Author: Geofrey Stephen

Na Doreen Aloyce, Dodoma WAKALA wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ADEM imesema kuwa imejipanga kutoa Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Shule kwa Walimu Wakuu wapatao elfu 17,000, mafunzo hayo yakiwa ni kutoa mafunzo ya utawala bora kwa wasimamizi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ADEM Dkt Siston Mgullah wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wakala huo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa 2022/2023 Amesema Katika kipindi cha mwaka 2021/2022, Wakala umeweza kushirikiana na…

Read More

mwandishi wetu,Tanga Wafanyabiashara wadogo katika mpaka wa Tanzania na Kenya, eneo la Horohoro na Lungalunga ,wametaka serikali za Tanzania na Kenya, kuondoa vikwazo vya kibiashara ,hasa baada ya kukamilika miundombinu ikiwepo barabara ya Tanga- Horororo. Barabara la lami ya Tanga- Horohoro, imejengwa na Serikali ya Marekani kupitia miradi ya malengo ya milenia(MCC). Wakizungumza na mwandishi habari hizi, katika mpaka huo, baadhi ya wafanyabiashara wadogo wa Kenya na Tanzania, walitaka serikali za Kenya na Tanzania, kuendelea kupunguza vikwazo ili biashara iwe rahisi zaidi baina ya nchi moja hadi nyingine, hasa ya mazao, mifugo na bidhaa za ndani. Joseph Mwanganya mfanyabishara mdogo…

Read More

Mgogoro waibuka Burunge WMA , Kampuni ya kitalii ikitaka kuwinda Pembezoni mwa Tarangire Bodi ya wadhamini yampinga spika . . Tarangire ndio hifadhi nyenye Tembo wengi na wakubwa wanaoishi eneo Moja Afrika Mwandishi wetu, Babati .Vita ya kutaka kuwinda wanyamapori baina ya makampuni yameingiza katika mgogoro Jumuiya ya Hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Burunge, Wilaya ya Babati,mkoa wa Manyara baada ya spika wa Jumuiya hiyo kutangaza Kitalu cha uwindaji kipo wazi bila ridhaa ya Bodi ya wadhamini . Wakati spika akiwa amesaini barua ya kutangaza Kitalu hicho kutaka kampuni kuomba kuwinda ,tayari Bodi ya jumuiya hiyo Julai 14,2022 ilisaini…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha .  Jiji la Arusha limekabidhi hundi ya mkopo yenye thamani ya sh, milioni 404.5 kwa vikundi 52 vya ujasiriamali kutoka kata 25 za jiji la Arusha. Akiongea wakati wa kukabidhi hundi  hiyo jana, kaimu mkurugenzi wa jijj la Arusha Hargeney Chitukulo,alisema mkopo huo ni awamu ya pili kwa vikundi vya ujasiriamali. Alisema kati ya vikundi hivyo ,28 ni vya akina mama waliopata sh, milion 198.6 na vikundi 14 vya vijana waliopata sh, milioni 143. Alisema wengine walionufaika na mkopo huo usio na riba ni vikundi 10 vya walemavu ,waliopata sh, milioni 62.9. Chitukulo alisema kuwa mkopo …

Read More