Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Duniani Bw. Houlin Zhao akiwahutubia washiriki wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) katika dhifa fupi ya chakula cha mchana, iliyolenga kuendeleza ushirikiano na wadau wa mawasiliano, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022), tarehe 14 Juni, 2022, jijini Kigali- Rwanda. Tanzania imetumia fursa hiyo kuomba uungwaji mkono ili kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza-Tendaji la ITU kwenye Mkutano Mkuu wa Shirika hilo unaotarajiwa kufanyika Septemba 2022 jijini Bucharest, Romania.

Read More

Na Geofrey Stephen Iringa Mhadhiri wa Shule Kuu ya Habari Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Dk. Darius Mukiza amewapongeza waandishi wa habari za mitandao ya kijamii wanaoshiriki katika semina ya siku mbili ya Sensa ya watu na makazi inayofanyika kwenye Chuo Kikuu Kishiriki Cha Mkwawa mjini Iringa Kwa kazi kubwa iliyofanyika Jana katika kuripoti masuala ya sensa. Amebainisha kuwa mmedhihirisha kwamba ninyi ni muhimu kwenye jamii katika kufikisha ujumbe husika na ndiyo maana Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeanza kuwapa mafunzo nyie Kwa kuona umuhimu wenu. “Jana Kila group la Whatsapp nililoingia au Facebook, Instagram,Blogs,YouTube na mitandao…

Read More

Na Pamela Mollel, wa A24Tv . Iringa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa Mafunzo kwa Waandishi wa Habari wa Mitandao ya Kijamii (Bloggers/Youtubers),kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022. Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza leo Jumanne Juni 14,2022 katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu  Mkwawa Iringa,ambayo yanawakutanisha wanahabari mbali mbali kutoka mitandao ya kijamii nchini. Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Said Ameir amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa uhamasishaji na ushirikishwaji wa makundi maalum vikiwepo vyombo vya habari katika zoezi la…

Read More

Rwanda . Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabiri Bakari (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba (kulia) wakifurahia jambo wakati wa dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022), Kigali – Rwanda. Tanzania imetumia fursa hiyo kuongeza wigo wa mashirikiano katika sekta ya mawasiliano sambamba na kuomba uungwaji mkono kuchaguliwa kama Mjumbe wa Baraza-Tendaji la ITU.

Read More

Dodoma . Serikali inatarajia kufanya marekebisho kwenye sheria ya mifumo ya malipo ya Taifa kwa kupunguza tozo ya muamala wa huduma za fedha katika simu za viganjani. Hayo yamesemwa bungeni leo Jumanne Juni 14, 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akisoma hatuba ya mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/23. Akisoma kipengere cha sheria ya mifumo ya malipo ya taifa, Dk Mwigulu amependekeza kufanya marekebisho kwenye mfumo huo. “Napendekeza kupunguza tozo ya muamala kutoka kiwango kisichozidi Sh7, 000 hadi kiwango kisichozidi Sh4,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa.…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv  Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro pamoja na wataalam kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri wameendelea na ziara ya utatuzi wa kero za wananchi na safari hii wamefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi katika kijiji cha Choda kata ya Mkiwa jimbo la singida mashariki Dc Muro pamoja na wataalamu walilazimika kwanza kufanya mkutano wa ndani na halmashauri ya kijiji cha choda pamoja na kamati ya usimamizi wa mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji na kukubaliana kuwasilisha mpango huo kwenye mkutano wa kijiji siku hiyo hiyo hatua iliyomaliza mgogoro na mvutano wa muda…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Katika jitiada za kulifanya taifa liweze kwendana na kasi ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu Taasisi ya Future STEM Business Leaders kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha ( Arusha Technical College ) wameandaa na kutoa mafunzo ya siku nne kwa wanafunzi wa kidato cha tano na Sita katika Jiji la Arusha kutoka katika shule Saba zilizopo mkoani hapa Hayo yamebainishwa na  kaimu Mkurugenzi mtendaji wa atamizi ya DTBi Dkt Erasto  Mlyuka wakati akifungua mafunzo maalumu ya siku nne ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu  Kwa wanafunzi wa shule za sekondari ambapo alisema kuwa taifa la Tanzania ili likue…

Read More