Author: Geofrey Stephen

Mwandishi wetu, Arusha. Vijiji 20 kati ya 49 wilayani Longido, mkoa wa Arusha, vimetenga eneo la hekta 186.794.2 kwa ajili ya nyanda za malisho ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi. Katika wilaya hii, asilimia 95 ya wakazi ni wafugaji ambao wanamiliki mifugo 918,248 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 hata hivyo hivi sasa wamekosa malisho ya mifugo na maji kutokana na mabadiliko ya tabia nchi. Afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Longido, Nestory Daqarro akizungumza na waandishi wa habari za mazingira kupitia mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa maarifa asilia ambao unafadhiliwa na shirika la maendeleo…

Read More

Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji amewataka wafanyakazi wa Kiwanda cha nguo cha 21th Century kilichopo mkoani Morogoro kuendelea kufanya kazi masaa 24 kwa siku saba kwa kuwa Serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika kiwanda hicho bila kupunguza wafanyakazi au kufunga kiwanda. Waziri Kijaji ameyasema hayo baada ya kufanya ziara katika kiwanda hicho Septemba 17, 2022 ambapo amesema kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi – CCM ya mwaka 2020/220 imeitaka Serikali kuendeleza viwanda vilivyopo na kufufua vilivyokufa ili kuweza kutengeneza ajira za watanzania milioni saba hivyo Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haipo tayari kuona kiwanda hicho…

Read More

mwandishi wetu,.Arusha Viongozi wa mila wa Masai,Barbeig,Akie na wataturu wamesaini makubaliano ya kukubali kushiriki katika mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Tanga. Viongozi hao wamesaini makubaliano na uKampuni ya ujenzi wa boma la mafuta ya EACOP Tanzania hafla iliyofanyika Mountmeru hoteli na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanyakazi na jamii hizo. Akizungumza kwa niaba ya wazee wa mila ,Laigwanani Joseph Laizer amesema wamekubali kuwa na makubaliano na kampuno ya EACOP baada ya kuwashirikisha katika mradi huo. “sisi kama viongozi tumeridhishwa na makubaliano ya leo na tutakwenda kuwa mabalozi kwa wengine”amesema Hata…

Read More

Na Emmanuel mkulu Mkuu wa mkoa wa Njombe anthony_mtaka amesema ifike wakati walimu wasiendelee kutapeliwa na mikopo umiza ilihali walimu wamekuwa muhimu na wenye tija katika taifa. Ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Programu ya benki ya NMB mkoani Njombe ya Walimu spesho ambayo amesema inapaswa iwe suluhisho la utapeli wanaofanyiwa walimu nchini. vicky_bishubo Mkuu wa Idara ha biashara za serikali wa Benki amesema NMB Mwalimu spesho imelenga kuwasaidia walimu kupata mkopo wa kujiendeleza kielimu pamoja na kilimo kwa riba isiyozidi asilimia 9 sambamba na mikopo ya biashara ndogondogo na bima. Amesema benki hiyo inawatambua walimu kuwa ni watu…

Read More

MTAKWIMU mkuu wa Sensa ya watu na makazi nchini ameipongeza taasisi ya dini ya kiislamu ya Twarika Qadiriya, viongozi wa mila na dini mkoani Arusha kwa kuipa heshina serikali kwa kufanikisha kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo na kuifanya  Tanzania kuingia kwenye rekodi ya kidunia. Akisoma taarifa kwa niaba ya mtakwimu mkuu wa serikali,katika hafla ya kumpongez rais Samia Suluhu Hasan kwa kuandaa na kufanikisha zoezi hilo,Seif Kuchengo alisema kuwa taaisis hiyo ya dini ilikuwa mstari wa mbele katika kuratibu na kuyashirikisha makundi mbalimbali katika kuhamasisha zoezi la sensa hapa nchini. Alisema kuwa ofisi ya mtakwimu  mkuu wa serikali haina budi…

Read More

Mwandishi wetu, Monduli AWananchi wa Kata ya Selela na Engaruka wilayani Monduli mkoa Arusha,wameomba serikali kuwasaidia kuweka uzio katika vyanzo vya maji vya asili katika maeneo yao ili visiendelee kuharibiwa na wanyamapori. Kata hizo zina vyanzo vya maji vya asili ambazo zimekuwa zikitoa maji kwa mwaka mzima ambayo ndio tegemeo kwa mahitaji ya Maji katika Kata hizo kwa matumizi ya majumbani,kilimo na mifugo Wakizungumza na waandishi wa habari za Mazingira,kupitia mradi wa Utunzwaji Mazingira kwa maarifa asilia unaendeshwa na taasisi ya wanahabari ya MAIPAC na taasisi ya CILAO mradi ,anaofadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP) kupitia program…

Read More