Na Geofrey Stephen .ARUSHA MAKAMU wa Rais Dkt Philip Mpango amebainisha maeneo sita vinara yanayoongoza kwa rushwa nchini kuwa ni pamoja na sekta ya Ardhi, Polisi,ukusanyaji wa mapato serikali kuu na Halmashauri,utoaji wa Tenda,upat ikanaji wa Leseni na upande wa chaguzi. Dkt Mpango amebainisha hayo jijini Arusha wakati akifungua Mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Takukuru nchini ,na kuitaka Taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini Takukuru, kuongeza nguvu katika maeneo hayo ili kutokomeza vitendo vya rushwa Nchini . Alisema bado malalamiko kwa wananchi kunyimwa haki na kuombwa rushwa ni makubwa ,hivyo alitaka jitihada zaidi kwa Takukuru…
Author: Geofrey Stephen
Karibu Arusva24tv leo December 16 Mwaka 2024 kutazama kilicho andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv. Mwisho .
Siha, Mahakama ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imemuhukumu Wilson Mollel (29),mkazi wa Majengo Sanya juu Wilayani humo,mkulima kwenda jela kutumikia miaka 30 kwa kosa la kumuingilia kinyume na maumbile mwanaume wa miaka (45)ambaye walikuwa wakiishi wote chumba kimoja Hukumu hiyo imetolewa December 12 mwaka huu na Hakimu mkazi mwandamizi wa mahakamani hiyo ,Elibahati Petro. Mwendesha mashitaka wa serikali Kurwa Mungo , amesema tukio hilo lilitokea Junuary 2024,katika eneo hilo la Majengo majira ya jioni ,na kwamba kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 6 akiwamo muhanga mwenyewe ,Daktari pamoja na Mwenyekiti wa eneo hilo Kurwa amesema siku ya tukio mshitakiwa waliondoka…
Na Mwandiahi wa A24tv. Kamanda wa Polisi wilaya ya Arusha (OCD)amepiga marufuku bodaboda kusafirisha wanafunzi pamoja na kuwataka wamiliki wa shule kuacha kusafirisha wanafunzi na mwalimu wa jinsia moja na badala yake kuwepo na jinsia mbili katika kila gari linalobeba wanafunzi . Akizungumza kwa niaba ya (OCD) wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Georgina Matagi ASP Chate ambaye ni mkuu wa Kituo cha Murieti katika hafla ya kuwapongeza wahitimu wa Darasa la Saba ambao wamefanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa darasa la Saba Shule ya awali na Msingi Socrates iliyopo Mkoani hapo,alisema jukumu la jeshi hilo…
Na Mwandishi wetu Geita Kesi namba No. 32126/2024 inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Msingi Waja Josphat masenema anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake imeendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita. Kesi hiyo ambayo imetajwa Mahakamani Desemba 12, 2024, mbele ya Hakimu Mkazi Geita, Cleofas Waane, mashahidi watatu upande wa Jamhuri wametoa ushahidi wao, wakiongozwa na Wakili wa Serikali Verena Mathias. Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Jumatatu Desemba 16, 2024 ambapo itaendelea katika hatua za kusikiliza ushahidi. Itakumbukwa mtuhumiwa alifikishwa mahakamani siku chache baada ya familia ya mtoto anayedaiwa kufanyiwa ukatili huo pamoja na wadau kupaza sauti kutaka mtuhumiwa afikishwe mahakamani, kutokana na…
Karibu Arusha24rv leo December 14 kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni 24tv. Mwisho .
Karibu Arusha24tv kutazama kilicho andikwa katika Magazeti ya leo December 13 mwaka 2024 ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv. Mwisho
Na Geofrey Stephen , ARUSHA CHUO cha Uhasibu Arusha (IAA), kimejipanga kufanya maboresho Makubwa ili kwendana na mabadiliko ya teknolojia kwa kuanza kutumia madarasa mtandao ili kuwezesha kutoa elimu kwa kundi kubwa la wanafunzi maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi Madarasa hayo ya kisasa yatamwezesha mwalimu atakayekuwa kwenye chumba cha darasa katika kampasi zake Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Babati mkoani Manyara na Songea na nchi watakazofungua matawi Sudan Kusini na Comorro kusoma kwa wakati mmoja. Hayo yamebainishwa na Mkuu wa chuo hicho, Profesa Eliamani Sedoyeka wakati alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali…
Na Mwandiahi wa A24tv. Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Taasisi ya Jiolojia ya nchini Uingereza (BGS) zimefanya mazungumzo ya namna bora ya kuanzisha mashirikiano katika tafiti za madini na kujengeana uwezo. Taasisi hiyo ya Jiolojia kutoka nchini Uingereza ikuwa na GST kwa muda wa siku 3 kwa lengo la kujifunzo namna GST inavyotekeleza majukumu yake kwa kufanya ziara ya kujifunza katika Kurugenzi ya Huduma za Jiolojia, Kanzidata na Maabara. Akizungumza wakati wa kuhitimisha, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba amewashukuru wataalamu hao kutoka BGS kwa kuona umuhimu wa kuanzisha mashirikiano na GST na kuahidi…
Na Mashala .Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema malengo makuu ya Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ni kugusa moja kwa moja katika kuboresha maisha ya watu, elimu, afya, ustawi wa amani na haki pamoja na kuwa na Dira jumuishi ambayo itamshirikisha kila mwananchi kutoa mchango wake kwa maendeleo ya Taifa. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipozindua rasimu ya kwanza ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa ndege Mkoa wa Mjini Magharibi, hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali za SMT na SMZ akiwemo…