Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba, 2022 ambacho ni robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022-2023, Tume ya Madini imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 178.01 kwenye madini. Mhandisi Samamba aliyasema hayo jana tarehe 28  Oktoba, 2022 kwenye Kikao cha 16 cha Tume ya Madini kilichofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022-2023. Aliongeza kuwa ili kuvuka lengo lililowekwa na Serikali la kukusanya shilingi bilioni 822…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Mohamed Abdullah amesema kufuatia kuwepo kwa uzinduzi wa matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi ya mwaka huu unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imefikia asilimia 85. Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wakati alipotembelea kukagua uwanja wa Jamhuri ambapo kutafanyika uzinduzi huo mnano oktoba 31 mwaka huu ambapo utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali.Aidha ali Aidha amefafanua kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na hali iliyopo inavyoonekana imefikia zaidi ya asilimia 85 kilichobaki ni kukamilisha mambo madogo…

Read More

Na WyEST, DAR ES SALAAM. Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imepongeza Wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa kuwa na mfumo wa kielektroniki wa usahihishaji mitihani ambao umerahisisha zoezi la usahihishaji mitihani ya Taifa. Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo wakati Kamati ilipofanya ziara katika Taasisi hiyo ambapo mfumo huo kwa sasa unatumika kusahihisha mitihani ya darasa la Saba na Ualimu. Kamati hiyo pia imeishauri Wizara kuwatambua kitaifa Watanzania waliovumbua mfumo huo kutokana na kuwa umejibu changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kufupisha…

Read More

Na John Mhala,Bumbuli Zaidi ya Wakulima 200 wa Mashamba ya Chai katika kata 14 kati ya kata 18 za  Halmashauri ya Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wameanza kunufaika kuuza zao la Chai katika Kiwanda cha Chai cha Mponde kilichofufuliwa na serikali  kwa Uwekezaji wa Shilingi Bilioni 4 Hayo yalisemwa  na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Kalisti  Lazaro wakati alipotembelea kiwanda hicho kujionea uzalishaji  na kuwataka wakulima kuongeza jitihada zaidi katika kilimo cha zao hilo kwa kuwa wataweza kuuza zao hilo eneo la karibu na kunufaika na kujiinua Kiuchumi. Lazaro alisema kuwa kiwanda hicho kilisimama uzalishaji miaka 10 iliyopita lakini mwezi mmoja…

Read More

Na John Mhala,Bumbuli Nyumba tano za Upanuzi wa Mradi wa Kituo cha Afya kata ya Mgwashi Jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga umegharimu zaidi ya shilingi milioni 247.6 hadi sasa Nyumba hizo ni pamoja na jengo la Maabara,jengo la Mochwari,jengo la Upasuaji,jengo la Wazazi na nyumba ya Mtumishi ujenzi wa nyumba hizo umefikia hatua ya asilimia 80 kukamilika. Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mgwashi,Kelvin Shukia alisema mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ,Kalist Lazaro aliyetembelea mradi huo kuwa mradi ulikuwa ukamilike ndasni ya siku 90 ambapo ulikuwa ukamilike julai mosi mwaka huu. Alisema lakini hadi sasa…

Read More