Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Iringa . Serikali imesema itaendelea kushirikiana na kuziwezesha Taasisi za umma na binafsi zinazotoa elimu nchini ili kuhakikisha zinatoa elimu bora inayolenga taaluma na ujuzi. Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda (Mb) leo Julai 14, 2022 mjini Iringa katika maadhimisho ya siku ya Chuo Kikuu cha Iringa ambapo imeitaka Tume ya Vyuo Vikuu nchini kuwa imara katika kusimamia ubora na kuwa haitaingiliwa katika kazi hiyo. Mkenda amesema Serikali pia imekuwa ikiwezesha wanachuo wa Vyuo vyote vikiwemo vya umma na binafsi kupata mikopo bila kubagua. Ameongeza kuwa mbali na mikopo…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. SAKATA la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela kuwaonya  madiwani wa Jiji la Arusha kuacha kutumika limechukua sura mpya  baada ya madiwani kumjibu wakielezea kusikitishwa na hatua yake ya kuwasema mbele ya wataalam huku akiwaombea mabaya. Wakiongea kwa nyakati tofauti diwani wa kata ya Daraja Mbili, Prosper Msofe na diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita walisema kuwa wao ni madiwani kwa awamu ya tatu sasa hivyo wanajielewa na wanapoingia kwenye vikao wanakuwa wanabishana kwa hoja na si majungu kama ambavyo RC Mongela alisema. Diwani wa kata ya Daraja Mbili, Msofe alisema kuwa lengo lao madiwani ambao…

Read More

Na mwandishi wa A24Tv Watu watatu wa familia moja akiwemo mtoto mdogo,wakazi wa kata ya Terat katika jiji la Arusha,wamepoteza Maisha papo hapo kwa ajali baada ya kugongwa na gari wakitoka hospitalini wakiwa wamepakizana kwenye pikipiki. Tukio hilo la kusikitisha limetokea mapema leo majira ya saa 10.45 usiku katika barabara ya bypass katika jiji la Arusha wakati marehemu wakitoka kumpeleka hospitalini, mtoto Ebenezer Mollel mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu aliyekuwa ameandikiwa sindano za masaa. Wengine waliofariki dunia ni pamoja na mama wa mtoto ,Neema Mollel(27) pamoja na mdogo wake ,Agustino Mollel (24) ambaye alikuwa dereva wa pikipiki…

Read More

Na Geofrey Stephen .ARUSHA . Mzee mwenye umri wa miaka 89,Iddy Nzella Maganga ameamua kuzivunja nyumba  zake 2,zenye thamani ya sh,mil 200,zilizopo Ngarenaro NHC, jijini Arusha ,kwa madai kwamba baadhi ya watoto wake wanataka kumdhulumu akimtuhumu mmoja wapo kumfungia kwenye chumba cha giza kwa wiki moja, bila kumpatia chakula wala mahitaji muhimu . Akiongea na waandishi wa habari huku akilia kwa uchungu,Maganga ambaye alifiwa na mke wake wa ndoa , alisema kuwa uamuzi wa kuzivunja nyumba hizo ni baada ya kubaini kwamba baadhi ya watoto wake wakiongozwa na Abdalah Maganga  wanania ovu juu ya mali zake na huenda akafa siku…

Read More

Mwandishi wa A24Tv, Handeni Wakala wa Maji na usafi wa mazingira Vijijini(RUWASA) imeleta faraja Kwa wakazi 17,000 wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga Kwa kuwapata maji safi na Maji ya Mifugo . RUWASA inatumia zaidi ya sh 3 bilioni Kwa sasa katika miradi ya maji Msomera Kwa kusambaza maji na kichimba bwawa kubwa la Mifugo. Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA,Mhandisi Clement Kivegalo akizungumza na waandishi wakati wa kutembelea kijiji Cha Msomera kukagua utekelezaji wa miradi ya maji katika eneo hilo,amesema hadi kufikia mwakani kijiji hicho kitakuwa cha mfano kupata maji safi na salama. Mhandisi Kivegalo amesema hadi sasa utekelezwaji…

Read More

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam, Bw. Jumanne Shauri pamoja na watumishi wengine tisa wa jiji hilo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za Serikali ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 10 zilizokusanywa na hazikuwasilishwa benki kama sheria inavyoelekeza. Agizo hilo linatokana na matokeo ya ukaguzi maalum kuhusu Mapato ya Ndani katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa mwaka wa fedha 2019/2020 hadi 2020/2021 uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Watumishi hao pia wamekabidhiwa kwa Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na…

Read More