Author: Geofrey Stephen

Na John Mhala,Bumbuli Nyumba tano za Upanuzi wa Mradi wa Kituo cha Afya kata ya Mgwashi Jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga umegharimu zaidi ya shilingi milioni 247.6 hadi sasa Nyumba hizo ni pamoja na jengo la Maabara,jengo la Mochwari,jengo la Upasuaji,jengo la Wazazi na nyumba ya Mtumishi ujenzi wa nyumba hizo umefikia hatua ya asilimia 80 kukamilika. Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mgwashi,Kelvin Shukia alisema mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ,Kalist Lazaro aliyetembelea mradi huo kuwa mradi ulikuwa ukamilike ndasni ya siku 90 ambapo ulikuwa ukamilike julai mosi mwaka huu. Alisema lakini hadi sasa…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa ya kuwania Tuzo za Ubora za Kitaifa kwa mwaka 2022/2023 ambazo zinahusisha Sekta mbalimbali na watu binafsi wanaofanya vizuri kwenye masuala ya Ubora ambazo zitasaidia kuitangaza nchi. Akizungumza na Vyombo vya Habari (leo) jana Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Tuzo za tatu za Ubora za Kitaifa Mwaka 2022/2023 Kaimu katibu mkuu wizara ya uwekezaji, Viwanda na Biashara Aristides Mbwasi amesema kuwa tuzo hizo zitaleta fursa ukuaji na maendeleo ya sekta ya viwanda na Biashara. Amesema mashindano ya Tuzo hizo ni pamoja na Tuzo kwa kampuni bora , tuzo kwa bidhaa bora…

Read More

Taasisi ya EBN yachimba mabwawa kusaidia wanyamapori kukabiliana na Ukame. Mwandishi wetu. Babati.Taasisi EBN ambayo inamiliki Kitalu Cha uwindaji katika eneo la jumuiya ya uhifadhi wa Wanyamapori ya Burunge ,imechimbwa bwawa ili kusaidia wanyamapori kupata maji. Uamuzi huo umefikiwa kutokana na Ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi umeanza kusababisha vifo kwa wanyamapori katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Burunge(WMA) wilaya ya Babati mkoa wa Manyara. Burunge WMA ipo kati kati ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Hifadhi ya Taifa ya Manyara na inaundwa na vijiji 10 ikiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 24,319. Licha…

Read More

Na Geofrey Stephe Lushoto Zaidi ya shilingi Bilioni 3.2 zimetumika katika Ujenzi wa jengo la Utawala la ghorofa mbili katika jimbo la Bumbuli Wilayani Lushoto Mkoani Tanga. Jengo hilo ambalo litakuwa na vyumba 72 vya watumishi wa idara zote za Halmashauri ya Jimbo hilo linatarajiwa kukamilika ifikapo desemba mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitembelea miradi ya maendeleo katika Jimbo la Bumbulu,Mkuu wa Wilaya ya Lushoto,Kalist Lazaro alisema kuwa bajeti ya ujenzi wa ofisi za Halmashauri ni kiasi cha shilingi bilioni 4 na ujenzi umefika asilimia 90 mpaka kukamilika kwake. Lazaro alisema kuwa Jimbo la Bumbuli lenye kilimo…

Read More

Na Geofrey Stephen . Lushoto AKINA MAMA zaidi ya 250,000 katika Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wanatarajia kuondokana na changamoto ya vifo vya watoto wachanga baada ya serikali kujenga hospitali ya kubwa ya kisasa ya mama na mtoto yenye thamani ya zaidi ya bilioni 1.3 Muonekano wa Jengo la Kisasa la  Hospital ya Mama na Mtoto  Akiongea na vyombo vya habari katika ziara yake ya  kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali wilayani humo ikiwemo  hospitali hiyo, Mkuu wa Wilaya hiyo,Kalisti Lazaro alisema kuwa mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na kukamilika kwake kutaondoa changamoto ya…

Read More

Na Geofrey Stephen ,Lushoto Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga,Kalist Lazaro amewataka Wakurugenzi wa Kampuni ya M/S PNR SERVICES ya Jijini Dar es Salaam waliopewa zabuni ya shilingi Bilioni 1.8 ya kuvuta maji km 14 kutoka Hifadhi ya Msitu wa Magamba hadi katika Mji wa Lushoto kujisamilisha wenyewe ofisini kwake kwa nini hadi Sasa wameifanya kazi hiyo kwa asilimia 20 tu. wakati mradi huo wanapaswa kuukabidhi kwa Mamlaka ya maji Lushoto(RUWASA) januari 30 mwaka kesho. Lazaro alisema hayo katika chanzo Cha maji Cha Msitu huo alipotembelea Mradi huo na kusikitishwa kuona Mkandarasi amelipwa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt.Emanuel Ng’umbi amesema kuwa Taasisi imefanikiwa kuwafikia wasichana 3,333 sawa na asilimia 111 ya lengo ambao walishindwa kuendela na shule ya sekondari kutokana na mazingira magumu, kupata ujauzito na ndoa za utotoni. Dkt. Ng’umbi ambapo ameyabainisha leo Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa wameendesha mafunzo kwa nyakati tofauti kwa wasimamizi na watendaji, wawezeshaji na walimu wa madarasa ya mradi wa SEQUIP. “Kwa mwaka 2022/2023, TEWW itaendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Tekonolojia katika kuandaa Juma la Elimu ya Watu Wazima kwa mwaka 2023,Vile vile, TEWW itahamasisha,…

Read More