Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha . Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 15.01.2025 kwa niaba ya Kamishna Jenerali imeteketeza dawa za kulevya kilogramu 185.35 katika Dampo la Maji ya Chai liliopo wilayani Arumeru katika Mkoa wa Arusha. Katika dawa hizo zilizoteketezwa, mirungi ilikuwa kilogramu 154.35 na bangi mbichi ilikuwa kilogramu 31 ambapo jumla ya watuhumiwa watano walikamatwa kwa makosa ya kupatikana na dawa hizo. Uteketezaji wa dawa hizo umefanyika kwa kuzingatia taratibu zote za kisheria ambapo Mahakama ya Wilaya ya Arumeru iliridhia vielelezo hivyo viteketezwe kwani uwezekano wa kuleta madhara kwa binadamu ni…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ameweka jiwe la msingi la Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi ya Bahari, Buyu, Akizungumza baada ya kuweka jiwe la Msingi  Zanzibar Dkt. Mwinyi amesema kuwa taasisi hiyo itasaidia kuendeleza uchumi wa bluu kupitia tafiti na mafunzo ya wataalamu wa sekta za uvuvi, utalii, na mazao ya baharini. Ameongeza kuwa Mradi huo wa zaidi ya Shilingi bilioni 11 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia utaboresha elimu ya juu na kuongeza wataalamu wa uchumi wa bluu. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amesema mkopo…

Read More

Na mwandishi wetu Zambia Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, wakiongozwa na Mbunge wa Geita Mjini anayemwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu wako nchini Zambia katika ziara ya mafunzo kuhusu Uongezaji Thamani Madini. Mhe. Kanyasu ameambatana na wajumbe wengine watatu wa Kamati hiyo akiwemo Mhe. Ndaisaba Ruhoro, Mhe. Aleksia Kamguna na Mhe. Janeth Mahawanga pamoja na Katibu wa Kamati, Bw. Chacha Nyakenga. Kwa upande wa Wizara, ujumbe huo unawakilishwa na Kamishna Msaidizi Sehemu ya Uongezaji Thamani Madini Bw. Archard Kalugendo. Ziara hiyo, iliyoandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na…

Read More

Na Geofrwey Stephen Arusha . Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani kimesema kuwa baada ya kuhitimisha zoezi la ukaguzi wa magari ya shule(School Bus) kwa kipindi cha likizo ambacho kilitangazwa ili kuondoa usumbufu kwa wanafunzi wanaotumia vyombo hivyo kimeanza kuwakamata wale wote walio kaidi agizo hilo huku kikosi hicho kikiwaomba wananchi kuweka uangalizi wa kundi hilo. Akiongea katika zoezi hilo Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Zauda Mohamed amesema kuwa kikosi hicho kilitangaza zoezi hilo ambapo ameweka wazi kuwa wameanza operesheni za ukamataji wa magari ambayo haya jakaguliwa na kikosi hicho.…

Read More