Author: Geofrey Stephen

Na Joseph Ngilisho, ARUSHA MAMIA ya wakazi wa jiji la Arusha wamejitokeza kwa wingi kushiriki maandamano makubwa ya kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi yaliyoandaliwa naTaasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Qadiriya mkoani Arusha ambapo wananchi hao walisema wapo tayari kuhesabiwa. maandamano ya sensa na makazi jijini Arusha Akiongea mara baada ya kupokea ujumbe wa maandamano hayo ,kamishna wa ardhi Mkoa wa Arusha,Essay Mwakatumbula aliwataka wananchi hao kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha zoezi la Sensa ili kila mtu ashiriki kikamilifu zoezi hilo. Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Arusha kutoa ushirikiano wa dhati kwa makarani wa Sensa…

Read More

*DKT. KIRUSWA ATOA MAAGIZO MAHSUSI MTWARA* *Aitaka GST na STAMICO kufanya utafiti wa madini Lindi na Mtwara* *Amuagiza Afisa Madini kutoa elimu ya usalama na utunzaji wa mazingira. Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kuwasadia wachimbaji wadogo wa madini katika mkoa wa Lindi na Mtwara kwa kuwafanyia tafiti za madini ili waweze kuchimba bila kubahatisha. Dkt. Kiruswa ametoa agizo hilo baada ya kutembelea migodi ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu ya Utimbi na Upaso iliyopo katika wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.…

Read More

Na WyEST, MOROGORO Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga (Mb) ameutaka uongozi wa chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi (VETA) Morogoro kuhakikisha ujenzi wa mabweni kwa ajili ya wanafunzi chuoni hapo unamalizika ifikapo tarehe 1 Septemba mwaka huu. Mhe. Kipanga ameyasema hayo alipotembelea chuoni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi huo ulioanza mapema mwezi Februari. Ujenzi wa mabweni hayo ya kisasa umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 400 na ulitarajiwa kukamilika Juni 3, hivyo Naibu Waziri amemtaka mkandarasi (Arusha Technical College) kumaliza ujenzi huo ndani ya siku 15. “Mmefanya kazi nzuri lakini bado mpo taratibu ‘speed’ ni ndogo.…

Read More

Na Geofrey Stephen .Arusha Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanga imefanikiwa kuvuka lengo la kuhudumia jumla ya tani 867,00 ikiwa ni Matokeo ya awali mara baada ya uwekezaji mkubwa wa bandari hiyo Akiongea na waandishi wa habari mapema Leo jijini hapa Msemaji wa bandari hiyo Peter milanzi alisema kuwa uboreshaji huo ulianza toka mwaka 2019. Milanzi alisema kuwa katika mamlaka hiyo tangu kujengwa kwake,Bandari ya Tanga ilikuwa inahudumia shehena katika kina kirefu Cha maji (Stream Operation)eneo la umbali wa kilomita 1.7kutoka gatini kwa sababu ya changamoto ya kina kifupichq maji eneo la gati amabpi kina Cha maji kilikuwa ni mita…

Read More