Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Munduli . Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amekagua ujenzi wa barabara za Monduli Mjini zinazojengwa kwa Kiwango cha Lami , Pamoja na soko kuu la Monduli. Fredrick Lowassa amesema Fedha zinazotumika katika ujenzi huo ni Fedha zilizotoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwenda kwa Wabunge ambapo yeye ameelekeza Fedha hizo kutumika katika ujenzi wa barabara ndani ya wilayani hiyo. Kwa Upande wake Eng Janeth Mkoreha Meneja Tarura -Monduli, amewahakikishia Wananchi wa eneo hilo kukamilika kwa Barabara hiyo kwa Wakati pamoja na Mitaro kufanyiwa kazi kwa wakati. Ukaguzi huo…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv  Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewataka madiwani wa Jiji la Arusha kuacha kutumika vibaya kisiasa na kwa kupandikizwa unafiki na majungu na mtu moja na kuacha kufanya kazi za maendeleo kwaajili ya wananchi. Mongela ameyasema hayo wakati akizungumza na madiwani wa Jiji la Arusha pamoja na wakuu wa idara wa Jiji hilo katika kikao cha kujadili hoja za mkaguzi mkuu wa serikali CAG. Rc Mongela amesema kwamba Jiji hilo lina kila aina ya vyanzo vya mapato ambavyo madiwani hao wangevitumia vyema wangeweza kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 50 kila mwaka wa fedha lakini…

Read More

Na Joseph Ngilisho, ARUSHA Kamati ya bunge ya bajeti imeitaka mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira (Auwsa), katika jiji la Arusha, kuongeza kasi ya usambazaji wa maji safi na salama katika kata ya Muriet  yenye wakazi zaidi ya elfu 60 huku wanaopata huduma hiyo wakiwa ni 400,000 tu. Mwenyekiti wa kamati hiyo,Daniel Sillo ametoa kauli hiyo wakati alipoongoza ujumbe wa kamati hiyo kwenye ziara ya kutembelea baadhi ya miradi inayotekelezwa na Auwsa jijini Arusha. Akizungumza mara baada ya kutembelea kituo cha kuuza huduma ya maji kilichopo Muriet Sillo alisema kuwa kutokana na changamoto ya idadi ya wakazi kuwa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema Wizara imeandaa programu maalumu ya Suluhisho la Pamoja la Uwekezaji katika Viwanda inayojulikana kama “Total Industrial Solution” inayolenga kuwawezesha wananchi kumiliki viwanda kuanzia vijijini hadi mijini ndani ya miezi sita (6) kwa milioni 6 – 600. Prof. Kahyarara ameyasema hayo Julai 7, 2022 wakati wa kipindi cha Supa Brekfast kinachoendeshwa na Kituo cha Radio cha East Africa, jijini Dar es salaam kwa lengo la kuelimisha umma kuhusu programu maalumu ya Total Indusrtial Solution inayowawezesha wawekezaji wa ndani kumiliki viwanda vidogo na vya…

Read More

Na Geofrey Stephen .Arusha Kamati ya Bunge ya Bajeti imeipongeza Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuhakikisha fedha za Utekelezaji wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19 zinakamilisha ujenzi wa madarasa,maabara na ofisi katika Chuo cha Ufundi Arusha(ATC). Pongezi hizo zimetolewa Jijini Arusha na Mwenyekiti wa kamati hiyo,Daniel Sillo wakati wa ukaguzi wa jengo hilo lililogharimu sh,bilioni 2.27 ambalo limefikia asilimia 90 ya utekelezaji wake. Alisema fedha hizo zimesaidia ujenzi wa madarasa nane yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 880 kwa wakati mmoja,maabara sita zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 270 kwa wakati mmoja ikiwemo ofisi 26 zenye uwezo…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Prof. Godius Kahyarara amesema biashara kati ya Tanzania na Kenya imekuwa zaidi baada ya ya makubaliano kati ya Tanzania na Kenya kuondoa vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru 49 kati ya 64 wakati vikwazo vingine 15 vilivyobaki vinafanyiwa kazi. Prof. Kahyarara ameyasema hayo Julai 6, 2022 wakati wa kipindi cha Morning Trumpet kinachoendeshwa na Kituo cha Televisheni cha Azam, jijini Dar es salaam Amesema katika kipindi cha mwaka mmoja (1) na miezi mitatu (3) cha Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, uwekezaji umeongezeka kutoka bilioni…

Read More