Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen lushoto Watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majangili sugu wamekatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro baada ya kukamatwa na meno ya tembo matano yenye uzito wa kilo 24 yenye tahamani ya mamilioni ya pesa wakisafirisha na usafiri aina ya pikipiki. Kwa mujibu wa Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro,Kamishina Msaidizi wa Polisi,Saimoni Maigwa ilieleza kuwa majangili hayo yakiwa katika usafiri wa pikipiki mbili aina ya King Lion yakifunga kwa ustadi mkubwa nyara hizo za serikali katika mfuko wa salfeti walikamatwa juni 20 mwaka huu majira ya saa 7.30 mchana katika kijiji cha Malolo wilayani Lushoto Mkoani…

Read More

Mwenge wa uhuru umefika jijijini Arusha na kuzindua miradi mbali mbali ikiwemo bara bara miradi binafsi bila kuwepo na kasoro Wakishuhudia miradi hiyo baadhi ya wadau wa maendeleo jijini Arusha akiwemo Eng. kutoka katika kiwanda kikubwa jijini Arusha cha A,Z  Eng. Rwehumbiza amesema Mh Rais anafanya kazi kubwa sana hivyo wao kama sekta biafsi wanashuhudia miradi mbali mbali ikizinduliwa bila kuwepo na kasoro . Matukiokatika picha .mapokezi ya mwenge Picha zikimuonyesha mdau wa maendeleo Eng. Rwehumbiza kutoka kiwanda cha A,Z jijini Arusha akishiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Jijini Arusha Mwisho

Read More

Dar es Salaam. Na Mwandishi wa A24Tv. Mahakama Kuu Dar es Salaam imetupa maombi ya Halima Mdee  na wenzake kutokana na kasoro katika jina la mjibu maombi wa kwanza. Halima ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na wenzake waliomba kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama wa Chadema  katika mahakama hiyo. Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha…

Read More

Na WyEST, DODOMA. Taasisi na Mamlaka za Uthibiti ubora wa bidhaa na huduma zimeshauriwa kuangalia upya sheria wanazozitumia ili kuhamasisha ubunifu na kulinda wabunifu wachanga. Ushauri huo umetolewa Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati akifungua kikaokazi cha kupitia Mwongozo wa Kitaifa wa Kuibua, Kutambua na Kuendeleza Ugunduzi, Ubunifu na Maarifa Asilia wa Mwaka 2018. Prof. Mdoe amesema kazi za taasisi hizo ni kuthibiti ubora kwa maana ya kuhakikisha huduma na bidhaa zinazozalishwa zinakuwa na ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na kusaidia wabunifu wachanga kufikia ubora na viwango vinavyotakiwa ili…

Read More

Na Mwandishinwa A24Tv Arusha  Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima (44) na wenzake wawili leo Juni 22, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita ikiwemo mawili ya utakatishaji fedha. Wengine ni Mariam Mshana (40), aliyekuwa mkuu wa idara ya fedha ya halmashauri hiyo na Innocent Maduhu (40) aliyekuwa mkuu wa idara ya mipango ya uchumi. Mbali na watuhumiwa hao, wengine ni Nuru Ginana na Alex Daniel ambao walikuwa wachumi katika jiji hilo, nao walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kukamilisha dhamana ambapo kupitia mawakili…

Read More