Author: Geofrey Stephen

Mwananchi wetu. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kupitia Mradi wa Kigoma Pamoja (KJP), limefanikiwa Kuwatajirisha wananchi mkoani Kigoma kwa kununua mazao yao wanayozalisha,kuwajengea maghala na kuwapatia mashine za kuwasaidia kuandaa mazao. Miradi hiyo inatekekezwa Kwa kushirikisha mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) mbali ya WFP, ni pamoja na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (ITC), Shirika la Uendelezaji wa Mitaji la Umoja wa Mataifa (UNCDF) na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO). Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Rashidi Mchatta alisema WFP ni moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yamekuwa na Manufaa makubwa kwa wananchi kwa…

Read More

Na Joseph Ngilisho ARUSHA Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya mjini Kati ,Arusha,limewashukuru na kuwapongeza waumini wake kwa kuinusuru hoteli ya kitalii ya nyota tatu ya Corridor Springs ambayo ni Mali ya kanisa Hilo isiuzwa kutokana na deni kubwa la mkopo lililofikia kiasi Cha sh,bilioni 13.5. Akiwashukuru waumini wa kanisa Hilo waliofurika Katika ibada maalumu ya shukrani iliyofanyika katika kanisa Hilo usharika wa Kimandulu jijini hapa ,Askofu Mkuu Solomon Massangwa alisema waumini wa kanisa hilo wameliheshimisha kanisa kwa kukubali kuchangia na hatimaye kumaliza Deni Hilo. Alisema ilifika mahala walitofautiana na baadhi ya viongozi wenzake huku wengine wakiwa…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Arusha.Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita baada ya ushahidi uliotolewa na Jamhuri kugubikwa na utata, hivyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili na kuwatia hatiani Wakili mauna akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama Mbali na Sabaya wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya .Hata hivyo Sabaya, Nyegu, Aweyo na Msuya wataendelea kubaki mahabusu katika gereza la Karanga kwa kuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi Hukumu hiyo imetolewa…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Bunge la Afrika Mashariki limewapongeza na kuwaenzi Hayati Spika Mstaafu wa Uganda  Mashariki Jacob Oulanya na Hayati Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki kwa kudumisha demokrasia na utawala bora. Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Afrika Mashariki Fatuma Ndangiza amesema kwamba ipo haja kwa Bunge hilo japo hakuna sheria ikawekwa ili kuendelea kuwaenzi viongozi na kujenga Utamaduni huo. Amesema kwamba ukiangalia nchi ya Kenya imekuwa ikisifika kwa katiba bora,hapa utaona mchango mkubwa uliotolewa na Hayati Mwai Kibaki kujenga Demokrasia Wakati wa uongozi wake. Alisema viongozi hao ni wakupigiwa mfano na kuendelezwa kwa Bunge hilo kuendelea kuwaenzi kukumbuka…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha WABUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), wamezitaka nchi wanachama kutimiza wajibu wao wa kuchangia bajeti ya jumuiya hiyo huku wakitilia mashaka kushuka kwa bajeti hiyo wakati idadi ya nchi wanachama ikiongezeka kufikia saba baada ya Jamhuri ya Kidemokradia ya Kongo kujiunga mwaka huu . Waliyasema hayo mwishoni mwa wiki nje ya bunge muda mfupi mara baada ya mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa EAC, Betty Maina kusoma bajeti hiyo ya mwaka 2022/2023 ya dola za Marekani milioni 91.57. Wabunge hao walisema kuwa bajeti hiyo imepungua ikilinganishwa na bajeti ya mwaka uliopita ya dola za Marekani…

Read More