Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua rasmi tuzo za uhifadhi na utalii na kusisitiza kuwa Serikali itendelea kubuni mikakati ya kuimarisha sekta ya Maliasili na Utalii kwa kuwa sekta hiyo ni nguzo muhimu ya uchumi wa Taifa. Amesema hayo leo Desemba 20, 2024 alipozindua Tuzo za Uhifadhi na Utalii katika Ukumbi wa Hoteli ya Mt. Meru jijini Arusha. Tuzo hizo zina lengo la kuchochea ushindani kati ya wadau wa sekta ya maliasili na utalii nchini. Amesema kuwa Sekta ya maliasili na utalii ni chanzo kikubwa cha mapato ya taifa kwa kuwa inahusisha shughuli nyingi za kiuchumi.  “Sekta…

Read More

Na Mwandishi wetu Dar es laam Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesisitiza kuanza kwa wakati kwa Mradi wa Uchimbaji Madini ya graphite (kinywe) na kwa mujibu wa Matakwa ya Sheria ya Madini alipokutana na Mwenyekiti Mpya wa Kampuni ya Evolution Energy Minerals, katika kikao kilicholenga kufahamiana na kujadili maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa kupitia kampuni ya KUDU Graphite. Kampuni ya Evolution Energy Minerals ni mbia na Serikali yenye umiliki wa hisa za asilimia16 zisizohamishika kwenye kampuni ya ubia ya KUDU GRAPHITE inayomiliki mradi wa uchimbaji madini hayo eneo la Chilalo, Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi. Kikao hicho kimefanyika…

Read More

Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amelihakikishia Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF kuwa Zanzibar ipo tayari na inajiandaa vema kufanikisha Mashindano ya CHAN yanayotarajiwa kufanyika Februari mwakani. Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 19 Disemba 2024 alipozungumza na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe aliefika Ikulu Zanzibar . Aidha , Rais Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inaendelea na Ujenzi wa Miundombinu ya Viwanja kwa kasi kubwa ili ikamilike kwa wakati na kufanikisha Mashindani hayo na kuishukuru CAF kwa Kuiamini Zanzibar. Rais Dk.Mwinyi amesisitiza kuwa mbali…

Read More

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wataalam wa ununuzi na ugavi nchini kizingatia misingi ya maadili ya taaluma yao ili kuiwezesha Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake kwa araka zaidi . Mh Dkt. Biteko amesema hayo leo Desemba 17, 2024 wakati akifungua Kongamano la 15 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linaloendelea Jijini Arusha. Amesema wataalam wa ununuzi na ugavi ni muhimu katika kuchagiza maendeleo na Serikali inawategemea ili kufanikisha mipango yake. “ Wataalam wa manunuzi na ugavi mna mchango mkubwa, zaidi ya asilimia 70 ya bajeti nzima ni kwa ajili ya manunuzi, hivyo…

Read More

Hai,Diwani wa kata ya Masama Magharibi Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro,Mashoya Natai amewataka baadhi ya Wasichana Wilayani humo,kuacha tabia ya kuzaa watoto mjini na kuja kuwatelekeza kwa wazazi wao vijijini na wao kurudi mjini ,kwani jambo hilo linawafanya watoto hao kukua katika mazingira magumu na hatarishi Haya yamesemwa na Diwani huyo ,wakati wa sherehe fupi kwa watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu kituo cha lukani Children Center,kituo ambacho Diwani huyo ndiyo kiongozi ambapo watoto hao walipewa chakula na mavazi kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka. Akizungumza kwenye hafla hiyo iliudhuriwa na Wadau mbali mbali wa elimu pamoja…

Read More