Author: Geofrey Stephen

Na Bahayi Hai. Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda amefariki dunia katika ajali ambayo imetokea eneo la Njia panda ya KIA, Wilaya ya Hai, akiwa kwenye ziara Mkoani humo. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo na kwamba ajali hiyo imetokea muda wa saa 8 kuelekea saa 9 mchana leo, Juni 18, 2024. “Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,”amesema RC Babu Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi…

Read More

Hai Sheikh wa mkoa wa Kilimanjaro Shaabani Mlewa,Amewataka waumini wa Dini ya kiislamu kujitokeza katika uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa kuchangua Viongozi wenye sifa na waadilifu ili kuwa maendeleao Pia amewataka kujitokeza na kujiorodhesha katika Daftari la wapiga kura muda ili uwawe na sifa ya kuwa mpiga kura. Akizungumza Mara baada ya kuswali Idd El hajj kimokoa katika msikiti wa Safii Bomang’ombe Wilayani Hai mkoani hapa ,Amesema mwaka huu ni wauchaguzi wa Serikali za mitaa muhimu kujitokeza kugombea na kama hautaki kugombea basi tutafutie mtu mwenye sifa za kugombea , muadilifu kwani nchi hii inataka watu wenye sifa ya…

Read More

Hai, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Wangub Maganda ,ametaka Wananchi Wilayani humo kuanzia miaka 18 kujitokeza kwa wingi katika Maeneo yao muda utakapofika wa kujiorodhesha kwenye Daftar la wapiga kura ili wawe na sifa ya kupiga kura Aidha amesema utakapofika wakati wa kupiga kura za maoni chagueni mtu ambaye atauzika ,anayekubalika na Jamii. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti huyo wakati wa mkutano mkuu wa CCM kata ya KIA wakati wa uwasilishaji utekelezaji wa ilani ya chama hicho mwaka 2020 na 2024 uliofanyika ofisi ya Kijiji cha Sanya Station , ambapo amesema ili uwe na sifa ya…

Read More

Na Beatus Maganja, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Mej. Jen. (Mstaafu) Hamis Semfuko amesema Bodi anayooingoza imejipanga kuja na mipango madhubuti ya kuifanya Hifadhi ya Pande iliyopo Jijini Dar es Salaam kuwa kivutio kikubwa kwa watu waishio ndani na nje ya Jiji hilo. Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara iliyofanyika Juni 13, 2024 hifadhini humo, Semfuko amesema Bodi yake imedhamiria kuwafanya watanzania waione Hifadhi ya Pande kuwa ni sehemu ya kipekee kwa ajili ya kustarehe na kupumzisha akili zao, na kwa kuanzia imeanzisha bustani wa wanyamapori hai ndani ya hifadhi hiyo ambao wako huru…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Mtafiti wa Sokwe mtu (Sokwe) kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Bw. Simula P. Maijo amesema Sokwe ni mnyama adhimu Tanzania ambaye kwa asili anapatikana katika mikoa ya Kigoma (Gombe na Mahale), Mkoa wa Katavi ( Misitu ya Tongwe) na baadhi ya maeneo ya Rukwa (Kalambo). Pia, Tanzania ina Sokwe katika hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo ambao siyo wa asili katika maeneo hayo. “Kwa Tanzania Sokwe wanakadiriwa kuwa chini ya 2500 kwa idadi. Na kati ya idadi hiyo, zaidi ya asilimia 75% wanapatika na na kuishi katika maeneo ambayo yanapatikana nje ya…

Read More