Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo nchini (TEMDO) imebuni mtambo mpya wa kisasa wa kuchakata mafuta ya alizeti ambayo yatasafishwa katika ubora kwa kiwango cha juu kwa  ajili ya matumizi ya binadamu. Taasisi hiyo imeutambulisha mtambo huo kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya sikukuu za wakulima nchini (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane eneo la Njiro jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko katika taasisi hiyo,dkt Sigisbert Mmasi alisema kwamba mtambo huo mbali na kuchakata mafuta ya alizeti lakini utayasafisha mafuta hayo na kisha kutawekea virutubisho. Alisema…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv  Utata umeibuka kuhusu ujenzi wa jengo la biashara linalojengwa katika eneo la Ndovu jijini Arusha baada ya halmashauri ya jiji kuzuia ujenzi huo lakini mmiliki wake ambaye hajajulikana amekaidi na kuendelea na ujenzi kinyume cha sheria . Ujenzi huo umeibua hali ya sintofahamu baada ya kujengwa katika mtindo wa maduka ya ndani(Kariakoo )kinyume na sheria za halmashauri ya jiji la Arusha zinazoelekeza majengo yote yanayojengwa katikati ya jiji yajengwe katika mtindo wa ghorofa. Hatahivyo,taarifa za uhakika zinaeleza kuwa mmiliki wa jengo hilo anayetajwa ni kigogo wa Ccm Arusha (jina limehifadhiwa kwa sasa )anatumia nguvu na kivuli…

Read More

Na Geofrey Stephen , ARUSHA Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Arusha(RTO),Solomon Mwangamilo amewaonya vikali wamiliki wa magari watakaoshindwa kuyafikisha magari yao kituoni ili yaweze kukaguliwa na kusisitiza watachukua hatua za kuwanyang’anya leseni za usafirishaji sanjari na kuwafikisha mahakamani. Mwangamilo ametoa kauli hiyo leo wakati akiongoza zoezi la ukaguzi wa magari ya wanafunzi ambalo limeanza leo nchi nzima na kutaraji kukamilika Agosti 13 mwaka huu. Katika zoezi hilo RTO,Mwamgamilo alisema kuwa wataanza kukagua magari yote ya wanafunzi katika wilaya za Arusha,Arumeru,Monduli,Karatu,Longido na kisha Ngorongoro ambapo jumla ya magari takribani 400 yanataraji kukaguliwa. Akiongoza zoezi la ukaguzi RTO Mwangamilo alisema…

Read More

Na Geofrey Stephen . Arusha. Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa maendeleo ya kilimo mifugo na uvuvi yana mchango mkubwa katika upatikanaji wa malighafi za nchi,na kuweza kupata masomo ya nje huku yakisaidia kuchangia ukuaji wa uchumi kwa maendeleo ya nchi. Ameyasema hayo jijini Arusha ,kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha wakati akifungua maonyesho ya kilimo na mifugo nanenane yanayofanyika katika viwanja vya Themi Njiro yenye kauli mbiu ya”agenda 10/30 kilimo ni biashara ,shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo,mifugo na uvuvi”. Alisema kuwa, maonyesho hayo yanatarajiwa kuchangia ukuaji wa mabadiliko kwa wakulima kutoka…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Tanzania na Zambia zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kuibua fursa za biashara na kutatua mara moja changamoto zilizopo na zitakazojitokeza katika uwekezaji na biashara ili kukuza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Hayo yamesemwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) na Waziri wa Biashara na Viwanda wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Chipoka Mulenga walipokutana na kujadiliana kuhusu masuala ya uwezeshaji, biashara na kukuza uchumi baina ya Tanzania na Zambia katika kikao kilichofanyika Agosti 3, 2022, Jijini Dar es Salaam. Mawaziri hao walikutana kufuatia maagizo yaliyotolewa na Mhe. Samia…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha .  ARUSHA Aliyekuwa katibu tawala wa mkoa wa Arusha, Athuman Kihamia amekabidhi ofisi kwa katibu tawala mpya ,Musaa Albano Qkisisitiza kufanya kazi kwa ufanisi Akiwaaga watumishi wa Sekretariet ya mkoa huo dkt Kihamia alisema Kuwa amekuwepo Arusha kwa kipindi kifupi cha miezi 14 tangia ateuliwe wadhifa huo Akiongelea miradi mbalimbali aliyoitekeleza kwa mwaka wa fedha 2021/2022 alisema mkoa ulipokea shilingi bilioni 1.3, kwa ajili ya ukarabati Jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa,ukarabati nyumba ya mkuu wa wilaya ya Arusha,sanjari na ujenzi wa ukuta wake wa uzio  ukarabati ofisi ya mkuu wa wilaya ya Longido ,uchimbaji…

Read More

Na WyEST, ZANZIBAR Wito umetolewa wa kufanya matayarisho ya kutosha ya matumizi ya lugha itakayokubalika kufundishia hasa kwa upande wa walimu na wanafunzi katika ngazi zote za Elimu nchini. Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Mwanahamisi Ameir wakati akifungua kikaokazi cha maoni ya uchambuzi na tathmini ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kinachofanyika Zanzibar. Amesema kuwa matayarisho ya walimu upande wa mafunzo ni ya muhimu katika kuhakikisha walimu wapya wanaozalishwa na ambao wapo tayari kazini wanakuwa na vigezo vinavyotakiwa. “Matayarisho ni ya muhimu kujua vitu kama sifa za wanaoenda…

Read More

Moses Mashalla, Waziri wa madini nchini,Dotto Biteko ametoa kauli kuhusu jiwe la madini ya Ruby lenye uzito wa kilo 2.8 lililoonekana Dubai kwenye maonyesho na kutamka kwamba serikali bado inachunguza Waziri Biteko alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akifungua mkutano wa tatu wa dharula wa baraza la mawaziri wa jumuiya ya nchi zinazozalisha almasi (ADPA) uliomalizika hivi karibuni jijini Arusha. Akihojiwa na waandishi wa habari waziri Biteko alisema kwamba serikali bado inaendelea kuchunguza sakata hilo kwa kushirikisha vyombo mbalimbali serikalini. “Bado tunaendelea na uchunguzi kwa kuwa tunashirikisha vyombo mbalimbali serikalini “alifafanua Biteko Hatahivyo,alisisitiza kuwa hivi karibuni wizara itatoa majibu kuhusu…

Read More