Author: Geofrey Stephen

Na Dorice Aloyce Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameeleza kuwa uwepo wa vivutio vizuri na vya kipekee vya Utalii katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania ni fursa kwa wananchi wa mikoa hiyo kuendelea kunufaika kiuchumi kutokana na shughuli za utalii zinazofanyika. Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo leo Novemba 10, 2022 mkoani Iringa alipokuwa akifungua rasmi Maonesho ya Utalii Karibu Kusini yaliyohudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka katika mikoa kumi ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Morogoro, Songwe, Rukwa na Katavi. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ametoa wito…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma. KATIKA kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi wa wahandisi nchini,Bodi ya wahandisi (ERB) imesema imeweka mipango ya kukuza na kuimarisha weledi wa sekta ikiwemo na kupambana na vitendo vya rushwa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 10 jijini Dodoma wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Msajili wa Bodi ya wahandisi Bernad Kavishe amesema Bodi itaweka maslahi ya Umma mbele ikiwemo na kuzingatia maadili. “Wahandisi pia lazima wadhibitiwe wawe na nidhamu na maadili mema wawe na uadilifu na kwa kifupi wahandisi tunaweka maslahi ya Umma mbele na…

Read More

Na Geofrey  Stephen  Arusha Kiongozi mkuu wa huduma ya Ngurumo ya upako yenye makao makuu jijini Arusha,Dkt Nabii Geor Davie ameendelea kuwa baraka kwa wahitaji wenye mahitaji ya kimwili pamoja na kiroho kwa kuwapa mitaji Aidha Nabii Dkt Geor Davie amekuwa mwangaza hata kwa taasisi za Serikali kwa kuwa amejijengea tabia ya kuwasaidia kwenye maitaji mbalimbali. Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti na Mwandishi wa habari hizi waliofanikiwa kupewa mitaji na misaada kutoka Nabii Dkt Geor Davie walisema kuwa anafanya yale ambayo yameandikwa katika maandiko matakatifu “Baba amekuwa ni msaada mkubwa sana hasa kwa jamii ambazo zinawaitaji,ukiangalia hata upande wa wasanii…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Serikali kupitia wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa imetoa fidia ya fedha kiasi cha shilingi milioni 243.7 kwa ajili ya wananchi 160 wa vijiji vya choda na mkiwa wilaya ya Ikungi. Akizungumza wakati wa kikao cha utoaji wa taarifa za mapokezi ya fedha hizo, Mkuu wa wilaya ta Ikungi Mhe. Jerry C. Muro amesema Mheshimiwa Rais. Samia Suluhu Hassan ameridhia fedha hizo kutolewa kwa wananchi 112 wa kijiji cha mkiwa na wananchi 48 wa kijiji cha Choda mara baada ya kufanyiwa uthamini na kukamilisha taratibu zote za kisheria za ulipwaji wa fidia. Kwa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Taharifa kwa wananchi Tunapenda kuwajulisha kwamba SHAURI (kesi) ya Kikatiba Namba 14 ya mwaka 2022 iliyofunguliwa na MARY BARNABA MUSHI wa Shirika la Women and Children Welfare Support katika Mahakama Kuu Masijala Kuu ya Dar es Salaam dhidi ya Wakili Mkuu wa Serikali kupinga mchakato wa kukusanya maoni kuhusu MABORESHO YA SHERIA YA NDOA ,uliotangazwa na Waziri wa Sheria na Katiba Dk Damas Daniel Ndumbaro (MB) imetajwa leo Tarehe 09 November 2022 Mbele ya Muheshimiwa Jaji Mosses Gunga Mzuna ambapo waleta maombi wamepewa siku mbili (2) kuwasilisha maombi ya nyongeza (Rejoinder ) na Tarehe 15…

Read More

Na Doreen Aloyce,Dodoma MFUKO wa Hifadhi ya Jamii wa PSSSF umesema unatarajia kuanza kuwalipa Watumishi waliokutwa na Vyeti Feki Jumla ya Shilingi Bilioni 20 ndani ya siku60takribani watumishi9000 mara baada tu yakupokea madai yao kutoka kwa waliyokuwa Waajiri wao. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo,ACP Hosea Kashimba ameyaeleza hayo Leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Mfuko wa PSSSF na mwelekeo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023. ACP Kashimba amebainisha kuwa hadi kufikia Mwezi Juni Mwaka2022Mfuko huo ulikuwa na Uwekezaji wenye thamani ya Shilingi Trlioni 7.5kwaajili ya kufanya uendelevu wa Mfuko huo. “Mafao…

Read More

Na Geofrey Stephen  Arusha MKUU wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amewataka watunzi wa vitabu  vya elimu hapa nchini ,kuanza mabadiliko ya kuingiza machapisho ya vitabu  kwenye  mfumo wa maktaba mtandao ili kuwafikia wasomaji  waliowengi kupata taarifa kwa gharama  nafuu Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizindua mfumo  wa usomaji wa vitabu mtandaoni katika chuo cha uhasibu Arusha (IAA)  unaoratibiwa na shirikisho la Maktaba za vyuo vikuu na taasisi zilizofanya utafiti COTUL. Alisema kwa sasa dunia  imeingia kwenye mabadiliko ya kimfumo na hivyo vitabu vyote vinavyochapishwa hapa nchini vinapaswa kuingizwa kwenye mfumo wa kisayansi na teknolojia…

Read More

WATU sita kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, sita wa kada ya afya na mmoja mwalimu, wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali maeneo ya  pori namba moja Wilayani Kiteto Mkoani Manyara. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kiteto, marehemu wawili ni mtu na mke wake, na walikuwa na mtoto wao wa miezi tisa ambaye amenusurika Akithibitisha ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga amesema majeruhi watano wamepelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi na wawili wamebaki katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto. Amesema ajali hiyo ilihusisha Gari la wagonjwa wa kituo cha…

Read More