Karibu A24Tv leo October 11 Kutazama kilicho Andikwa Katika Magazeti ya Tanzania Mbele na Nyuma Hii ni A24Tv.
Author: Geofrey Stephen
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Said Mtanda ameiamuru mamlaka ya usimamizi wa vyombo vya usafiri wa moto (Latra) mkoani Arusha kusitisha mara moja utoaji wa leseni za usafirishaji wa Bajaj mpaka pale serikali itakapojiridhisha mahitaji na idadi ya bajaji hizo jijini Arusha. Pia amelielekeza jeshi la polisi mkoani Arusha kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya madereva bajaj jijini hapa ambao wamedaiwa kutumia silaha za mapanga,visu na nondo kuwashambulia madereva wa dalaladala hali ambayo imeibua mgogoro baina yao. Mtanda ametoa kauli hiyo leo katika soko la Kilombero mara baada ya kufika hapo kutatua mgomo wa madereva wa daladala ambao walianzisha mgomo…
Na Mwandishi wa A24Tv Serikali imesema imeweka mkakati wa kufufua vituo vya walimu (Teachers Resource Centers) vya nchi nzima ili kuwawezesha walimu kupata sehemu ya kukutana na kubadilishana uzoefu pamoja na kujiendeleza kwa kujisomea Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda wilayani Bukombe wakati akiongea na walimu wa wilaya hiyo katika kuhitimisha Maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani ambapo amesema mbali ya kufufua vituo hivyo pia inaendelea kutoa mafunzo kazini kwa walimu. Prof. Mkenda amesema walimu wameandaliwa vizuri vyuoni lakini hiyo haitoshi kwa kuwa kila siku mambo yanabadilika na walimu wanapaswa kuendelea kujifunza kila mara…
Karibu Arusha 24Tv leob October 10, 2022,Tuakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania,Hii ni A24Tv .
Mwandishi wetu,Arusha. Wanafunzi wa shule ya msingi Prestige ya jijini Dar es salaam,wameeleza maajabu ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kushauri watoto wa shule nyingine kupatiwa nafasi ya kutembelea hifadhi za taifa na maeneo ya vivutio vya utalii. Wakizungumza na waandishi wa habari, wakiwa na kituo cha Utalii cha Cultural Heritage jijini Arusha, baada ya kutembelea Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, hifadhi ya Taifa ya Tarangire na hifadhi ya taifa ya Manyara, wanafunzi hao wameeleza kuona maajabu mengi katika hifadhi hizo. wanafunzi Kenzi Lewanga,Jaden James, Diana Komu ,Illa Munisi na Ebeneza Charles wamesema hakuwahi kuona kama Tanzania imejaliwa kuwa…
Karibu Arusha24Tv leo October 8 ,2022 Kilicho Andikwa Katika Magazeti ya Tanzania Mbele Na Nyuma Hii ni A24Tv .
Na Mwandishi wa A24Tv Geita . Kamishna wa Tume ya Madini Janet Lekashingo amewataka watanzania kujitokeza kwenye uwekezaji katika Sekta ya Madini kutokana na kuwepo kwa fursa mbalimbali kwenye mnyoyoro wa madini kuanzia uchimbaji, uchenjuaji, biashara ya madini na utoaji wa huduma kwenye migodi ya madini. Lekashingo ameyasema hayo kupitia kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa mubashara na kituo cha televisheni cha TBC1 leo tarehe 08 Oktoba, 2022 kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini katika Viwanja vya Bombambili mjini Geita. Amesema ili kuhakikisha kila mtanzania ananufaika na Sekta ya Madini, Serikali kupitia Wizara ya Madini imeweka mikakati…
*Na WyEST – Mwanza Serikali kupitia Wizara ya Elimu. Sayansi na Teknolojia inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha umahiri katika sekta ndogo ya ngozi. Kituo hicho kinachojengwa katika Chuo cha Teknolojia cha Dar es Salaam (DIT) kampasi ya Mwanza kinalenga kuimarisha mafunzo ya ujuzi juu ya bidhaa za ngozi yanayotolewa katika kampasi hiyo. Akielezea namna wizara ilivyojipanga katika kukiimarisha kituo hicho mara baada ya ya kukagua utekelezaji wa Mradi huo mwishoni mwa wiki Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema shilingi bilioni 19.6 zimetengwa katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/23 kwa…
Karibu Arusha 24Tv Leo Octoba 8 Kutazama Kilicho Andikwa Katika Magazeti ya Tanzania Mbele na Nyuma Hii ni A24Tv .
Na Mwandishi wa A24Tv Geita Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula akiwa ameambatana na Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo ametembelea banda la Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kwenye Maonesho ya Tano ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Bombambili, mjini Geita. Katika Banda la Wizara ya Madini alielezwa kuhusu namna Wizara ya Madini inavyoandaa na kusimamia Sera na Sheria ya Madini pamoja na kanuni zake pamoja na mikakati iliyowekwa katika kuhakikisha watanzania wananufaika na Sekta ya Madini. Katika banda la Tume ya Madini elimu ilitolewa katika…