaka 2023 kwenye hoteli yao. Meneja Rioba amesema watoto hao 13 watachuana kuwania nafasi hizo ambapo kwa wavulana mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi laki mbili na nusu, mshindi wa pili atapata zawadi ya shilingi laki moja na nusu na mshindi wa…

Read More

RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM BARA NA MWENYEKITI WA CHADEMA IKULU   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndugu. Abdulrahman Kinana wakati akipokea taarifa ya Maendeleo ya mazungumzo ya mchakato wa maridhiano ya kisiasa, Ikulu Jijini Dar es Salaam     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha . Madereva wanaotumia vyombo vya moto wakiwa wamelewa katika Mkoa wa Arusha wamepewa angalizo endapo watabainika kuendesha magari hayo wakiwa wamelewa. Hayo yamesemwa na Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha mrakibu wa Polisi SP SOLOMON MWANGAMILO wakati akizumgumza na Madereva wa mabasi mapema leo decemba 30.2022 katika stand kuu ya mabasi yaendayo mikoani na Nchi jirani. Mwangamilo amesema kuwa dereva atakaye bainika anaviashiria vya pombe atashugulikiwawa kwa mujibu wa sheria ambapo amewataka madereva wa magari hayo kutotumia vyombo hivyo wakiwa wameleva. Ameongeza kuwa kikosi hicho hakimkatazi mtu yeyote kutumia pombe ambapo amewataka…

Read More

Manyara Na Mwandishi wa A24Tv Manyara . BONANZA LA MIAKA 5 YA KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED LAFANA.  Wafanyakazi wa kampuni ya Mati Super Brands Limited wameshiriki katika bonanza Maalumu kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Miaka 5 ya kuanzishwa kwa kampuni ya Mati Super Brands Limited iliyoko mkoani Manyara.  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa bonanza hilo limehusisha michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu,kuvuta kamba n.k.  Mulokozi amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kudumisha umoja na mshikamano wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambao wamefanya kazi…

Read More