Na Mwqndishi wa A24Tv Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Jerry C. Muro leo tarehe 01/11/2022 amemuelekeza mkuu wa takukuru wilaya ya Ikungi kuanza uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili watumishi watatu waliokuwa wanasimamia ujenzi wa kituo cha afya kata ya Irisya tarafa ya Sepuka jimbo la singida magharibi. Pamoja na hatua hiyo pia amemuelekeza Mkurugenzi wa halmashauri ya Ikungi Mhe. Justice Lawrance kupeleka team ya uchunguzi ambayo itakuwa na lengo la kuchunguzi mienendo ya tabia za watumishi hao watatu ili pia waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi za halmashauri Dc Muro amesema hatua hiyo imekuja baada ya mradi…
Author: Geofrey Stephen
Na Emmanuel mkulu Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Adelina Ng’olo mwenye umri wa miaka 36 mkazi wa Nyombo wilayani Njombe kwa tuhuma za kuwachoma moto watoto wake wawili katika sehemu mbalimbali za miili yao kwa kile alichodai wamemdharirisha kwa kuomba chakula kwa majirani. Mbele ya vyombo vya habari Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa Amewataja watoto hao waliochomwa moto kuwa ni Eliud Chatanda[7] na Elina Chatanda mwenye umri wa miaka[4] ambao walikwenda kwa majirani kutafuta chochote ili mradi siku iende lakini majirani wakaanza kumsema mama huyo kuwa anashindwa kuwalea watoto wao mpaka wanakuwa ombaomba Kamanda Issa amesema…
Karibu Arusha 24Tv leo November 1 2022 Kutazama Kilicho Andikwa Katika Magazeti ya Leo ya Tanzania Mbelena Nyuma Hii ni A24Tv.
Karibu Arusha24Tv Leo October 31 Kutazama Kilicho Andikwa Katika Magazeti ya Leo ya Tanzania Mbele na Nyuma Hii ni A24Tv .
Na Mwandishi wa A24Tv Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba, 2022 ambacho ni robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022-2023, Tume ya Madini imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 178.01 kwenye madini. Mhandisi Samamba aliyasema hayo jana tarehe 28 Oktoba, 2022 kwenye Kikao cha 16 cha Tume ya Madini kilichofanyika Jijini Dodoma kwa lengo la kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2022-2023. Aliongeza kuwa ili kuvuka lengo lililowekwa na Serikali la kukusanya shilingi bilioni 822…
Na Doreen Aloyce, Dodoma MAKAMU wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemed Mohamed Abdullah amesema kufuatia kuwepo kwa uzinduzi wa matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi ya mwaka huu unaotarajiwa kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan imefikia asilimia 85. Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wakati alipotembelea kukagua uwanja wa Jamhuri ambapo kutafanyika uzinduzi huo mnano oktoba 31 mwaka huu ambapo utahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali.Aidha ali Aidha amefafanua kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na hali iliyopo inavyoonekana imefikia zaidi ya asilimia 85 kilichobaki ni kukamilisha mambo madogo…
Na WyEST, DAR ES SALAAM. Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imepongeza Wizara ya Elimu na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) kwa kuwa na mfumo wa kielektroniki wa usahihishaji mitihani ambao umerahisisha zoezi la usahihishaji mitihani ya Taifa. Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo wakati Kamati ilipofanya ziara katika Taasisi hiyo ambapo mfumo huo kwa sasa unatumika kusahihisha mitihani ya darasa la Saba na Ualimu. Kamati hiyo pia imeishauri Wizara kuwatambua kitaifa Watanzania waliovumbua mfumo huo kutokana na kuwa umejibu changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kufupisha…
Karibu Arusha 24Tv leo October 30 kutazama kilicho Andikwa katika magazeti ya leo ya Tanzania Mbele na Nyuma Hii ni A24Tv .
Na John Mhala,Bumbuli Zaidi ya Wakulima 200 wa Mashamba ya Chai katika kata 14 kati ya kata 18 za Halmashauri ya Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga wameanza kunufaika kuuza zao la Chai katika Kiwanda cha Chai cha Mponde kilichofufuliwa na serikali kwa Uwekezaji wa Shilingi Bilioni 4 Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Kalisti Lazaro wakati alipotembelea kiwanda hicho kujionea uzalishaji na kuwataka wakulima kuongeza jitihada zaidi katika kilimo cha zao hilo kwa kuwa wataweza kuuza zao hilo eneo la karibu na kunufaika na kujiinua Kiuchumi. Lazaro alisema kuwa kiwanda hicho kilisimama uzalishaji miaka 10 iliyopita lakini mwezi mmoja…
Karibu Arusha 24Tv Leo October 29 Kutazama Kilicho Andikwa Katika Magazeti ya Leo Ya Tanzania Mbele na Nyuma Hii ni A24Tv