Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha . Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Alhamisi Januari 09, 2025, amekagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Jiji la Arusha na kuagiza mkandarasi anayesimamia Ujenzi huo kwa awamu ya pili (Phase 2) kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi yake mwezi Mei mwaka huu badala ya mwezi Julai iliyokuwa imepangwa awali. Mhe. Makonda amefikia uamuzi huo baada ya kuelezwa kuwa mradi huo umekuwa ukisuasua bila sababu za msingi ilihali tayari Rais Samia Suluhu Hassan alikwisha idhinisha zaidi ya Bilioni 6 za ujenzi wa awamu ya pili ya Jengo hilo la…

Read More

Na John Mhala,Simanjiro WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} katika kata za Mirerani na Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamesikitishwa na hatua ya Katibu wa Chama hicho ngazi ya Wilaya,Amos Shimba kuingilia kati uchaguzi na kukiuka taratibu za uchaguzi wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani na wameomba viongozi wa juu wa chama kumwondoa katibu huyo kwa kuwa yuko kwa ajili ya maslahi yake na sio ya chama. Uchaguzi wa Mwenyekiti,Makamu na wajumbe wa Mji huo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu na taratibu zote za kichama zilifanyika ikiwa ni pamoja na wanachama kuchukua fomu na kurudisha lakini baadhi ya…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Mkoa wa Arusha utakuwa mwenyeji wa Mkutano mkubwa wa 73 wa Baraza la Kimataifa la viwanja vya ndege kwa Kanda ya Afrika utakaowakutanisha Wataalamu mbalimbali kutoka kwenye mashirika ya ndege, Makampuni na taasisi za Kimataifa za usafiri wa anga zaidi ya 400, ukitarajiwa kufanyika kwa siku saba kuanzia Aprili 24- 30, 2025. Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Kwenye ukumbi wa Mikutano uwanja wa ndege Arusha wakati akizungumza na wanahabari leo Januari 08, 2025, amesema maandalizi ya mkutano huo yanakwenda vizuri, akiushukuru Uongozi wa Mkoa wa Arusha chini ya Mhe. Paul Christian Makonda kwa ushirikiano…

Read More

Na Bahati Siha . Abiria wanaosafiri na Daladala za SanyaJuu Bomang’ombe na Moshi mjini pamoja na SanyaJuu West Kilimanjaro,Wametakiwa kabla ya kupanda kwenye magari hayo wahakikishe wanangalie ubavuni wa magari kumeandikwa nauli halali  wanazopaswa kulipa ili kuepuka usumbufu wakati wa kulipa nauli Haya yamesemwa Paulo Nyello Ofisa mfawidhi wa mamlaka ya udhibiti usafirishaji aridhini( latra) mkoa wa Kilimanjaro, baada ya kuwepo malalamiko kwa Abiria kwamba magari hayo yakiwamo Noah na haice yamekuwa yakipandisha nauli kiholela na kusababisha usumbufu kwa Abiria hao. Akizungumza na waandishi wa habari,kuhusu jambo hilo amewataka Abiria wote kabla ya kupanda kwanza waangalie upande wa ubavuni kumechorwa…

Read More

Na Mwandishi wetu.Dar es salaam Waziri wa Madini, Mh. Anthony Mavunde (Mb) amesena kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na Italia katika kuendeleza sekta ya madini nchini hususani katika teknolojia na mitambo. Ameyasema hayo jana tarehe 06 Januari, 2025 alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, *Mh. Giuseppe Coppola* katika ofisi ndogo za Wizara ya Madini Jijini Dar es Salaam. “Rais wetu *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* ameifungua nchi yetu kwa kuimarisha mahusiano kimataifa kupitia falsafa yake ya 4R. Sisi wasaidizi wake tutaendelea kuhakikisha tunasimamia maono hayo na kujenga…

Read More

Na Mosses Mashala Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa kuna ongezeko kubwa la Wawekezaji katika Sekta ya Utalii hatua inayochangia ukuaji wa Uchumi na Maendeleo ya nchi. Amebainisha kuwa Ongezeko hilo la Wawekezaji pia linachangia Ongezeko la Watalii wanaotembelea nchini hali inayoiimarisha sekta ya Utalii. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipoweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Hoteli ya SSPD-BUHAIRAN iliyopo Bwejuu Mkoa Kusini Unguja Inayomilikiwa na Wawekezaji kutoka Falme za Kiarabu. Aidha Rais Dk. Mwinyi amefahamisha Kuwa Faida za Utalii ni Kubwa kwa nchi katika nyanja mbalimbali za kiuchumi…

Read More

Na Mwadishi wa A24tv .Arusha . Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa kuongeza makusanyo ya kodi kutoka sh. trilioni 22.2 mwaka wa fedha 2021/22 hadi kufikia sh. tril. 27.6 mwaka wa fedha 2023/2024 na kuvunja rekodi ya kukusanya sh. trilioni 16.528 katika kipindi cha Nusu Mwaka wa Fedha 2024/2025 kinachoanzia Julai hadi Desemba Mwaka 2024. Dkt. Nchemba alitoa pongezi hizo, wakati akifungua Kikao Kazi cha siku 5 kinacho Tathmini Utendaji kazi wa Nusu Mwaka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa…

Read More