Author: Geofrey Stephen

Na Joseph Ngilisho,Arusha Kaya zaidi ya 280 zimeathirika  Kisaikolojia baada ya nyumba zao za kuishi na biashara walizojenga katika barabara Mianzini- Timbolo  kuvunjwa na Halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kufanya kuishi kwa kubangaiza . Waathirika hao wamemwomba  Rais Samia Suluhu Hassan aweze kuwasaidia kulipwa fidia ya shilingi bilioni 1.7 baada ya kushinda kesi mahakamani na halmashauri hiyo kushindwa kuwafidia . Nyumba 43 zilibomolewa na wananchi hao wamekuwa wakihangaika kule ya huko kutafuta haki lakini viongozi wa Halmashauri ya Arusha imekuwa ikiziba masikio na kuwaacha kama yatima na wasijue la kufanya. Ombi hilo,wamelitoa kwa Rais Samia baada ya…

Read More

Karibu Arusha 24Tv  Na Geofrey Stephen .Arusha Serikali imesema itachukua na kuyafanyia kazi maoni yote yanayotolewa na wadau wa elimu kuhusu Mapitio ya sera ya elimu ya mwaka 2014 na mitaala ya elimu ili kufanya mageuzi makubwa ya elimu nchini yanayotarajiwa kufanyiwa maamuzi mwakani. Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia ina vipaumbele saba vya Serikali kwenye sekta ya elimu ambavyo ni kufanya mapitio ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014; kuangalia sheria ili iendane na matakwa ya sera; Mapitio ya mitaala ya elimu; Kuangalia idadi ya waalimu, wakufunzi, na wahadhiri wanaohitajika; Ubora wa walimu, Wakufunzi, na Wahadhiri; Kuimarisha…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara upande wa Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Kitovu cha teknolojia za zana za kilimo kitakachoanzishwa Wilaya ya Maswa kitaongeza tija ya uzalishaji wa mazao mbalimbali ya kilimo kuanzia maandalizi ya shamba, uvunaji na uchakataji wa mazao hayo. Dkt Hashil ameyasema hayo Juni 4, 2022 alipotembelea Jengo  la raslimali za kilimo lililopo kijiji cha Mwandete Wilaya ya Maswa litakalotolewa kwa  Kituo cha Zana za Kilimo na Ufundi Vijijini  (CAMARTEC) kwa ajili ya kuanzisha Kitovu cha teknolojia za Kihandisi kitakachotoa huduma za mafunzo na zana za kilimo…

Read More

Na Joseph Ngilisho, Lushoto. Mbunge wa Jimbo la Lushoto,mkoani Tanga,Shaaban Shekilindi ameishauri serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya mchepuko kwa kiwango cha Lami ili kuondoa changamoto ya Mara kwa Mara inayotokana na maporomoko ya mawe kwa barabara kuu inayotoka Mombo Hadi Lushoto ambayo imekuwa kilio kikubwa kwa wafanyabiashara wa mazao na mbogamboga pindi inapoziba. Aidha ameishauri serikali kuangalia namna ya kuwachukukia hatua Kali makandarasi wanaochelewesha miradi mbalimbali ya maendeleo na kusababisha wananchi kuendelea kuteseka kwa kukosa huduma ya usafiri Katika wilaya hiyo. Shekilindi ametoa kilio hicho mwishoni mwa wiki mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa,Sahili Geraruma wakati Mwenge…

Read More

Juni 3/2022 ARUSHA Na Geofrey Stephen WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Pindi Chana ameihakikishia Dunia  sekta ya  utalii nchini  na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)  imefunguka kwa sasa,baada ya kupungua kwa janga la Uviko 19 na kuiomba kutembelea vivutio vilivyopo. Akizungumza jana wakati akifungua maonyesho ya kimataifa ya Utalii ya Karibu- Kili Fair kwa niaba ya Waziri Chana,Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki alisema kwa sasa masharti yamepungua ya janga hilo na maeneo mengi yanafikika kiurahisi. “Maonyesho haya watasaidia kutangaza Dunia kuwa sasa utalii umefufuka tena kwa Tanzania na nchi za EAC na natoa wito watu wote…

Read More

Fedha za Mapango wa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhiki ya Uviko 19 zaidi ya shilingi milioni 782.5 zimeweza kuwanufaisha wakazi zaidi ya 11,048 kupata maji Safi na salama katika vijiji 11 vya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga. Hayo yalisemwa Jana na Kaimu Meneja  wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa Tanga(RUWASA),Injinia Erwin Sizinga mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa,Sahili Geraruma muda mfupi kabla ya kuzindua miradi hiyo katika Halmashauri ya Bumbuli na Halmashauri ya Lushoto. Injinia Sizinga alisema fedha za Uviko 19 zilisaidia kupata Mkandarasi kampuni ya Mbesso Construction ya Jijini Dar es Salaam ambaye alisema kuwa mradi…

Read More