Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Mirerani Serikali imemtangaza bilionea mwingine mpya wa madini ya Tanzanite, Anselem Kawishe aliyepata mawe mawili yenye uzito wa kilogram 5.22 na thamani ya sh,bilioni 2.25 ambayo yamenunuliwa na serikali. Katibu mkuu wizara ya Madini, Adolf Nduguru alimtangaza bilionea huyo katika mji mdogo wa Mererani katika hafla ya kumtambulisha bilionea huyo mpya na kununua madini hayo na kusema  kuwa atasaidia kuitangaza Tanzania kimataifa na kufanya sekta ya madini hayo kufahamika zaidi duniani. Ndunguru alifafanua  kuwa Kawishe alipata vipande viwili vya madini ya Tanzanite vyenye uzito wa kilogramu 3.74 na kilogramu 1.48. “Kati ya madini hayo mawili, yenye uzito…

Read More

Na mwandishi wa A24Tv .Musoma. Karani wa Sensa ya Watu na Makazi wilayani Bunda mkoa wa Mara amejifungua muda mfupi kabla ya kuanza kazi hiyo, hivyo kulazimika kuondolewa kwenye orodha ya makarani katika wilaya hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Nassari amesema kuwa karani huyo amejifungua usiku wa kuamkia Agosti 23, 2022 ingawa hakuweza kumtaja jina “Tangu tumeanza tumepata changamoto ambayo pia ni baraka kuna karani wetu amejifungua usiku na bahati nzuri alijifungua kabla ya saa sita kwahiyo yeye na mtoto wake pia wamehesabiwa na baada ya hali hiyo kujitokeza tayari karani wa akiba ameshachukua nafasi na kazi inaendelea,”…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi likitarajiwa kuanza hapo kesho,mkuu wa wilaya ya Arusha,Saidi Mtanda amepiga marufuku kwa makarani  na wote watakao ambatana  katika zoezi hilo, kutovaa mavazi yenye mlengo wa vyama vya siasa ili kuepusha kutia dosari zoezi hilo. Akiongea na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake,amesema kuwa maandalizi ya zoezi hilo wilayani humo yamekamilika ,na hatua ya kwanza ya dodoso la kuhesabu linatarajia kuanza saa 6.01 usiku kwa  makundi maalumu yakiwemo ya watoto wa mtaani na waliolala hotelini na nyumba za kulala wageni. Alisema kuwa zoezi la Sensa halina itikadi ya…

Read More