Author: Geofrey Stephen

Njombe Wananchi wa kijiji cha Igombola kata ya Lupembe wilayani Njombe wameomba serikali kupitia Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa kuondoka na mganga wa zahanati ya kijiji hicho wakimtuhumu kukosa nidhamu,ulevi pamoja na kushindwa kutibu wagonjwa mpaka watoe fedha za matibabu wakiwemo wazee. Katika mkutano wa hadhara wa Mkuu wa wilaya hiyo wakati akisikiliza kero pamoja na kukagua miradi ya maendeleo,wananchi wamedai kuwa daktari Samweli Tupa amekuwa na changamoto zinazopelekea vifo kwa wagonjwa hali inayowafanya kuwa na wasi wasi mkubwa wa maisha yao ndio maana wamefikia hatua ya kuomba aondolewe Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa mara baada…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Wananchi wengi kutoka katika mkoa wa Pwani na mikoa ya jirani wameomba elimu kuhusu madini kujumuishwa kwenye mitaala ya shule za msingi na sekondari na kuhamasisha wanafunzi wengi kujiunga zaidi kwa shahada ya jiolojia katika vyuo vikuu nchini na kuongeza wataalam kwenye Sekta ya Madini. Waliyazungumza hayo kwenye kilele cha Maonesho ya Tatu ya Uwekezaji na Biashara yaliyofanyika katika Viwanja vya SIDO, Maili Moja Mkoani Pwani Oktoba 10, 2022 ambayo yalilenga kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa wa Pwani. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao waliomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kushirikiana na Wizara…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv _Ni kupitia kasi ya utoaji wa leseni za madini 9,498 mwaka 2021-2022_ _Uanzishwaji wa masoko 42 na vituo vya ununuzi wa madini 83_ _Leseni za madini 9,498 zatolewa mwaka 2021-2022_ Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Tume, Sekta ya Madini imeendelea kuimarika kutokana na mafanikio yaliyopatikana ndani ya muda mfupi ikiwa ni pamoja na kasi ya ukusanyaji wa maduhuli, uanzishwaji wa masoko na vituo  vya ununuzi wa madini nchini na utoaji wa leseni za madini. Profesa Kikula ameyasema hayo leo Oktoba 11, 2022 jijini Mwanza  kwenye kikao cha Tume…

Read More

Na Emmanuel octavian Katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Njombe baadhi ya wakazi hao akiwemo Peter Kyamani na Lucy Mligo Wamesema ubovu wa barabara hasa wakati wa masika umekuwa ukikatisha mawasiliano pamoja na mazao kuozea shambani. Awali diwani wa kata ya Lupembe Michael Mbanga amesema changamoto ya miundombinu ya barabara ni kubwa hususani katika kipindi cha masika kwani shughuli za kiuchumi zimekuwa zikisimama. Mtaalam wa ujenzi toka Wakala wa barabara za mijini na vijjini TARURA wilaya ya Njombe Mhandisi Mussa Mwansule amekiri kuwapo kwa changamoto ya miundombinu hiyo huku akisema itatazamwa katika bajeti ya mwaka ujao kwani…

Read More

Na Mwadishi wa A24Tv Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Dkt Ashatu Kijaji ( Mb.) amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha viwanda vya nguo nchini vinavyoajiri watu wengi hususani wanawake na vijana vinafanya kazi kwa ufanisi ili kuongeza ajira, pato la taifa, kukuza biashara ya ndani na nje ya nchi na uchumi kwa ujumla. Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha nguo cha A TO Z Bw. Kalpesh Shah akiwa na Meneja Mauzo ya Nje wa Kiwanda hicho Bw. Sylvester Kazi Oktoba 10, 2022 katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara – Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Serikali imetoa vivutio vya uwekezaji katika Sekta ya Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba ikiwemo kupunguza Kodi ya Makampuni (corporate tax) kutoka 30% mpaka 20% kwa viwanda hivyo vipya kwa miaka mitano ya mwanzo ya uwekezaji sambamba na kutoa kodi kwenye vifungashio vya dawa. Dkt Abdallah ameyasema hayo alipokuwa akizindua Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Masuala ya Viwanda vya Dawa na Vifaa Tiba na Warsha ya kutoa maoni kuhusu Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Kuendeleza Sekta ya…

Read More

Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda ameiamuru mamlaka ya usimamizi wa vyombo vya usafiri wa moto (Latra) mkoani Arusha kusitisha mara moja utoaji wa leseni za usafirishaji wa Bajaj mpaka pale serikali itakapojiridhisha mahitaji na idadi ya bajaji hizo jijini Arusha. Pia amelielekeza jeshi la polisi mkoani Arusha kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya madereva bajaj jijini hapa ambao wamedaiwa kutumia silaha za mapanga,visu na nondo kuwashambulia madereva wa dalaladala hali ambayo imeibua mgogoro baina yao. Mtanda ametoa kauli hiyo leo katika soko la Kilombero mara baada ya kufika hapo kutatua mgomo wa madereva wa daladala ambao walianzisha mgomo…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Serikali imesema imeweka mkakati wa kufufua vituo vya walimu (Teachers Resource Centers) vya nchi nzima ili kuwawezesha walimu kupata sehemu ya kukutana na kubadilishana uzoefu pamoja na kujiendeleza kwa kujisomea Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda wilayani Bukombe wakati akiongea na walimu wa wilaya hiyo katika kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambapo amesema mbali ya kufufua vituo hivyo pia inaendelea kutoa mafunzo kazini kwa walimu. Prof. Mkenda amesema walimu wameandaliwa vizuri vyuoni lakini hiyo haitoshi kwa kuwa kila siku mambo yanabadilika na walimu wanapaswa kuendelea kujifunza kila mara…

Read More