Na Geofrey Stephen,ARUSHA Warembo kutoka nchi nane duniani wametua nchini kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali hapa nchini na kutangaza utalii baada ya kuvutiwa na filamu ya Royal tour iliyochezwa na rais Samia Suluhu hasan . Pamoja na mambo mengine warembo hao watatembelea na kujionea machimbo ya madini adimu duniani ya Tanzanite yanayopatikana katika mji mdogo wa Mererani,wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara. Akiongea na Vyombo vya habari kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha, baada ya kuwapokea warembo hao,Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Frank Mwaisumbe ,aliipongeza taasisi ya Miss Jungle international kwa kuwaleta warembo hao waweze kujionea vivutio mbalimbali hapa…
Author: Geofrey Stephen
Na Mwandishi wa A24Tv .Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP) aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma Rais wa Jamhuri ya Muungano…
Na Joseph Ngilisho Arusha Vifo vya utata kwa watoto watano wa familia moja waliofariki kwa kufuatana, wakazi wa kijiji cha Mswakini wilaya ya Monduli,mkoani hapa,uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa ,marehemu hao walikula ama kunywa kimiminika chenye sumu. Aidha wataalamu wa maabara katika hospitali ya mkoa Mt.Meru tayari wamechukua Sampuli za marehemu kwa ajili ya kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali ili kubaini chanzo halisi juu ya vifo vya marehemu. Akiongea na vyombo vya habari wakati wa kuagwa kwa miili ya marehemu wanne katika hospitali ya Mkoa Mt Meru,jijini hapa,mkuu wa wilaya ya Monduli ,Frank Mwaisumbe alibainisha kuwa uchunguzi wa awali…
karibu Arusha 24Tv leo July 20, 2022,Tunakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania,
Mwananchi wetu,Dodoma. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Nchini Vijijini (Ruwasa) imeokoa zaidi ya Sh57.4 bilioni ambayo ilikuwa itumike kugharamia miradi ya maji vijijini. Fedha hizo zimeokolewa katika kipindi cha mwaka 2021/2022 katika miradi ya maji 86 ambayo ilikuwa itekelezwe kwa gharama ya Sh367.3 bilioni. Mkurungezi Mkuu wa Ruwasa, Clement Kivegalo amesema hayo leo Jumanne Julai 19,2022 wakati akielezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali za taasisi na mwelekeo kwa mwaka wa fedha 2022/2023. “Hapo awali ujenzi wa miradi ya maji ulikuwa ukifanyika kwa gharama kubwa ukilinganishwa na uhalisia. Kwa kutambua hilo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 ilifanya majadiliano…
Na Geofrey Stephen Arusha Mzunguko wa Nne 4) wa Mashindano ya Magari ya Afrika unaofahamika kama Africa Rally Champion Ship Mwaka 2022 unatarajiwa kuanzia July 22 hadi 24 mwaka huu katika eneo la Monduli Mkoani Arusha ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa Mashindano hayo kufanyika Nje ya Mkoa wa Pwani. Klabu ya Mbio za magari Arusha kwa kushirikiana na chama kinachosimamia Mashindano ya mbio za magari Tanzania (AAT) kwa pamoja watafanya Mashindano hayo yanayofahamika kwa jina la Tanzania Atlantic Rally ambayo yanajumuisha na ligi ya ndani ya mbio za Magari mzunguko wa Tatu Mratibu alisema.Shindano hayo Satinder Birdi kando…
Na Geofrey Stephen Arusha . Uongozi wa Chuo Kikuu cha Arusha(UOA) umejipanga kukusanya jumla ya kiasi cha sh,50 milioni kila mwezi kupitia programu ya “Book Project” Kama njia mojawapo ya kujikwamua na changamoto ya kifedha. Mbali na programu hiyo pia kimeanzisha miradi mbalimbali ambayo ni ufugaji wa ng’ombe wa maziwa,kuoka mikate,kilimo cha mahindi,pilipili,maharage sanjari na duka kubwa la dawa za binadamu. Chuo Hicho ni miongoni mwa vyuo vinavyomilikiwa na kanisa la Waadventista Wasabato nchini ambapo hivi karibuni kilizuiwa na serikali kudahili wanafunzi kutokana na sababu mbalimbali kabla ya kuruhusiwa kudahili wanafunzi mwishoni mwa mwaka huu . Akizungumza na waandishi wa…
Karbu Arusha 24Tv leo July 19, 2022,Tunakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania,Hii ni A24Tv.
Na Mwandishi wa A24Tv. Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela ameionya Halmashauri ya Arusha DC kuacha utegenezi wa fedha kutoka serikali kuu na kujikita kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo. Mongela Ameyasema hayo kwenye Kikao Maalum cha Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali kilichofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo. Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa Kwa miezi mitatu serikali kuu isipoleta fedha Halmashauri hiyo inaweza kufungwa tafsiri halisi ya CAG asilimia 87 inatoka serikali kuu ambapo Halmashauri hiyo uwezo wake ni asilimia 13 Alisema kwamba Halmashauri ijadili jinsi ya kujenga uwezo wa mapato yake…
Na Geofrey Stephen .ARUSHA Chama cha walimu Mkoa wa Arusha(CWT)kimeitaka serikali kuhakikisha inaboresha maslahi bora ya walimu ikiwemo mazingira mazuri ya kufundishia na kulipa stahiki za walimu kwa wakati pindi wanapohamishwa vituo vya kazi. Akiongea na waandishi wa habari katika kikao kazi cha wafanya maamuzi ngazi ya halmashauri na Mkoa,mwenyekiti wa CWT mkoani hapa,Mwl.Lotta Laizer alisema kuwa pamoja na Rais Samia Sululu Hasani kujitahidi kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo nyongeza ya mshahara lakini bado hangamoto ni kubwa. Laizer alisema kuwa serikali kama mwajiri wa walimu nchini inawajibu wa kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao sahihi kwa wakati jambo litakalo saidia kuongeza…