Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv  Halmashauri ya Arusha DC inatekeleza Mradi wa Ujenzi wa Madarasa 8 katika Shule mpya ya Sekondari ya kata ya Kiutu wilayani Arumeru. Akiongea Wakati Mkurugenzi na viongozi wa Halmashauri hiyo walipotembelea kukagua shule hiyo Diwani wa kata ya Kiutu Malaki Malambo amesema wanaishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za Utekelezaji wa miradi. Amesema kwamba fedha iliyotengwa imetumika vizuri hakuna ubadhirifu na Mkurugenzi ameahidi kuongeza fedha kwa ajili ya kumalizia kazi iliyoanzwa na wananchi ambapo Kuna Madarasa nane hayajakamilika ili January wanafunzi waanze masomo kwa kidatocha kwanza. Ameeleza kwamba serikali kupitia Halmashauri imejielekeza…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha Vijana wa UVCCM  kata ya Levolosi jijini Arusha,wametishia kurejesha kadi za uanachama wa chama hicho na kujiunga na vyama vya upinzani baada kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi uliofanyika katika ofisi ya ccm katika kata hiyo. Wakiongea kwa jazba mara baada ya katibu wa ccm kata hiyo,Aisha Mbaraka kutangaza matokeo,mmoja ya vijana hao,Hasan Ayub alisema kuwa hakubaliani na matokeo hayo kwani wanaami yalipangwa na mshindi aliandaliwa na hakuwa na sifa za kuchaguliwa. Alisema kuwa mshindi aliyetangazwa,Rasul Ramadhani aliyeshinda kwa kura 19 na kuwashinda wenzake, Hasani abdul aliyepata kura moja na Justine…

Read More

Na Geofrey Stephen . ARUSHA. SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imejipanga kwakushirikiana na Wadau  wa sekta binafsi kujadili mapendekezo ya sera, Sheria, Taratibu na kanuni kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji katika sekta ya utaliinchini . Aidha Serikali imejipanga kuhakikisha inatengeneza mfumo wa pamoja wa biashara baina ya wadau wa Utalii ikiwa lengo ni kupata. huduma zote sehemu moja za tozo kodi na malipo yote ya sekta hiyo(Onestop Shop) ili sekta hiyo ichangie kikamilifu katika uchumi Akiongea wakati akifungua mkutano wa Wadau wa sekta ya Utalii (MPPD) Jijini Arusha Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt,Pindi…

Read More

Na Geofrey Stephen , Arusha Mavetenari waliopigana  Vita vya Kagera  (leo) wameadhimisha siku ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kuweka silaha za jadi kwenye bustani ya Mnara wa Mashujaa Jijini Arusha. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Pindi Chana sambamba Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Irrange,Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella,viongozi wa dini pamoja na wananchi. Akizungumza mara baada ya uwekaji wa silaha za jadi ikiwemo ngao,mkuki,shoka na sime,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mongella alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo ndani ya nchi kwakuhakikisha wanalinda amani na kudumisha mashikamano. Ambapo Luteni Mstaafu,Allais Robert ambaye alicha nafasi…

Read More

Moses Mashalla, Diwani wa viti maalumu (CCM) kata ya Mbuguni wilayani Meru mkoani Arusha,Husna Abdallah amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameonyesha kwa vitendo kuwa mwanamke akipewa nafasi anaweza kuitumikia kwa uweledi na kufanya vizuri tofauti na ilivyozoeleka. Diwani huyo alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na waandishi wa habari jijini Arusha huku akisema kuwa Rais Samia amekuwa ni alama na ameonyesha kuwa wanawake wana uwezo wa kuongoza wakipewa nafasi. “Rais Samia amekuwa ni alama kwetu sisi wanawake na ametuoyesha kuwa wanawake wana uwezo wa kuongoza wakipewa nafasi hata za juu “alisema Diwani Husna Alimpongeza Rais…

Read More

Moses Mashalla, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Akheri ,Anael Nasari ameshauri watoto wafundishwe uungwana na maadili mema kuanzia ngazi ya familia ili kukomesha janga la mauaji nchini. Hivi karibuni kumeripotiwa habari za mauaji ya mara kwa mara yanayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini yakiwemo mauaji yanayotokana na wivu wa kimapenzi. Akizungumza katika ibada ya jumapili katika kanisa la KKKT usharika wa Akheri mchungaji Nasari alisema kwamba watoto wanapaswa kufundishwa maadili na uungwana tangu wakiwa wadogo ili wakikua wawe na tabia njema. “Watoto wafundishwe maadili mema tangu wakiwa wadogo ni lazima uungwana uanzie katika ngazi ya…

Read More