Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Dar es Saalam Sekretarieti ya Chama cha TLP kimemchagua Hamad Mkadam kurithi kwa muda nafasi  ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Augustine Mrema. Mrema alifariki Agosti 21, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa akipatiwa matibabu. Uchaguzi huo umefanyika leo Ijumaa Septemba 9, 2022 katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho Magomeni, Hamad Mkadamu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho upande wa Zanzibar ameshinda kwa kura nne dhidi ya  mpinzani wake Dominata Rwechungura (Bara) aliyepata kura mbili kati ya kura sita zilizopigwa na wajumbe sita. Akizungumza leo, Ijumaa Septemba 9, 2022 Katibu…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Katika kuakikisha vijana wanajikwamua katika ajira kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo SERIKALI kwa kushirikiana na Shirika la viwanda vidogo SIDO,kupitia mradi wa wanagenzi , imewawezesha vijana wapatao 130 mkoani Arusha ,kupata mafunzo ya ujasiriamali kupitia viwanda vidogo ,ambayo yamewasaidia kuwapatia ujuzi na uthubutu katika sekta hiyo. Hayo yamebainishwa na Katibu tawala Rasilimali watu Mkoani hapa,David Lyamongi wakati akifunga mafunzo ya mwezi mmoja kwa vijana hap 130 waliohitimu mafunzo ya viwandani  pamoja na kuwatunuku vyeti wanagenzi, iliyofanyika jijini Arusha. Lyamongi ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela,alitoa rai kwa wahitimu hao kuhakikisha wanatumia uzoefu…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Singida Arusha.Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu(LHRC) kimeanza kutoa bure ushauri wa kisheria kwa wananchi wa mkoa wa Singida. Akizungumza na waandishi,Wakili Hamis Mayombo alisema zoezi hilo ambalo limeanza jumatatu wiki hii litakuwa la wiki moja. Wakili Mayombo amesema hadi Sasa mashauri mengi ambayo wamekuwa wakipokea ni migogoro ya ardhu,masuala ya mirathi na utawala bora, baadhi yatafikishwa mahakamani na mengine kupatiwa suluhu. Wakili Mayombo ambaye ni Mkuu wa LHRC Ofisi ya Arusha,alisema mashauri ya ndoa yanatokana na migogoro ya kifamilia huku migogoro ya ardhi ikitokana na uvamizi wa ardhi. Wakili w Fides Mwenda alisema baadhi…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatarajia kuanza ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 62 ambazo hazina vyuo hivyo. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga (Mb) katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii cha uwasilishaji wa utekelezaji wa mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 kilichofanyika Septemba 6, 2022 Jijini Dodoma Mhe. Kipanga ameieleza Kamati hiyo kuwa katika Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara imetenga jumla ya Shilingi bilioni 100 ambazo zitawezesha…

Read More

Mahakama ya juu imeidhinisha Uchaguzi wa William Ruto kuwa rais mteule wa Kenya baada ya kesi iliowasilishwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi huo Raila Odinga kukosa ushahidi wa kutosha. Wakitoa uamuzi wao wa pamoja, majaji hao walioongozwa na jaji mkuu Martha Koome walisema kwamba ushahidi uliotolewa na mlalamishi Raila Odinga ulikuwa umejaa uvumi na porojo. Akiangazia maswala tisa ya kesi hiyo, Jaji Martha Koome amesema kuwa mshindi wa uchaguzi huo William Ruto alifanikiwa kupita kikwazo cha kura asilimia 50 na moja ya kikatiba. Akitangaza matokeo hayo , mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati, alimtangaza…

Read More