Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha Wizara ya Katiba na Sheria Imeeleza kwamba imejipanga katika mfumo wa Tehama katika utoaji haki nchini utaosaidia kuboresha kurahisisha na kuondoa changamoto za wananchi kufuata huduma umbali mrefu. Aidha Serikali imeweka mazingira mazuri ya mfumo wa kidigiti kuweza kupatikana katika Katiba na sheria sanjari na elimu mtandao ya sheria ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwa urahisi Popoto walipo. Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro wakati akizindua mafunzo ya mifumo ya Tehama kwa sekta ya sheria kwa wadau wa huduma za kisheria kwa siku mbili jijini Arusha.Alisema kwamba katika Bajeti ya…

Read More

Na Julian Laizer Munduli . Wazee wasiojiweza kutoka vijiji vya Mti Mmoja na Lashaine, Kata ya Sepeko na Lashaine wilayani Monduli mkoani Arusha wametatuliwa changamoto ya kimatibabu waliyokuwa wakiipitia kwa kipindi cha muda mrefu kwa kukabidhiwa kadi za bima ya Afya zitakazowasaidia kutibiwa bure. Mbali na kadi hizo wazee hao wamekabidhiwa mashuka mazito kwa ajili ya kujifunika usiku na kuzuia baridi na hapa wanaeleza namna walivyotwaliwa mzigo wa matibabu. Wakizungumza baadhi ya wazee , akiwemo mzee Lowasare Loderieki, Maria Saitoti na Leparakwo Melakiti , kwa pamoja wameshukuru shirika la DIVINE MERCY CARE AFRICA (DMCA) chini ya Mkurugenzi wake Lekoko Kipuyo…

Read More

Moses Mashalla,Arusha Mfanyabiashara wa madini ya vito ambaye aliwahi kutajwa kuwa bilionea wa madini aina ya Spinner,Salim Alaudin maarufu kama “Salim Almasi” amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kukutana na wafanyabiashara wa sekta ya madini nchini ili waweze kumweleza changamoto wanazopitia. Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Ulanga ametoa kauli hiyo wakati akihojiwa na waandishi wa habari ofisini kwake. Akizungumza na waandishi wa habari Mfanyabiashara huyo amesema kwamba Rais Samia ni vyema akaitisha kikao na wadau wa sekta ya madini nchini kama ambavyo anakutana na makundi mbalimbali ndani ya jamii. “Rais Samia ni…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Madini imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Sekta ya Madini inanufaisha kila mwananchi na kuinua sekta nyingine za kiuchumi na uchumi kuendelea kukua kwa kasi. Profesa Kikula ameyasema hayo leo Oktoba 13, 2022 jijini Mwanza kwenye kikao cha nne cha Baraza la Wafanyakazi kilichoshirikisha Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Nsubisi Mwasandende, Mwakilishi wa Kamishna wa Kazi – Ofisi ya Waziri Mkuu, Goodluck Luginga, watendaji kutoka Tume…

Read More

Na WyEST Kagera Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania anatarajiwa kupokea na kuzindua Chuo kipya cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Kagera. Halfa hiyo inatarajiwa kufanyika Alhamis tarehe 13 Oktoba, 2022. Katika Chuo hicho kipya kilichopo Burugo Nyakato Kagera. Chuu hicho chenye karakana, vifaa na miundo mbinu ya kisasa kimejengwa kwa msaada wa Serikali ya China kitakuwa na uwezo wa kuchikua wanafunzi zaidi ya 1,400 kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika fani mbalimbali za ufundi na huduma. Hayo yameelezwa na Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipokagua maandilizi ya halfa hiyo…

Read More