Author: Geofrey Stephen

Na Doreen Aloyce, Doreen Katika kuboresha mawasiliano ya kidigit hapa nchini Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imetoa leseni 3132 katika makundi aina 6 ikiwemo leseni ndogo za ufungaji utengenezaji uagizaji usambazaji wa vifaa vya simu 2161. Haya yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Dkt. Jabir Bakari wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya kudhibiti anga ya mawasiliano nchi kuanzia septemba hadi novemba jijini Dodoma Aidha akibainisha Leseni hizo Dkt. Jabir amesema kwamba aina hizo ni pamoja na leseni za miundombinu ya mawasiliano 22, utumiaji wa miundombinu ya mtandao 10,matumizi ya huduma 107,huduma maudhui 741 television…

Read More

Halmashauri ya Wilaya ya Makete kupitia 10% ya mapato yaa ndani imewakopesha vijana pikipiki (bodaboda) 20 kutoka Kata ya Kitulo na Iwawa. Kati ya vijana hao 20, vijana 10 ni kutoka Kata ya Iwawa na Vijana 10 ni kutoka kata ya Kitulo…Mkopo huo ni kiasi cha shilingi Milioni 51 na zitarejeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja bila riba. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Viwanja vya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Makete mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda, Makamu wa Halmashauri Mhe. Hawa Kader, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya William Makufwe, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Ndg. Clement…

Read More

Njombe Na Emmanuel octavian Wakulima mkoani Njombe wameshauri wawekezaji waachane na biashara ya kuwekeza mashambani na badala yake wawekeze kwenye viwanda vitakavyowasaidia wao kupeleka mazao yao. Katika mkutano mkuu wa mtandao wa vikundi vya wakulima MVIWATA Tanzania katika mikoa ya Njombe na Iringa baadhi ya wanachama hao ambao ni wakulima wanasema kitendo cha wawekezaji kwenda kuwekeza mashambani kinawanyima fursa wakulima ambao ndio wahusika wakuu katika sekta ya kilimo. Hosea Mangula,Sikujua Mbata,John Kiswaga na Sarah kaduma ni baadhi ya wakulima wanaosema wawekezaji wanaoingia mashambani kuwekeza pia wanasababisha kuibuka kwa migogoro ya ardhi inayochochea chuki baina ya wakulima, Wawekezaji na serikali inayowaruhusu…

Read More

Doreen Aloyce, Dodoma Serikali imesema katika kutekeleza maboresho ya mazingira ya Biashara hapa Nchini Imeanzisha kitengo maalumu kinachoitwa _Business Inviroment Unit_ (BIU) ambacho kitasimamia sekta zote za kibiashara ili kubainisha Changamoto na kero zilizopo katika Biashara na kuzifanyia utatuzi kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali zikiwemo za kisera na mamlaka za kodi. Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya semina na kamati ya kudumu ya bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira Bungeni Dodoma , Naibu waziri Wizara ya Uwekezaji , Viwanda na Biashara Mh. Exaud Kigahe amesema kuwa mpango huo unaojulikana kama Blueprint utajikita kusimamia changamoto zote katika sekta mbalimbali zinazolalamikiwa…

Read More

Mwandishi wetu, Babati Mzuka wa Nusu Fainali ya michuano ya Chemchem CUP 2022, inatarajia kuanza leo, ambapo timu ya Mshikemshike FC ya vilima vitatu itachuana na Timu ya Macklion kutoka kijiji cha Mwada wilaya ya Babati mkoa Manyara Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu 16 kutoka katika vijiji 10 ambavyo vinaunda jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge zaidi ya sh 25 milioni zinatarajiwa kutumika, ambapo awali timu zote zilipewa seti ya jezi na mipira. Nusu fainali ya pili ya michuano hiyo, timu ya Mdori FC ya kijiji cha Mdori itachuana na timu ya Mofuri FC ambayo pia inatoka katika kijiji…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara – Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amezishauri Taasisi za umma pamoja na watendaji wake wanaotoa huduma kuhakikisha wanaweka mazingira bora ya biashara na uwekezaji ili kifikia malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita na kuliwezesha Taifa kufikia uchumi wa Kati wa Juu. Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah katika ufunguzi wa semina ya Wajumbe wa Baraza la Ushindani iliyofanyika Novemba mosi (1) 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Uvuvi, Mbegani, Bagamoyo amesema mazingira bora na wezeshi ni muhimu…

Read More

Mkuu wa mkoa wa Arusha,John Mongella amekitaka chuo cha ufundi Arusha ATC,kuhakikisha huduma zitakazotolewa katika  mradi wa hospitali unaojengwa chuoni hapo,unaimarisha sekta ya afya  nchini  na kukidhi mahitaji ya afya kwa wanafunzi  , jamii na  watalii. Akiongea mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa jengo la hospitali ya kufundishia na Tiba ( Polyclinic )katika chuo hicho ,alisema Kliniki hiyo ikikamilika isaidie kutoa huduma za kiwango cha juu kwa wanafunzi kujifunzia na tiba kwa wananchi. Alisema kuwa ubora wa huduma zitakazotolewa katika hospitali hiyo uwe wa kiwango cha juu na uendane na hadhi ya majengo na kukidhi…

Read More

Na Geofrey Stephen Lushoto . WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), kupitia shamba la Miti la  Shume,lililopo Wilayani Lushoto, Mkoa wa Tanga katika mwaka wa fedha 2022/23 imepanga kukusanya mapato ya serikali ya shilingi Bilioni 3.7. Makusanyo hayo yanatokana na mauzo ya mazao ya miti na zao la nyuki  . Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea shamba hilo katika ziara ya Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Kalisti Lazaro,Mhifadhi Mwandamizi wa Shamba hilo,Ernest Madata alisema mwaka wa fedha 2020/21 walishindwa kufikia malengo ya kukusanya sh,bilioni 3.8 waliojiwekea na kukusanya sh,bilioni 2.2 sawa na asilimia 59.4. Alisema kutofika kwa malengo hayo  kulichangiwa…

Read More