Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv. Arusha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika Mashariki (Arusha Bypass km 42.4) uliofanyika Ngaramtoni Jijini Arusha.     Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni, Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Kikanda ya Afrika…

Read More

Na Geofrey Stephen, Manyara. WAREMBO nane kati ya 50 mashuhuri duniani wanaoshiriki shindano la Miss Jungle international 2022 wametembelea mgodi wa madini ya Tanzanite ambao Rais Samia Sulubu alishiriki kutengeneza filamu ya Royal tour . Mgodi huo wa kampuni ya Franone Mining, umepata umaarufu wa aina yake , baada ya warembo hao kuwa na shauku ya kuingia ndani ya mgodi huo kujionea uzalishaji wa madini pekee adimu duniani ili kuitangaza Tanzania na vivutio vyake . Mmoja ya waandaaji wa shindano hilo,Martin Rajabu alisema ziara hiyo imekuja baada ya warembo hao kuiona filamu ya Royal Tour na kuhamasika kuja nchini kujionea…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv. Monduli Hali isiyo ya Kawaida imeibuka katika kata ya Majengo Wilayani Monduli Baina ya vijiji vya Losirwa,Majengo ,Mungere,na Baraka baada ya wakulima kushikilia Mifugo ya wafugaji kwa Madai ya kuwaingiza kwenye Mashamba yao . “Nilipigiwa simu nikiwa Naelekea Mswakini kwenye Mazishi ya wale watoto 5 wa familia moja , ikabidi nifike na kuwapa pole familia , ndugu na Majirani kwanza ili niweze kufika na hapa Majengo kutokana na taharuki baina ya wakulima na wafugaji ninachoweza kusema MARIDHIANO ndiyo Njia pekee ya kupata Suluhu ya kudumu juu ya mgogoro huu naomba viongozi wa Eneo husika kukaa pamoja…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Munduli Mbunge wa jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amefanya ziara ya Kusikiliza kero za Wananchi kupitia Mkutano wa Hadhara katika Kijiji cha Lendikinya Kata ya Sepeko . Awali Akisoma Risala mbele ya Mbunge ,Kereto Moipan Amesema kijiji cha Lendikinya kuna miradi Mingi yanayoendelea ni pamoja na Ujenzi wa Madarasa Shule ya msingi Lendikinya na imekamilika kwa asilimia 99. “Changamoto zipo nyingi ikiwemo Ukosefu wa maji na Hii ni kwa sababu ya Malimbikizo ya bili ya maji kuwa kubwa kwa sababu ya mita Kusoma Monduli na si Kijiji husika, Miundombinu ya bomba mbunge tunaomba marekebisho ya na…

Read More

Na Geofrey Stephen,ARUSHA Warembo kutoka nchi nane duniani wametua nchini kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali hapa nchini na kutangaza utalii baada ya kuvutiwa na filamu ya Royal tour iliyochezwa na rais Samia Suluhu hasan . Pamoja na mambo mengine warembo hao watatembelea na kujionea machimbo ya madini adimu duniani ya Tanzanite yanayopatikana katika mji mdogo wa Mererani,wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara. Akiongea na Vyombo vya habari kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha, baada ya kuwapokea warembo hao,Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Frank Mwaisumbe ,aliipongeza taasisi ya Miss Jungle international kwa kuwaleta warembo hao waweze kujionea vivutio mbalimbali hapa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv .Dodoma   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP) aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi  katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma  Rais wa Jamhuri ya Muungano…

Read More

Na Joseph Ngilisho Arusha Vifo vya utata kwa watoto watano wa familia moja waliofariki kwa kufuatana, wakazi wa kijiji cha Mswakini  wilaya ya Monduli,mkoani hapa,uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa ,marehemu hao walikula ama kunywa kimiminika chenye sumu. Aidha wataalamu wa maabara katika hospitali  ya mkoa Mt.Meru tayari wamechukua Sampuli za marehemu kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali ili kubaini chanzo halisi juu ya vifo vya marehemu. Akiongea na vyombo vya habari wakati wa kuagwa kwa miili ya marehemu wanne katika hospitali  ya Mkoa Mt Meru,jijini hapa,mkuu wa wilaya ya Monduli ,Frank Mwaisumbe alibainisha kuwa uchunguzi wa awali…

Read More