Author: Geofrey Stephen

Na Doreen Aloyce, Dodoma WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua zoezi la ugawaji wa vishikwambi 293400 Kwa walimu wote nchini lengo ni kuboresha mazingira ya ufundishaji Kwa njia ya TEHAMA. Ameagiza vishikwambi hivyo kuwafikia walengwa pasipo ubadhilifu huku akiwasisitiza walimu kuvitumia kwa usahihi. Akizungumza katika uzinduzi huo Majaliwa amesema serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa vitendo kuwekeza katika eneo la TEHAMA ili vijana wapate ajira na kujiajiri wenyewe kupitia shughuli mbalimbali na kusaidia Taifa kukua kiuchumi. Amesema adhma hiyo inaakisi mpango mkakati wa maendeleo wa Taifa ambao unaainisha afua ya kimkakati katika kuboresha na…

Read More

 NA: VERONICA MAKONGO, ARUSHA Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye manufaa Kwa jamii Kwa kuandika habari bunifu zinazolenga kuwakwamua wananchi  kuondokana janga la umaskini. Sekta ya habari na utangazaji ikitumika ipasavyo hususani vyombo vya habari mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia  vinaharakisha  zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka  zaidi hivyo kuwa chachu ya mabadiliko Mkurugenzi wa taasisi ya wanahabari ya MAIPAC  Bw Musa Juma akitoa hotuba katika mahafali ya 16 ya chuo cha uandishi wa habari Fanikiwa. PICHA na Marystela Bryson. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wanahabari inayosaidia jamii za pembezoni nchini…

Read More

Na Doreen Aloyce , Dodoma Katika juhudi za serikali za kuimarisha mazingira ya ujifunzaji wanafunzi wa kike hapa nchini,Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru iliyopo Jijini Arusha kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imeipatia shilingi Bilion 2.3 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la kike ambalo litasaidia kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo vitendo vya ubakaji . Akizungumza na vyombo vya habari Jijini Dodoma wakati akiwasilisha utekelezaji na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Mkuu wa Taasisi ya maendeleo ya jamii Tengeru Dkt. Bakari George amesema kuwa Bweni hilo lenye uwezo wa kubeba wanafunzi 568 litakuwa mkombozi kwao na taasisi hiyo Amesema…

Read More

Na Geofrey Stephen ,ARUSHA KATIBU Mkuu wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Allan Kijazi amevitaka vituo vya makusanyo ya Kodi na masulufu ya serikali,kutozifumbia macho taasisi za Serikali ambazo zinadaiwa kwa kuwa suala la ulipaji wa Kodi ni suala la kisheria na sio hiari. Dkt Kijazi aliyasema hayo mapema Leo jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mkakati wa makusanyo ya Kodi ya pango la Ardhi Kwa kushirikiana na benki ya CRDB. Alisema kuwa ni muhimu kwa wamiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipa Kodi hizo Kwa wakati ili kuruhusu utekelezaji na mikakati mbalimbali ya…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Tanzania ina Zaidi ya ndege zilizosajiliwa 400 ambazo zimekifanya chuo cha usafirishaji nchini NIT kuanzisha mafunzo ya urubani sanjari na kununua ndege mbili za mafunzo kutoka nchini Marekani zenye thamani ya dola milioni 1.2. Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji nchini NIT Prof. Zakaria Mganilwa ameeleza kwamba asilimia 60 ya marubani nchini wanatoka nje ya nchi hivyo wameona ili kupunguza ombwe la upungufu wa marubani wazawa chuo hicho kimeanzisha mafunzo ya urubani. Amesema Serikali imetenga fedha za kuanzisha kozi mahusisi kiasi cha billion 50 ikiwemo ujenzi wa majengo matano yenye…

Read More

Na Doreen Aloyce, Doreen Katika kuboresha mawasiliano ya kidigit hapa nchini Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imetoa leseni 3132 katika makundi aina 6 ikiwemo leseni ndogo za ufungaji utengenezaji uagizaji usambazaji wa vifaa vya simu 2161. Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Dkt. Jabir Bakari wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya kudhibiti anga ya mawasiliano nchi kuanzia septemba hadi novemba jijini Dodoma Aidha akibainisha Leseni hizo Dkt. Jabir amesema kwamba aina hizo ni pamoja na leseni za miundombinu ya mawasiliano 22, utumiaji wa miundombinu ya mtandao 10,matumizi ya huduma 107,huduma maudhui 741 television…

Read More

Halmashauri ya Wilaya ya Makete kupitia 10% ya mapato yaa ndani imewakopesha vijana pikipiki (bodaboda) 20 kutoka Kata ya Kitulo na Iwawa. Kati ya vijana hao 20, vijana 10 ni kutoka Kata ya Iwawa na Vijana 10 ni kutoka kata ya Kitulo…Mkopo huo ni kiasi cha shilingi Milioni 51 na zitarejeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja bila riba. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Viwanja vya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Makete mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda, Makamu wa Halmashauri Mhe. Hawa Kader, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya William Makufwe, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Clement…

Read More