Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha Mwenyekiti wa bodi ya PURA Halfan Ramadhani Halfani amesema wamejipanga vizuri kuongeza wawekezaji kwenye utafutaji kwani kwa mda mrefu walikuwa hawana wawekezaji wa kutosha Amesema sasa hivi wanalo jukumu la kutafuta wawekezaji hususani kwenye hayo maeneo ambayo yako wazi ili kutekeleza hilo kwa sababu taasisi imekua ikifanya matayarisho. Amesema sheria ya mafuta inasema wawekezaji watafutwe kwa njia ya ushindani na sio kwa kuokotwa na ili uwapate kwa ushindani kuna kitu kinafanyika kinaitwa Duru, Duru ni mkutano wa kutangaza maeneo husika ya miradi hivyo wanakuja pale kisha wanapewa utaratibu wa kuandika madokezo ya kuomba miradi. Amesema na Duru…

Read More

Na Mwandiahi wa A24rv . Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Halmashauri za Wilaya 91 nchini zinazokabiliwa na migongano kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu, ambapo imekuwa ikipata madhara mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mashamba hekari mia mbili themanini katika vijiji kumi na nne na watu wawili kupoteza maisha katika kipindi cha mwaka 2023-2024.. Hayo yamebainika na mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Leila Sawe ambaye pia ni Afisa Tawala wa Wilaya hiyo, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya utatuzi wa migongano kati ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu yaliyoendeshwa na Wizara ya Maliasili na…

Read More

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Julai 09, 2024 jijini Dar es Salaam amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya King’s Trust International (KTI) ya Uingereza anaeshughulikia Kusini mwa Jangwa la Sahara Bw. Andre Harriman na kujadili ushirikiano katika kuimarisha mafunzo ya ufundi. Akizungumza katika kikao hicho Prof. Mkenda amesema kutokana na maendeleo na mabadiliko ya teknolojia, juhudi za kuwezesha vijana kuwa na ujuzi utakaowawezesha kushiriki kikamilifu katika sekta mbalimbali za uzalishaji ikiwemo viwanda. “Nimewaambia sisi tunataka kupitia Vyuo vya VETA tushirikiane nao kuimarisha ujuzi katika maeneo mawili, moja kuimarisha ni katika eneo la __Mechatronics_ , tuwafundishe…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . mafunzo ya ujasiriamali wa kuzalisha bidhaa mbalimbali yanayotolewa kwa vijana na walezi ikiwa ni hatua ya kuwezesha jamii kujitafutia kipato ili kumudu malezi ya watoto. vijana na walezi hao ni zaidi ya 1000 mkoani arusha wamekusanywa kwa pamoja na wameanza kupatiwa mafunzo ya ujuzi wa ujasiriamali kupitia shirika la viwanda vidogo dogo nchini sido kwa kushirikiana na taasisi ya sos pamoja na wadau wengine kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiuchumi. meneja wa sido mkoa wa arusha jalphary donge akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo amesema mpango huo wa awamu ya kwanza imejumuisha vijana na…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Vijana katika kata ya Sekei Jijini Arusha wameaswa kuacha matumizi ya dawa za kulevya kwani zinasababisha nguvu kazi ya taifa kupotea, kuwafanya kuwa tegemezi katika familia zao pamoja na kupata madhara mbalimbali ya kiafya. Mkaguzi Kata ya Sekei Jijini Arusha, Mkaguzi wa Polisi (A/INSP) Ditrick Mtuka ametoa wito huo leo Julai 05, 2024 wakati akizungumza na Waraibu wa Dawa za kulevya wanaopatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha. “Vijana mnapaswa kujiepusha na makundi yanayoweza kusababisha kutofikia ndoto zenu kwani makundi hayo yanaweza kusababisha kutumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya”. Alisisitiza Mkaguzi…

Read More

Na Richard Mrusha MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele kutokana na mazingira ya uwekezaji kuboreshwa ,kumeifanya Tanzania kuwa mahali  salama pa kufanya biashara na uwekezaji. Akizungumza leo Julai 3 ,2024 na waandishi wa habari katika banda la JKT kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ,Meja Jenerali Mabele amesema   hali hiyo imefanya watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini. “Naipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira  mazuri ya kufanya biashara na hivyo watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini na hivyo kuifanya Tanzania kuwa…

Read More